Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kiswahili kinahitaji kusanifisha upya.Jadili kauli hii

      

Kiswahili kinahitaji kusanifisha upya.Jadili kauli hii

  

Answers


Faith
Kiswahili kinahitaji kusanifishwa upya kwa kuwa;
• Kuna haja ya kutumia mtindo mmoja wa kuandika kila neno katika Kiswahili. Kuna maneno yanayoleta tatizo kwa kuwa inaweza kuandikwa kwa mitindo miwili kwa mfano;
Dereva- dreva
• Msamiati wa kilahaja unaotumiwa na kukubaliwa katika utunzi wa ushairi umepenya katika riwaya na ni tishio kwa Kiswahili.Imeonekana kuwa waandishi tajika wameweza kutumia lahaja hizi na kwa hivyo Kiswahili kinafaa kusanifishwa upya.
• Kiswahili kinafaa kusanifishwa upya ili kuhakikisha kuwa sarufi imesanifishwa kwa kuchapisha vitabu vya sarufi.
• Ili kukabiliana na Sheng'- Sheng' ni lugha ya inayotumiwa mitaani hasa na vijana.Watu wengi wanatumia lugha hii na lugha ya kiswahili na wanapozungumza wao hufikiri wametumia Kiswahili.Sheng' huathiri lugha ya Kiswahili kwa hivyo inafaa kusanifishwa upya.
• Ili kupata istilahi mwafaka tunazohitaji kutumia katika nyanja mbalimbali kama vile uwanjani,teknolojia na sayansi.
• Ili kudumisha mawasiliano ya kitaifa na kimataifa.Nchi zinazohusika katika usanifishaji lazima iwajuze na kuwajumlisha nchi zingine katika usanifishaji ili kuwe na maelewano na kukubaliwa kwa istilahi za kiswahili. Kwa mfano nchi ya Tanzania inafaa kuhusisha nchi zote za Afrika Mashariki katika usanifishaji.


Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:56


Next: Tathmini mchango wa kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(K.K.A.M) katika kusanifisha lugha ya Kiswahil
Previous: Tathmini kiwango cha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vituo vya redio na magazeti ya Tanzania

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions