Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza jinsi sera ya lugha nchini Tanzania ilivyosaidia lugha ya Kiswahili kupiga hatua kubwa katika matumizi nchini humo kuliko nchini Kenya baada ya uhuru

      

Eleza jinsi sera ya lugha nchini Tanzania ilivyosaidia lugha ya Kiswahili kupiga hatua kubwa katika matumizi nchini humo kuliko nchini Kenya baada ya uhuru

  

Answers


Faith
a) Wizara ya elimu na utamaduni ilianzisha kamati maalum iliyojishughulisha na SoMo la kiswahili na pia walimu wa lugha hii. Sehemu ya utamaduni nayo ilichukua nafasi ya kuzitalii tanzu za fasii simulizi Kama vile nyimbo, ngoma na ngano, na baadaye kuzitafsiri kwa kiswahili ili wananchi wengi waweze kuzifahamu.
b) Mara tu baada ya Uhuru, Sheik Amri Kaluta Abeid aliunda kamati ya wataalamu kumi wa kiswahili ili kutafsiri Sheria kwa kiswahili. Kutokana na juhudi za wanakamati hao, kamusi rasmi ya Sheria ilitolewa mwaka wa 1967.
c) Taasisi ya elimu ya Tanzania iliyoanzishwa mnamo mwaka 1966 na kazi yake ni kukiza na kutathmini mitaa. T.E.T huandaa miongozo ya masomo pamoja na vifaa Kama vile vitabu vinavyohitajika kutumika katika shule za msingi, secondary na vyuo vya ualimu.
d) Taasisi ya elimu ya watu wazima iliundwa mwaka wa 1963 Kama chombo Cha kutoa masomo ya jioni kwa mwananchi pamoja na kufundisha masomo mengine,Taasisi hii imekuwa ikifundisha watu wazima stadi za kusoma na kuandika kiswahili.
c) Baraza la kiswahili la Tanzania, shirika la umma likiloanzishwa na serikali mnamo mwaka 1967 ili kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania pamoja na kufuatilia naendelea yake katika nchi za nje.
f) Chama cha usanifu wa kiswahili na ushairi Tanzania kiliundwa kuimiza uigizaji na Mambo mengine ya utamaduni, kuandika kamusi na sarufi iliyofaa zaidi kuliko zile zilizokuwa zikitumika wakati huo, kuamsha ari ya kuandika vitabu kuhusu mada mbalimbali za Kiswahili pamoja na ushairi na kutafta mbinu za kuchapisha kazi zao.
g)Taasisi ya Kiswahili na lugha za kigeni ilianzishwa mnamo mwaka 1979 kisiwa Zanzibar. Mbali na kufunza kiswahili kwa wageni na lugha za kigeni kwa wenyeji, kilijishughulisha na utafiti kuhusu lahaja na hadhi zake, muundo wa lahaja hizo, matumizi yake na hali yake ya baadaye kisiwani Zanzibar.
h) Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili (Tuki) ilijishughulisha na utafiti wa kiswahili katika nyanja zake zote pamoja na ufundishaji na usambazaji wake.
I) Idara ya Kiswahili- chuo kikuu Cha Dar es Salaam, kiliundwa na wanafunzi waanzilishi wa Idara ya kiswahili ambao walikusaidia kuleta mapinduzi katika kuendeleza kiswahili na kupinga madai kwamba kiswahili ni lugha duni.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:09


Next: Taja vituo mbalimbali vya redio nchini Kenya ambavyo hutangaza kwa Kiswahili kisha ueleze ni vipi lugha hii inaendelezwa katika vituo hivyo
Previous: Tathmini mchango wa tume ya Mackey (1981) na time ya Koech (1999) katika kustawisha Kiswahili nchini Kenya

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions