Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwa kutoa mifano, fafanua mbinu mbalimbali zinazotumiwa kuundia msamiati na istilahi za Kiswahili

      

Kwa kutoa mifano, fafanua mbinu mbalimbali zinazotumiwa kuundia msamiati na istilahi za Kiswahili

  

Answers


Faith
a) Uradidi
Ni urudiaji wa neno zima au sehemu ya neno ili kupata neno jipya lenye maana tofauti.mfano
Mbele - kimbelembele
Tinga- tingatinga
b)Ufupishaji
Ufupishaji wa akronimu ni uunganishaji wa sehemu ya kwanza ya maneno mawili au zaidi.mfano
UKIMWI- ukosefu wa kinga mwilini
CHAKITA - chama cha kiswahili cha taifa
C)Kutafsiri
Katika mbinu Hii ,maana ya neno lililokopwa hutolewa kwa lugha nyingine,yaani lugha pokezi.mifano
Right Angle - pembemraba
Armyworm- Viwavijeshi
Absurd - Ubwege
d)Utohozi
Ni kuyapatia maneno yaliyokopwa matamshi na maandishi ya lugha pokezi.mifano
Office - Ofisi au Afisa
Bicycle - baiskeli
e)Uhulutishaji
Ni kuunganisha visehemu mbalimbali vya maneno mawili au zaidi ili kubuni neno moja la mchanganyiko.Kwa kawaida ,sehemu ya mwisho ya neno la pili.mifano
Chajio - chakula cha jioni,yaani supper
Chamcha - Chakula cha mchani,yaani lunch
Msikwao - mtu asiye na kwao,yaani 'vagrant'
F) Unyambuaji
Ni upachikaji wa viambishi awali au viambishi tamati kwenye mzizi wa neno ilu kuunda maneno tofauti.mifano
Pika - m + pishi 'mpishi'
Tega - m+tego. 'mtego'

Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:24


Next: Juhudi za kuendeleza kiswahili nchini Uganda baada ya uhuru bado hazijafaulu" jadili kauli hii
Previous: Huku ukitoa mifano jadili matatizo yanayokumba uundaji wa istilahi za kiswahili na jinsi yanavyoweza kutatuliwa

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions