Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taja vituo mbalimbali vya redio nchini Kenya ambavyo hutangaza kwa Kiswahili kisha ueleze ni vipi lugha hii inaendelezwa katika vituo hivyo

      

Taja vituo mbalimbali vya redio nchini Kenya ambavyo hutangaza kwa Kiswahili kisha ueleze ni vipi lugha hii inaendelezwa katika vituo hivyo

  

Answers


Faith
Vyombo vya habari ni asasi muhimu sana katika kukuza na kueneza lugha yoyote ile. Katika nchi ya Kenya kuna vyombo vya habari vinavyotoa huduma anuwai kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya wateja wao. Hivyo basi vinalazimika kuhakikisha kuwa wateja wao wananufaika kutokana na huduma mbalimbali ambazo hutolewa kila kukicha. Redio na magazeti yanatathmini juhudi za kukuza na kueneza Kiswahili nchini Kenya. Vituo vya redio nchini Kenya ni kama:
Idhaa ya redio KBC(Kenya broadcasting corporation)
Hiki ndicho kituo cha kwanza katika taifa la Kenya. Azma kuu ikiwa ni kufahamisha wananchi kuhusu yale yanayotendeka kila uchao ndani na nje ya nchi. Lugha zinazotumiwa katika kituo hiki ni Kiswahili. Makala haya yanajikita katika matangazo na vipindi vinavyoangazwa kwa Kiswahili mbali na kuwa chombo cha kuwafahamisha idhaa hii pia imetumika kuwaelimisha wanafunzi wa shule za msingi na upili kupitia vipindi vinavyotolewa na taasisi ya elimu nchini Kenya (KIE). Mojawapo kati ya masomo yanayofundishwa ni Kiswahili yaani isimu na fasihi.
Kipindi ya mafunzo au masomo kwa wanafunzi.Kipindi hiki hujulikana kama KBC broadcast to schools,ambayo huandaliwa na KIE na kutangazwa hewani na shirika la taifa la KBC.Taasisi hiyo huandaa mafunzo katika masomo anuwai.
Kwa kiasi kikubwa vipindi hivi vya mafunzo ya Kiswahili huchangia katika kukuza na kuendeleza Kiswahili. Mbali na kunufaika kiakademia wanafunzi na walimu wanakuza kiwango kikubwa cha misamiat. Kwa jinsi hiyo idhaa hii ya redio KBC inakuza na kuendeleza Kiswahili.

Idhaa ya redio citizen.
'Citizen' ni jina lenye asili ya kiingereza lenye maana ya mwananchi.Katika Kiswahili jambo hili linaashiria kuwa ni idhaa ya kila mtu kwa kuwa husikika karibu pembe zote za Kenya.Idhaa hii imechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kueneza Kiswahili kwa njia zifuatazo.

Kipindi cha Rusha Roho
Hupeperushwa kila jumapili .Hiki ni kipindi cha muziki wa taarabu ambacho aghalibu huratibiwa na watangazaji walio na ufahamu kuhusu utamaduni wa Waswahili katika kipindi hiki.Masuala Mbalimbali yanayohusu utamaduni wa Waswahili hupeperushwa.

Bahari ya lugha.
Hupeperushwa kila jumamosi kati ya saa tatu na saa tano asubuhi.Mbali na waratibu wa vipindi ambao ni waajiriwa wa idhaa ya Redio Citizen, wataalamu na mabingwa wa Kiswahili hualikwa studioni ili kusaidia katika kufundisha Kiswahili kwa wakenya wote.Kwa upande mwingine wasikilizaji hupewa nafasi ya kuuliza maswali kutokana na Mambo waliyoyapata kwa kutumia ujumbe mfupi au kupiga simu moja kwa moja.

Chemsha bongo
Ni kipindi ambacho hutokea kila jumapili kati ya saa kumi na saa mbili jioni hadi saa moja usiku.Katika kipindi hiki waratibu wa kipindi huwauliza wasikilizaji maswali kisha wakajibu kwa kutuma ujumbe mfupi au kupiga simu.Baadhi ya vipengele vinavyojadiliwa ni masuala ya kisiasa ,ufahamu wa lugha ya kiswahili na michezo.Mbali na waratibu wa kipindi pia wasikilizaji huuliza maswali.
Kwa kiasi kikubwa vipindi hivi vimechangia katika kukuza na kuenea kwa lugha ya kiswahili nchini Kenya.Hii ni kwa sababu vipindi hivi vinaweza kuwafikia watu wengi sana wanaoishi katika sehemu Mbalimbali nchini. Kwa jinsi hiyo Kiswahili hukuzwa na kusambazwa katika sehemu mbalimbali nchini Kenya

Titany answered the question on December 6, 2021 at 10:09


Next: Tathmini kiwango cha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vituo vya redio na magazeti ya Tanzania
Previous: Eleza jinsi sera ya lugha nchini Tanzania ilivyosaidia lugha ya Kiswahili kupiga hatua kubwa katika matumizi nchini humo kuliko nchini Kenya baada ya uhuru

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions