Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza dini ya Waswahili

      

Eleza dini ya Waswahili

  

Answers


Faith
Dhana ya dini limesawiriwa na waandishi mbalmbali katika vitabu vywa fasihi. Hata hivyo,
usawiri wa swala hili la dini umetofautiana katika kazi ya mwandishi mmoja hadi mwingine na
tena baina ya kazi moja na nyingine. Suala la dini limesawariwa kwa namna mbalimbali, chanya
na hasi. Aidha inaonekana kwamba suala hili la usawiri wa dini na jinsi linavyojitokeza katika
kazi za fasihi limeshughulikiwa zaidi na wahakiki katika kazi za Euprase kezilahabi. Kwa
upande wa Omari (1981:39-40), yeye anaitazama dini kama mfumo wa kiitikadi, viashirio na
matendo, mambo na vitu ambavyo hueleweka na kutambulika kwa njia ya imani na si kwa njia
ya utafiti wa kitaaluma. Zaidi, dini ni lazima imhusishe mwanadamu na Mungu au viumbe
vingine viisivyo ambayo hayafahamiki kitaaluma, kiutafiti au ktawaliwa nayo.
Kabla ya kuchanganua kueleza dini ya waswahili hebu tuangalie maswali ni nini? Katika fasihi
simulizi ya waswahili, wazee wa Pwani wanadai kwamba walitoka sehemu za kazkazini ya
Pwani ya Kenya mahali panapoitwa Shungwaya karibu na mji wa Lamu. Kutoka Shungwaya,
waswahili walihamia sehemu mbalimbali. Matatizo hayo pamoja na vita, njaa, magonjwa na
ongezeko kubwa la idadi yao. Wazee hawa wa owani waneleza kuwa zamani walikuwa
waongozi, na waswahili ni jina la kubadilika tu. Wao walikuwa wakivaa nguo za ngozi na
kupima mashamba kwa kanda ya ngozi (Mbabu 1985:1-5). Wao wanadai kuwa neon Waswahili
au Kiswahili lilitolewa na kijana wa kiongozi aliyezaliwa na wasafiri wa Kiarabu kuwa wao ni
akina nani? Akawaambia sisi ni wasiwahili. Inaaminika kwa jina hili liliendelea kubadilika na
wakati na kuwa Waswahili.
Stiganda, Rewab, Knapppert na Whiteley (1969:7-9). Walidai kwamba Kiswahili ni moja kati ya
lahaja ya Kiarabu vilevile wanasema utamaduni wa Waswahili ni utunzi wa utamaduni wa
Waarabu. Wanasema kuwa lugha ya Kiswahili imegungamana na mafunzo ya dini ya kiislamu
na Waswahili wengi ni Waislamu. Wao hutumia majina ya dini ya kiislwamu kama vile
Mohammed, Ramadhani, Rajabu, Maulidi, Haji na mengineyo. Aidha ,baadhi ya maneno ya
Kiswahili yaliyokopwa kutoka Kiarabu yanahusiana na nyakati ambapo, Waislamu huswali, kwa
mfano, alfajiri, adhuhuri na kadhalika. Inajulikana kwamba dini ya Kiislwamu ilieletwa kwa
lugha ya Kiarabu. Kwa sababu hiyo, vifungu vya Qurhan tukufu aghalabu hukaririwa kwa
Kiarabu. Hali kadhalika, waandishi wa tenzi za Kiswahili ambao walikuwa wakitumia hato za

Kiarabu mara nyingi walikuwa wakitanguliza tungo zao kwa kumshukuru Allah na Mtume
Mohammed. Waswahili pia hufanya sherehe za Maulidi mjini Lamu kila mwaka ambazo
zinahusu kuzaliwa kwa mtume Mohammed. Kwa hivyo Kiswahili na dini ya Waswahili,
nitaeleza maisha ya mtoto wa Kiswahili tangu kuzaliwa kwake hadi kifo na sherehe mbalimbali.

1. KUZALIWA NA MALEZI YA MTOTO WA KISWAHILI
Malezi ni njia ya ukuzaji wa mtoto kwa kutarajiwa kufuata tabia na mwenendo unaostahiki.
Katika hali ya kawaida katika jamii ya waswahili, motto ni mtu au kijana ambaye bado kimalezi
na kimatunzo yako chimi ya himaya ya wazazi au walezi wake. Mtoto anakuwa chini ya
uangalizi wa wazazi ambao ndio waasi wa familia. Yule anayejitegemea ambaye hata kisheria si
mtoto tena, nap engine ameoa au kuolewa, atabaki kuwa ni motto mbele ya wazazi wake na
atatambulika hivyo wahenga walisema kwamba julea mimba si kazi, bali kazi ni kulea mwana na
umleavyo ndivyo akuavyo. Kuzaliwa kwa mtoto ni jambo muhimu kwa familia na jamii nzima.
Familia ndiyo msingi wa maisha na hali kadhalika uti wa mgongo wa jamii. Familia huhusisha
jamaa wengi kama baba, mama, wajomba, ndugu, dada, wapwa, ami n.k. kuzaliwa kwa mtoto ni
hatua inayowapa watu hakikisho kwamba familia na jamii kuonyesha kuwa maisha ya usoni
imeshughulikiwa. Uzazi ni mchakato unaoanzia katika mume na mke kuoana ambapo huleta
pamoja familia mbili au zaidi. Muungano huo hudumishwa tu iwapo mtoto atapatikana. Ndoa
huwapa hawa wawili mamlaka ya kujihusisha katika ngono. Baada ya kitendo hiki mwanamke
alitarajiwa ashike mimba. Kutoshika kulimaanisha kutoendeleza kwa kizazi. Hali hii ilifasiriwa
kama laana au mkasa wa kijamii. Maandalizi kabambe yalistahili kufanyika kwa kuilea mimba
na vilevile kwa shughuli ya kujifungua. Kwa waswahili mama mja mzito alilishwa vizuri ili
kuiboresha afya yake na hali kadhalika ya mtoto aliye katika tumbo la uzazi. Mama huyu pia
alistahili kulindwa kutokana na hatari yoyote kwa mfano kujiweka mbali na vitu vinavyoweza
kumdhuru. Maamdalizi mazuri yalifanyika na vifaa vinavyostahili kwa kuzaliwa kwa mtoto
kuwekwa vizuri. Mama mjamzito huombewa dua na kupewa moyo na jamaa pamoja na
marafiki. Wakati kujifungua inapowadia wakunga huja kuuguza tumbo kwa maumizi na pia
mwongozi wa dini hualikwa kuomba. Waswahili wana iman kuwa wanahitaji Baraka na uwezo
wa mungu wao katika kuzaliwa kwa mtoto ndipo tutaona sala. Kwa hivyo tutaona mwingiliano
mkubwa kati ya Kiswahili na Uislamu.

Kuzaliwa kwa mtoto huandamana na sherehe muhimu. Mtoto anapozaliwa huoshwa na mama
kabla ya baba wa mtoto kuruhusiwa kumwona mtoto na mkewe. Mtoto hufungiwa vigwe,
mvunje na mjambili, hufunguliwa koo kwa kurambushwa asali au maji ya tende, hurembwa
muru na wanja mikononi, miguu na usoni. Shimo huchimbwa nyuma ya nyumba na kitovu cha
mtoto huyo kuzikwa pamoja na makaa, chumvi na chuma. Kabla kufunikwa kitovu hiki
kulifundikizwa kijungu kipya tena kikafunikwa na kabla shumo kujaa vizuri unazi ulipandwa.
Mambo haya hufanywa kuondoa peopo wanaoweza kumyemelea mtoto. Kurambishwa asali na
maji ya tende huonnyesha furaha na ufanisi wa mtoto maishano, shubiri ni misuko suko
inayomsubiri. Kufukiwa kwa kutovu ni hali ya kuendelea kwa kizazi na kupandwa kwa mnazi ni
asili ya jamii na kuonyeshwa uendelevu wake.
Mtoto anapofikisha umri wa miaka saba, mtoto anafanyiwa ada ya akika. Sherehe hii huongezwa
na mwalimu wa kidini. Mbuzi wawili huchinjwa iwapo mtoto ni mvulana na mmoja iwapo ni
msichana. Mbuzi mmoja hukaangwa na kulwa kwa wali na wa pili huchomwa kwa mishikaki na
kuliwa na asali na mifupa ya mbuzi kufunikwa udongoni. Inamaanisha mifupa itatumiwa na
mwenyezi Mungu kuumba ngamia atakayotumiwa na mtoto kukwea mbinguni siku ya kiama.
Ada ya akika inaangaziwa kuhusu kuendelea kwa maisha hata baada ya kifo. Kubadilishwa kwa
mifupa kuwa ngamia siku ya kiama ni athari za Kiislamu. Hii sitiari ya maisha mzima wa
mwanadamu.
Kabla mtoto kutolewa nje mwanamke mzee hutoa wosia wake kwa njia ya kiapo. Wosia hii
hutolewa kwa wakati huu bongo za mtoto huwa tupu na hunasa chochote. Katika mazingira
mapya, wosia hutolewa hivi “Mungu amekuleta ulimwenguni, shinda moyo wako, na vitu vya
watu usiwe mtamani, umekujaulimwengu, usiwe mgovi ukagombanisha watu, kwa sababu
wahenga wamesea, liffalo kueleza lieleze, lisilofaa limeze, umekuja ulimwengu, usipite nyumba
zenye wake wa watoto, utapotea roho yako. Mungu amekuleta katika dunia ukae kwa heshima na
watu, kwa sababu wahenga wamesema, mwiza mwiza si utumwa.” Wosia hutolewa kusisitiza
mtoto awe na maadili anayopaswa na kufuata maishani ili awe na maisha marefu na yenye
ufanisi. Mwanamke mzee hutoa wosia kwa kuwa ana tajriba na maisha marefu. Mtoto
anayekiuka wosia aliyopewa huwaletea wazazi wake aibu na fedheha hata akapoteza maisha
yake. Wakati wosia unpotolewa mwanamke huwa amemweka mtoto kifuani na kwenywe nchi.
Mchi huonyesha mtu anastahili kuvumilia vishindo vya maisha na kwa hivyo moyo unatarajiwa
kuwa imara wakati wowote. Baada ya wasia mtoto hutolewa uwanjani na kudakwa mara saba
akiambiwa atazame juu na kurejeshwa ndani. Kumrusha mtoto juu mara saba akiwa amelitazama
juu ni njia mtoto anapaswa kuandama maaishani. Mtume Mohammed inasemekana ndiye wa
pekee aliyesafiri juu kuzipata mbingu saba hadi akakutana na mwenyezi mungu.
Katika miaka hii ya saba mtoto hunyolewa nywele. Desturi hii ni mchanganyiko wa Uislamu na
asili ya waswahili. Katika kunyolewa hatua ya kwanza huwa ni kumualika mwalimu wa dini
ambaye huja na wanafunzi wake wa vitabu vya maulidi na matari ya kuitikia vipoleo. Walimu
hukaa katika chumba kimoja kwenye mikeka na wanaume wengine walioalikwa. Chumba cha
pili hutumiwa na wanawake na mtoto anayenyolewa. Maulidi huanza saa nne za usiku mpaka
alfajiri. Mwalimu wa dini huanza sala alfajiri na mtoto huletwa na kutiwa tibu. Mtoto hushikwa
mikono na mama na baba au mwalimu. Tibu hupakwa juu kichwani na shingo yake. Kasha
babake mtoto hujitokeza na kuwapo walimu wa dini zawadi. Tibu iliyobaki hupakwa mkononi
mwa jamaa waliohidhuria sherehe hyo, kasha marashi na udi humwagiwa watu hao. Baadaye
watu hufika msikitini kusali na baadaye kurudi nyumbani kula na kuagana baada ya maombi ya
Mungu kumkuza mtoto.
Pia mtoto hupewa jina halizi kwa kuwa wakiwa wadogo hawana majina halisi. Watoto hupewa
majina baada ya siku saba ya kuzaliwa. Majina halisi ya watoto yaweza kutokana na wajomba
wakiwa ni wa kiume au shangazi wakiwa ni wa kike, au kwa wakati mwingine kutokaza na hali
ya mazingira. Hatua ya kumpa mtoto jina ni muhimu sana kwa sababu ndiyo humpa mtoto
utambulisho katika jamii yake. Majina anayopewa mtoto anapofika umri wa kuota meno hupewa
daa ili meno yasitoke vibaya. Dawa ya tungo hutengenezwa na wazee. Mtoto pia hufungiwa
hirizi ambayo huivaa shingoni kuwezesha kuota meno. Iwapo mtoto amekawia kuota meno
huogeshwa na kupewa dawa na waganga. Mtoto kwa wakati huu hupewa vyakula vya kijenga
mwili kwa mfano uji na mamake. Baada ya kuamka mtoto huoshwa uso wake na kupakwa
wanja. Kabla ya kulala hunywesha muru na mwingine akapakwa mwili mzima. Muru huaminiwa
kutuliza change. Pia mtoto hulindwa kutokana na peopo, magonjwa na maovu mengine. Hii
hufanywa kwa maombi, kunyweshwa na kupakwa dawa. Baada ya mtoto kufika umri wa kupata
elimu, hufundishwa dini na utamaduni wa uislamu na uswahili. Mambo ambayo huzingatiwa na
adabu, kazi mbalimbalo na majukimu ya kijamii. Katika elimu ya chuoni mtoto hufunzwa
kukarir vifugu vya Kurani. Pia elimu nje ya chuo au nyumbani inaendelezwa na wazazi katika
asasi ya tohara. Tohara hufanywa kumbini, kabla ya kuenda kumbini mtoto hualika jamaa zake
mkesha wa kutahiriwa na kucheza manyago. Alasiri baba na jamaa zake huandamana hadi
makaburini kufanya makafara ili kufanikisha tohara. Kaburi hutolewa majani yaliyomea, ubani
hutiwa ndani ya chetezo na kuwekwa chini ya kichwa cha kaburi. Wakati wa usiku ngoma
huchezwa pamoja na ngariba au mwinzi. Alfajiri ngariba huingia kumbini na kutahiri mtoto kwa
kirimbo na kila mtoto kutiwa dawa. Baada ya siku sita watahiriwa huitwa kwa sherehe ya mojo
ambayo huhusisha kuoga mwari na baadaye hupakwa dawa. Baada ya kurejea kumbini wazazi
wao huwatetea tu na pamba inayotumiwa kwa majeraha. Wakati wapo kumbiu watoto
hufundishwa adabu na makungwi zao. Baada ya kupona wazazi huwanunulia nguo moya watoto
wao na ngoma ya manango kuchezwa usiku kucha karibu na kumbini. Asubuhi watoto
hunyolewa. Kunyolewa huonyesha utakaso na kufuzu kutoka utotoni hadi ukubwani. Mtoto
huwa amekaribushwa katika jamii na kwa hivyo ni mali ya jamii na anachofanya sasa ni kwa
manufaa ya jamii.

2. NDOA NA HARUSI
Uswahilini ndoa na harusi ni asasi ya kwanza kwa uzito wa maisha ya kila siku ya mtu. Ubikira
ni ada kubwa sana kwa wasichana wa Kiswahili kabla ya kuolewa kwani ndoa ndicho kitovu cha
maisha ya Kiswahili. Ni desturi iliyoenea mwote Uswahilini kwa wazizi kuwa mtotokuwa
washauri wakuu wa ndoa za watoto wao. Kuna hatua kadha wa kadha tangu mtu aposapo hadi
kutoa mahari n akufanya harusi. Chuo hicho huwashirikisha makungwi na masomo katika
kuwaelekeza na kuwafundisha wari harusi kabla na baada ya harusi. Sharia za Uislamu huwa
ndicho kigezo pekee cha kuendesha maisha ya ndoa. Mtu akitaka kuoa kwanza huposa. Jamii
yake Yule mwanamke ndiye hutumwa kupeleka habari ya posa. Huyu huitwa mshenga. Watu
wengine humtuma mshenga kusema maneno ya babaye mchumba na huandika barua. Baadaye
barua inasomwa na ushauri kufuatwa. Iwapo watakubali mshenga atamwarifu mposaji kwamba
wakwewe wameridhishwa wote. Yule mchumba atanunua kila zawadi kumpelekea mchumbawe
kama ngua mzuri au matunda yaliyoiva. Bali hawaruhusiwi kuonana hadi siku ya harusi.
Mshenga tena hurudi kuuliza kiasi cha mahari wanachkitaka na akikubaliwa hurudi kwake na
kumpa mchumba habari zile na akikubali humpa mshenga fedha azipeleke kwa mkewe. Fedha
hizo huitwa kifunga mlango au uchumba. Baada ya uposa, wakwe hulipwa mahari kamili na siku
ya kuoa inakubaliwa na kupitishwa . baada ya hapo watu, majamaa na marafiki huywa kahawa
na vyakula vinginevyo. Kijana pia hucheza ngoma ya tari.
Siku tano baada ya kahawa na kuposa, mshenga kwenda kupiga pamba. Mshenga huwarifu watu
kina mwana na bwana kushona godoro na mto. Baadaye lile godoro na mito mitatu hupelekwa
katika chumba cha bi. Harusi na kufunikwa nguo. Harusi hufanyika katika nyumba ya wazee wa
harusimwanamke. Asubuhi ya harusi nyumba hupambwa, vizuri na kila sehemu ikanadhifiwa
vizuri. Alasiri huja shogaze bi arusi kumpeleka kumwosha na kumpamba. Sherehe ya nikaha
hufanyika msikitini au kwa nyumba. Baada ya kulipa ada zinazohitajika, mume huenda
ukumbini. Nyimbo na ngoma mbalimbali huandamana na sherehe hii. Baada ya shughuli zote
bwna na bi harusi huoana kasha ikafuata fungate.

3. KIFO NA MAZISHI
Mazishi ni taasisi ya kuwarejesha waja walikotoka ama kuwakumbusha walio hai juu ya
marejesho hayo kwa Mola wao. Msiba wa kufiliwa huwa ni faridhi-kifaya kwa Waisilamu wote.
Huzuni za kufiliwa huwa ni za wote na kazi kubwa ya majirani na marafiki ni kuwafariji
wanandugu waliofiwa. Maiti ni lazima azikwe kabla ya masaa ishirini na ne kuisha kulingana na
dini ya Waisilamu. Maiti huoshwa kwa uana iwapo ni mume anaosha na wanaume na iwapo ni
mke huoshwa na wanawake. Baada ya hapo anatiwa kwa janda kasha maiti hupelekwa msikitini
ambapo sala hufanyika. Kaburi huwa imechimbwa kitambo kabla ya kila kitu kufanywa. Baada
ya sala maiti hupelekwa kuzikwa na maombi ya mwisho kufanywa makaburini. Iwapo mume wa
mkw ndiye alifariki bana mke ndiye alifariki bana mke ni mjamzito basi atakaa kwa miezi kadha
hadi ajifungue ndipo arudi kwake.

4. ITIKADI NA USHIRIKINA
Jambo la ushirikina si la waswahili pelee bali watu wote hata wazungu, waisilamu, wakristo n.k.
uislamu na ukristo haitunzi wala kuhimiza itikadi hii. Lakini baadhi ya waumunu hujikuta
wamejaa tele ndani ya uwanja huu wa maisha.
Itikadi ya kuwepo pepo-majini, mashetani n.k nguvu na uwezano wa pepo hao katika kulinda
mashamba, mali, majini, kusaidia kutibu maradhi na mashamba, mali, majini, kusaidia kutibu
maradhi na mashetani kuroga n.k. itikadi hizi zina nafasi katika upwa wote wa waswahili.
Pamoja nazo waswahili wana mila kama vile ya miiko mbalimbali, kwa mfano kula gizani ni
kula na shetani, kunywa maji msalani mtu huwa mwongo. Bundi akilia juu ya paa la nyumba
anatangaza kifo n.k. itikadi hii ina mafunzo mengi yanayostahili kuhifadhiwa na kuzingatiwa.
Titany answered the question on December 6, 2021 at 12:23


Next: Elezea kazi mbalimbali zilizofanywa na Waswahili
Previous: Jadili Ngoma za Waswahili

View More Utamaduni Wa Waswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions