Ili kuelewa kazi zilizofanywa na waswahili, tunaangalia na kujadili kategoria za kifasihi kama
vile visasili, hurafa, nyimbo za kale, mashairi, ngano, vitendawili n.k. vipera hivi vya fasihi
huibuka kutokana na utamaduni wa watu fulani . Huelezea filosofia na desturi ya watu hao. Ni
vipera hivi vinavyodhihirisha uchumi na asasi mbalimbali katika jamii husika. Pia tunaweza
kueleza kazi zilizofanywa kwa kuangalia Sanaa zisizo za kifasihi kama vile;uchoraji,
ufinyanzi,utarizi, ususi n.k. Sanaa hizi mbali na kutueleza kazi za waswahili, vilevile hutueleza
umuhimu unaowekwa kwenye uchumi. Sanaa hizi ni dhihirisho kwamba watu wa jamii husika
wana uwezo wa kufikiria na hata kuunda vitu mbalimbali: Sanaa hizi vilevile huangazia kuhusu
swala la vipawa katika jamii, yaani umuhimu wa vipawa katika jamii. Kazi mbalimbali kama
vile uvuvi,kilimo, uhunzi huelezea na kudumisha mahusiano na mtagusano baina ya watu wa
jamii moja au baina ya jamii mbalimbali, kazi ni nyenzo muhimu ya uzalishaji ambao
unategemewa na jamii kwa uhai wake. Katika kazi hii yangu ya kujadili swala la kazi kwa
waswahili nitaelezea kwa kina na kutoa mifano yanayoafikiana na maelezo.
1. KAZI YA UVUVI.
Uvuvi ni sehemu muhimu sana ya uchumi wa waswahili. Uvuvi huu hufanywa mitoni na kwa
kiwango kikubwa , baharini. Uvuvi huhitaji mbinu na vifaa mbalimbali. Baadhi ya vifaa
vinavyotumiwa ni kama vile mkuki, mitego, nyavu na majahazi. Kuna aina mbalimbali ya
majahazi kama vile ngalawa, hori, mtumbwi, dau, mtepe na mashua.Mbali na vyombo hivi vya
majini, kuna vifaa vingine vinavyotumiwa katika shughli ya uvuvi kama vile, pondo, mishipi,
migono, madema, munda, kimia na ndoana. Isitoshe kuna aina mbali mbali za samaki kama vile
dagaa, kole, jodarishohewa, mkizi, mkundaji, muzia, paragunda, koana,changu, papa, chafi,
nguru, taa mwewe, kamba kole, pweza, nyangumi. Samaki hawa hutumiwa kama kitoweo au
huuzwa ili kuwaletea wavuvi pato. Fasihi ya Kiswahili, inadhihirisha ,matumizi ya stiari za
uvuvi. Kwa mfano methali- wavuvi wa pweza hukutana mwambani, mgaaga na upwa hali wali
mkavu, hasira ya mkizi furaha ya mvuvi. Pia kazi ya uvuvi unaambatanishwa na nyimbo si
nyimbo tu na nyimbo za uvuvi zinazoitwa kimai.Harnad na wenzake (1972)wanaeleza kuwa
nyimbo ni mashairi mafupi ambayo hujitokeza katika sehemu nyingi za jamii . nyimbo zinaeza
kuwa na ubeti mmoja au Zaidi. Sanaa za nyimbo zinatofautiana na Sanaa ya mazungumzo kwa
sababu ya matumizi ya lugha pamoja na vionjo maalumu vya kishairi vinavyoleta mvuto kwa
jamii na kazi mbalimbali
Aina za zana zinazotumiwa kutega samaki ni:
1. Malema/madema ambayo hutengenezwa na mianzi iliyopasuliwa kuunda kapu wenye
muundo wa pembe sita na macho ya kutoshana. Chomo huvutia samaki kuingia ndani ya
lema vipande vya mawe hufungiwa ili kuzamisha majini kisha hufungiwa boya/plastiki
ili isihame.Malema husetiwa usiku kisha hutolewa siku inayofuata na samaki kutolewa.
2. Mshipi ni mshipi wa nailon wenye uzi uliofungiwa ndoana moja au Zaidi zilizotungikwa
chambo. Mawe hufungiwa kwenye mshipi ili kuzamishwa na mvuvi aliye kwa
ngalawa.samaki walionaswa hutolewa.
3. Bunduki ni bunduki ndefu ya mkono iliyoundwa na kipande cha mbao na hutumika na
chuma kali hurushwa kwa kamba za mipira. Wavuvi huogelea ili kunasa samaki na
bunduki.
Kuvua samaki kwa waswahili ina vyombo na nyakati zake pamoja na itikadi na mbinu
mbalimbali katika katika habari za maisha ya bwana Muyaki Bin Hajj AL-Ghassang imesadiki
kweli. Waswahili shughli zao nyingi zilikuwa ni za baharini, mashairi mingi aliyotunga ni
kuhusu safari za baharini kwenye beti zake hii.
‘’migongo ya mishuwari,wimbini mwatia ngisha
Mukihimiza safari, vyombo mukiteremsha
Leo kufuli bahari, hata mtoni mwausha
Maunenao mwaatusha,hamtushi mwangojani’’
Na hata malenga wa mvita AL- Ustadh Ahmad Nassir Juma Bhalo, pia ametunga kuhusu bahari
wakati anajikaga na kujinaki juu ya ugwiji wake wa kutunga moja ya beti zake hii,
‘’ndimi mvuvi halisi,kila uvuvi nalijuwa
Nivuwaye mikambisi, na papa wenye hafuwa
Wala sivui vingisi, mishipi haisumbwa
Nimekwambiya elewa’’
2. KILIMO
Waswahili hujihusisha na kilimo cha aina mbalimbali. Kuna kilimo cha kuzalisha chakula na
kile cha kuleta fedha . Aidha kuna kilimo cha matunda . kilimo cha matunda huhusisha upanzi
wa minazi,miembe, mikirosho, michungwa,malimau, michenzo, mikoma na migomba. Mimea ya
chakula ni kama vile mihogo, nduma, njugu, mtama, mawele,mahindi, mpunga, miwa na nazi.
Mboga ni kama vile kunde, mbaazi, boga maharagwe na mchicha. Kilimo mbali na kuwapa
waswahili fedha hutegemewa sana kuwapa lishe bora ambayo ni muhimu kwa afya yao. Isitoshe
kilimo huendeshwa kwa vifaa mbalimbali kama vile miundu, majembe na viselema.Uzalishaji
mzuri wa mimea hutegemea ufahamu mzuri wa misimu ya kiangazi,vuli na masika.Shughuli za
kilimo hufanyika kulingana na matayarisho haya maalimu, sharti yafanywe ili kufanikisha
kilimo; kufyeka ,kutoa na kuchoma takataka,kulima kupalilia na kuvuna. Hali hii ya kiuchumi ya
waswahili inaonekana katika fasihi , kwa mfano, ngano nyingi huzungumzia umuhimu wa
kufanya bidii kondeni.Aidha lishe ya watoto huzungumziwa katika hadithi ya watoto. Sehemu
hii ni moja ya vipengee vya hatua mbalimbali za maisha ya waswahili. Utamaduni wa waswahili
unasisitiza haja ya kujituma katika ufanyaji kazi kwa bidii, kwamba kazi mtu ana haki ya
kufanya kazi na kazi ni uhai. Kulingana na Matiaria (2017)jamii ya waswahili, shughli za
ukulima na upanzi wa minazi ni tegemeo lao kuu. Kwa mfano shairi la mnazi katika diwani ya
sauti ya dhiki(kur 17-22) inaonyesha ufanyaji kazi.
‘’ Alii
Sababu ya kukwambiya ya kwamba ushuke
Ni kuwa nataka kweya huko juu mnazini
Kwa ajili name piya,nitunde nazi mwendani
Nishakueleza kwa nini(ubeti wa 3P)
Maelezo haya yanatoa umuhimu wa kufanya kazi katika jamii ya waswahili.Kutokana na
maelezo ya zamani AL-Idris aliyetembelea mwambao wa Afrika Mashariki mnamo karne ya 12
na akaandika kitabu kiitwacho Kitab Rujar. Alitaja miji ya Malindi na Mombasa akasema
kwamba jina la zamani la kisiwa cha Zanzibar lilikuwa Unguja.Pia aliandika baadhi ya majina
ya ndizi .Mifano ya ndizi aliyotaja ni ikiwemo: kikondo, kisukari na mkono wa
tembo.Waswahili pia walijihusisha na upanzi wa miti. Walitumia miti kutoa
mbao,matunda,madawa, ujenzi wa nyumba na vyombo vya majini kama vile dau , mitepe,kuni
za kupikia na kutengeneza tembo.Baadhi ya miti ilikuwa mikoko, mipera, minazi, mikorosho,
mikwaju, mifenesi, mivinye. Wao walitumia miti kwa shughli za kupungia mashetani na vilevile
majani na mizizi yake ilitumiwa kama dawa. Fasihi ya Kiswahili inatoa istiari zake nyingi
kutokana na miti hii, Aidha matumizi yake hudhihirika katika mashairi, nyimbo, methali, ngano
na hata miviga.
3. UFUGAJI NA BIASHARA.
Katika maenezi ya Kiswahili tunaambiwa kuwa katika lugha ya Kiswahili ilitumiwa kwa
biashara nah ii ilifanya Kiswahili kuwa bora na kuenea Zaidi barani.
Waswahili wanajihusisha katika biashara na ufugaji. Wanafuga kuku, mbuzi, ng’ombe, kondoo,
punda ,ngamia , bata n.k. mara nyingi mifugo wengi hustahiwa, hulishwa, na watoto na ni ishara
ya utajiri katika. Mtu aliye na mifugo wengi huheshimiwa, isitoshe mifugo huwapa maziwa
yanayotumiwa sana na akina mama na watoto ili kuimarisha afya yao. Waswahili wamejihusisha
katika biashara kwa muda mrefu. Tayari nmeshataja kuwa maingiliano baina ya waswahili na
watu kutoka jamii zingine za ulimwengu yalitokana na biashara. Waswahili ni watu kutoka
jamii zingine za ulimwengu yalitokana na biashara.Waswahili pia walifanya biashara wao kwa
wao na majirani wa karibu kama vile: wamijikenda, wapokomo, wanyamwezi, wayo, n.k.
Kulikuwa na siku maalumu za kuenda sokoni ambazo zilijulikana kwa majina mengi gulio na
soko.
4. USAFIRI NA USANAJI
Waswahili pia wanajishughulisha na kazi za usafiri na usanaji. Katika usafiri kuna usafiri wa
maji na nchi kavu. Usafiri wa majini umesifika sana.Ulihusisha kusafirisha abiria na bidhaa
katika sehemu mbalimbali za dunia . Usafiri huu unategemea sana hali ya bahari ,Hindi mna
upepo inayoenda misimu mbalimbali ya dunia, aina ya vyombo vya usafiri na waendeshaji
vyombo hivyo. Waswahili wanaunda vyombo vyao vya usafiri kama vile merikebu, majahazi,
mitumbwi, mashua, vidau, mitepe. Vyombo hivi vinaendeshwa na mabaharia wakisimamiwa na
manahodha.Lengo la usafiri ni kujishughulisha na biashara, uvuvi, kutembelea jamaa na
marafiki, safari za kidini hasa kwenda kuhiji. Mbali na usafiri huu wa majini, waswahili, vilevile
wanajihusisha na usafiri wa nchi kavu. Usafiri huu unahusisha kutembea kwa miguu, kutumia
wanyama kama vile punda wanaobebeshwa mzigo au kuwabeba watu, isitoshe mikokoteni ni
rakwama zinazotumiwa kwa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali. Waswahili wanajishughulisha na
usanaji na vyombo mbalimbali. Lengo la kufanya vitu hivi ama kudhihirisha riziki. Baadhi ya
Sanaa hizi ni uchongaji mawe, ufinyanzi, useremala, uundaji wa vyombo, vya majani, ususi,
uhunzi, ufuaji na vitu mbalimbali katika tanuri ya moto. Mawe yanachongwa ili kusaidia katika
shughuli za ujenzi na hata baada ya kuchimbwa yanatiwa nakshi ili kufanya kuvutia jana.
Ufinyanzi unahusisha utengenezaji wa vyombo ama vinavyotumiwa kuhifadhia vitu au kwa
kupika mapishi mbalimbali. Vyombo hivi vinatengenezwa kwa waswahili. Baadhi ya vyombo ni
kama vile vyungu, vikaango,magudulia,mitungi n.k.Vyombo hivi hutumiwa kuhifadhia maji,
nafaka, vyakula na tumbaku.
5. USEREMALA.
Katika useremala waswahili wanahusika katika kutengeneza samani, milango, madirisha, ngoma
mbalimbali, vitana, makasha, sanduku, mbuzi za kukunia nazi, viatu vya miti na mikongojo.
Vyombo hivi baada ya kutengenezwa hupigwa msasa na kutiwa nakshi kwa ufundi
mkubwa.Sanaa ya useremala inategemea sana shoka ,visu,koleo,
jiziwa,msumeno,misumari,randa na patasi.Vyombo vinatengenezwa kulingana na mahitaji
mbalimbali ya watu ili kurahisisha maisha yao.
Usukaji au ususi unategemea sana malighafi ya kienyeji au wakati mwingine yale yaliyoagizwa
kutoka nchi zingine. Baadhi ya malighafi haya ni pamba ambayo hutumiwa kutengeneza gora za
vitambaa, majani ya miti,minazi,majani yake hutumiwa kutengeneza
vifagio,mapakacha,pepeo,madema na kuezeka nyumba.Mbali na minazi,mikocho na mikindu
inatumiwa katika ususi wa mikeka ya kulalia,misala ya kusalia,vitanga na kawa za kutunzia
chakula,majamvi,vikapu,shupatu mbali na majani ya miti, kuna na ususi wa nywele hasa upande
wa wanawake kama njia ya kuwarembesha. Sanaa zingine kama vile viatu, vifuko vya
kuhifadhia vishale , visu na ndara, Hivi vinatengenezwa na ngozi ya wanyama. Ufuaji hali
kadhalika ni miongoni mwa Sanaa maarufu uswahilini. Kuna ufuaji wa vyuma (uhunzi),usonara
(fedha). Ufuaji wa madini haya unafanywa na wataalamu wanaitwa wajumi.Kwa kutumia
fuawe, mifuo, nyundo,shoka, koleo,tezo,pataji,juba na bisibisi.Ufuaji inawapa Waswahili kipato
cha kila siku na pia kuonyesha uwezo wao wa kiakili.
Titany answered the question on December 6, 2021 at 12:12