Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Juhudi za kuendeleza kiswahili nchini Uganda baada ya uhuru bado hazijafaulu" jadili kauli hii

      

Juhudi za kuendeleza kiswahili nchini Uganda baada ya uhuru bado hazijafaulu" jadili kauli hii

  

Answers


Faith
Ingawa rais Milton Obote wa U.P alijusudia kukiteua Kiswahili kuwa lugha ya taifa, alipingwa na chama cha Kabaka Yekka ambacho kilipendelea lugha ya kiganda. Aidha makabila mengine pia yalitaka lugha zao zitumike serikalini na hali hii imezidisha ukabila nchini humo.
Baada ya rais Idi Amin kuipinfua serikali mwaka wa 1971, alijaribu kuleta umoja kwa kuamuru kwamba kiswahili kitumike kama lugha pekee ya yaifa . Aliwatumia wanajeshi wake kutekeleza Amri hii kimabavu , Jambo ambalo liliwafanya waganda wengi kukichukia kiswahili kufikia Sasa.
Chuo kikuu Cha Makerere ambamo kiswahili hufundishwa katika kiwango cha shahada ya Kwanza , Mara nyingine hakuna wanafunzi wa kijisajili. Pia wahadhiri hawapatikani kwa urahisi na lugha ya kiswahili Haina maabara ambayo ni muhimu katika kuwafunza wanafunzi lugha kwa Mara ya Kwanza.
Baraza la mitihani la taifa linakitambua kiswahili Kama Somo la kutahiniwa katika shule za upili lakini hakifunzwi katika shule za msingi.
Takriban lugha kumi na mbili ya kienjeji hutumika katika redio Uganda, lakini kigannda na kingereza ndizo hutumika Sana kwenye runinga.
Kiganda na kingereza hutumika Sana zaidi magazetini kuliko lugha zingine. Hivi sasa hakuna gazeti wala jarida lolote la Kiswahili nchini humo.
Idara ya jeshi, polisi na magereza pia husaidia kukiza kiswahili ata ingawa ni Kiswahili Cha mazungumzo tu. Maoni ya wasomi wengi wanaotoka Uganda, Kama vile Senoga-zake ni kwamba waganda wengi wanakichukia kiswahili kwa sababu wanakinasibisha na idara hizi ambazo Zina sifa mbaya Sana. Kwa mfano Senoga-zake anasema kwamba mwanajeshi anapotaka kumwua mtu, lugha anayotumia ni kiswahili.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:22


Next: Eleza ni vipi sheng' inavyoathiri maendeleo ya kiswahili nchini Kenya na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kukabili
Previous: Kwa kutoa mifano, fafanua mbinu mbalimbali zinazotumiwa kuundia msamiati na istilahi za Kiswahili

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions