Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Baada ya mataifa ya Afrika Mashariki kupata uhuru.Kiswahili kilikuzwa na kuendeleza katika nyanja mbalimbali za kitaifa na kimataifa.Kila taifa lilibuni sera zake kuhusu matumizi ya Kiswahili katika miktadha tofauti tofauti. Kenya, Tanzania zilijaribu kukikuza na kuendeleza kwa kutumia katika biashara, elimu, siasa na vyombo vya habari. Kutokana na juhudi hizi Kiswahili kimeenea sana kiwango cha kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi.
Katika vyombo vya habari, sio vyote katika nchi hizi hutumia lugha ya Kiswahili. Kwa zenye zinatumia lugha hii hukuza na kuendeleza kwa kiwango kikubwa. Dhima kuu ya vyombo vya habari ni kutoa huduma kwa jamii. Huduma hizo ni kama vile kuifahamisha na kuihamasisha jamii kuhusiana na matukio mbalimbali yanayojiri kila siku. Katika mkabala huo hujaribu kutumia lugha husika ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wanajamii wanaolengwa. Hata hivyo ,hujaribu kutumia lugha sanifu ili kuhakikisha kuwa matumizi yake yanakuzwa kwa kuzingatia kanuni zake za kisarufi na fasihi vilevile.
Howard(2002) na Kandagor (2011) wanadai kuwa katika hali ya kawaida vyombo vya habari hufikia hadhira kubwa na huwasilisha ujumbe wa aina tofauti tofauti kuhusu nyanja tofauti za maisha.Vilevile huwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.Vyombo vya habari vina uwezo mkubwa wa kuendeleza au kuharibu lugha. Kiswahili kinanufaika sana kutokana na jukumu muhimu linalotekelezwa na vyombo vya habari katika harakati za kukikuza, kukiendeleza na kukisambaza. Nchini hizi redio na gazeti viko katika mstari wa mbele katika kukiendeleza Kiswahili.
Vyombo vya habari ni zao la maendelezo ya sayansi na teknolojia ambalo limeadhiri na kuibadili mwelekeo wa jamii nyingi duniani. Kuanzishwa kwa redio na magazeti ya Kiswahili si tu kwamba kumeisaidia katika kuikuza Kiswahili bali kimetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii moya;yaani jamii ya wasemaji Kiswahili katika nyanja zote za maisha.Katika jamii ya sasa utandawazi ni jambo lisiloepukika. Simala(2004/2006)anaeleza kuwa kimsingi utandawazi unarejelea jumla ya maisha ya watu duniani.
Mwanasoko(1995) anadai kwamba vyombo vya habari katika kufikisha ujumbe kwa usahihi kwa watu hutegemea sana uelewa nzuri wa istilahi zinazohusiana na mada anuwai wanazozishughulikia waandishi na watangazaji wa habari.Kwa upande mwingine anasisitiza kuwa ujuzi na ufahamu wa lugha ni kipengele muhimu katika uundaji na usambasaji wa habari katika vyombo vya habari.
Kwa ujumla jambo linalokubaliwa na watu wengi kutoka nchi hizi kwamba vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza Kiswahili.Hata hivyo ni vema kutaja kwamba vyombo vya habari vina umuhimu na uwezo wa kuendeleza,kukwamisha au hata kupotosha lugha husika
Titany answered the question on December 6, 2021 at 10:01
- Kiswahili kinahitaji kusanifisha upya.Jadili kauli hii(Solved)
Kiswahili kinahitaji kusanifisha upya.Jadili kauli hii
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Tathmini mchango wa kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(K.K.A.M) katika kusanifisha lugha ya Kiswahil(Solved)
Tathmini mchango wa kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(K.K.A.M) katika kusanifisha lugha ya Kiswahil
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza ni kwa nini lugha ya Kiswahili ilisanifishwa wakati wa ukoloni(Solved)
Eleza ni kwa nini lugha ya Kiswahili ilisanifishwa wakati wa ukoloni
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kwa msingi wa kusanifisha lugha ya kiswahili na wala sio kimvita au kiamu(Solved)
Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kwa msingi wa kusanifisha lugha ya kiswahili na wala sio kimvita au kiamu
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.(Solved)
Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.
"Malimwengu yote yawatiile
na dunia yao iwaokele
wachenenda zitea zao zilele
mato matumizi wayatumbiye"
Jawabu;
"Ulimwengu wote uwatii
na dunia yao iwaokoe
Wataenda Vita vyao vile macho yaliyofumbwa wayafumbue"
Hii ni lahaja ya kiamu.
(b) Kwa kutoa mifano kutoka ubeti huo na kwingineko ,zibainishe sifa Tisa zinazotofautisha lahaja hiyo na kiswahili sanifu.
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Huku ukitoa mfano mwafaka bainisha tofauti za kifonolojia na kimofolojia katika lahaja za kimvita ,kivumba na kiswahili sanifu(Solved)
Huku ukitoa mfano mwafaka bainisha tofauti za kifonolojia na kimofolojia katika lahaja za kimvita ,kivumba na kiswahili sanifu
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza matatizo mbalimbali yanayowakumba watafiti wanapojaribu kuhesabu na kuainisha lahaja za lugha(Solved)
Eleza matatizo mbalimbali yanayowakumba watafiti wanapojaribu kuhesabu na kuainisha lahaja za lugha
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Taja lahaja zinazopatikana katika lugha yako iwapo zipo kisha eleza jinsi zilizuka(Solved)
Taja lahaja zinazopatikana katika lugha yako iwapo zipo kisha eleza jinsi zilizuka
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Fafanua sababu zilizotatiza kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Uganda kabla ya uhuru(Solved)
Fafanua sababu zilizotatiza kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Uganda kabla ya uhuru
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Wajerumani na Wamishonari walikuwa marafiki wakubwa wa Kiswahili? Jadili kauli hii uku ukieleza jinsi walivyochangia maenezi ya lugha hii katika afrika mashariki(Solved)
Wajerumani na Wamishonari walikuwa marafiki wakubwa wa Kiswahili? Jadili kauli hii uku ukieleza jinsi walivyochangia maenezi ya lugha hii katika afrika mashariki
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Sera ya lugha ya uingereza ilitatiza kukua nakuenea kwa Kiswahili nchini Kenya “ jadili kauli hii kwa tafsili(Solved)
Sera ya lugha ya uingereza ilitatiza kukua nakuenea kwa Kiswahili nchini Kenya “ jadili kauli hii kwa tafsili
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza kwa nn wafanya biashara waarabu walfanikiwa sana kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko Kenya(Solved)
Eleza kwa nn wafanya biashara waarabu walfanikiwa sana kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko Kenya
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya(Solved)
Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika(Solved)
Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo(Solved)
Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu(Solved)
Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya mseto(Solved)
Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya mseto
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Orodhesha maneno mengine ya Kiswahili yakiyokopwa kutoka lugha mbalimbali za kigeni na uzitaje lugha hizo(Solved)
Orodhesha maneno mengine ya Kiswahili yakiyokopwa kutoka lugha mbalimbali za kigeni na uzitaje lugha hizo
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Je kwa maoni yako, unafikiri asili ya neno 'Kiswahili' ni nini?(Solved)
Je kwa maoni yako, unafikiri asili ya neno 'Kiswahili' ni nini?
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)