Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili Ngoma za Waswahili

      

Jadili Ngoma za Waswahili

  

Answers


Faith
1. SHABWANI
a) Hii ni ngoma ya Kiarabu, hasa kutoka jamii ya Kihadharami. Ilifika hapa Malindi na Mombasa
karne nyingi ziliopita na kutezwa katika sherehe nyingi kama za harusi na za Maulidi wakati wa zefe.
Shabwani ni ngoma ambayo inachezwa kwa harakati za kuruka ruka na mikononi wenye kucheza
huwana bakora au fimbo wakati wakicheza zile fimbo huwa zikirushwa rushwa juu na huku wakiiimba.
Arabuni waliokuwa wanao cheza huwa wana tumia panga lakini hapa watu hutumia fimbo au bakora.
b) Ngoma ya shabwani hutumia ngoma moja au mbili, matasa na vigoma. Ngoma ya tasa ni
huambwa kwa ngozi.(yaani karai liloombwa kwa ngozi)

c) Hii goma ya tasa ni lazima iwe itakanzwa moto wakati wa kutumika na kupigwa kwa vijiti viwii
vipana virefu. Kupata mlio mzuri ni lazima vile vijiti viwe vigumu na tasa limeoka moto uzuri.

d) Kuanza kucheza shabwani – wachezaji hujipanga laini mbili za kulekeana yaani kuangalian uso
kwa uso. Wakati huo wenye kupiga tasa huwa wanazikanza moto.

e) Kiongozi huingia katikatii na kuanza kutowa shairi la fumbo na kulekea laini moja. Na wale
wachezaji waliolekewa waitika kama vile kiongozi anavyo imba. Wakisha itikia anazungukia laini ya pili kutowa shairi ya jawabu yahilo fumbo. Sasa wachezaji wakaanza kuimba na kujibanza wakati huu wenye ngoma wataanza kupiga na shabwani kuanza ana wachezaji wote wakielekea upande moja wakiruka ruka na kurusha fimbo / bakora walizo nazo mikononi mwao kwa nidhamu ya kufuatia mdundo wa ngoma.

f) Shabwani – watu waenda wakicheza, wakifika mita 150 au 200 mita, hubidi wenye kucheza waanze
upya, kwani tasa huwa limeanza kupoa na mlio huwa si mzuri. Shabwani itaanzwa kama vile ilivyoanza mwanzo.

g) Shabwani zilikuwa ni tatu, kutoka Mombasa Malindi na Mambrui. Shabwani hizi mara nyingi
hushindana wakati wa sherehe za Maulidi.Mamburii na Malindi Shabwani ya Malindi na Mambarui
walikuwa wakishindana wakati wa sherehe za Maulidi ya Kipini.
h) Shabwani ilikuwa ikichezwa sana katika sherehe za harusi wakati wa kutia hina na kumnyowa
bwana harusi na kumpeleka nyumbani.

i) Shabwaini huchezwa siku ya kutiwa hina Bwana harusi. Sherehe kufanyika usiku wa siku ya
kuingia ndani, siku ya kuamkia nikaka. Sherehe hii hufanywa katika uwanja karibu na nyumba ya bwana harusi nayo inaanza baada ya ishaa na kuendelea hadi saa nne usiku au zaidi.

j) Katika sherehe ya kunyolewa bwana harusi ambayo hufanyika katika mmoja ya kitanguni(bustani
ya miti ya matunda na maua)
Sherehe ya kunyolewa, bwana harusi akiwa ananyolewa shabuwani wakati huo huwa inachezwa. Akisha
kunyolewa huchukuliwa Yule bwana harusi na shabwani hadi pale atakapo funga, Nikaha. Akisha funga Nikaha baada ya ishaa, bwana harusi hupelekwa kwa mkewe kutowa mkono na kisha kupelekwa kwake nyumbani.

2. KIRUMBIZI
a) Kirumbizi huchezwa sana na Wabajuni na Waswahili lakini huchezwa katika sherehe zote za
harusi hata ya Kiarabu. Kirumbizi Kawaida huchezwa na wanaume pekee, watu hufanya duwara kubwa
wa chezaji na wano piga ngoma huwa ndani ya hilo duwara au boma. Kirumbizi, ni mcheza wa bakora ua fimbo Watu wa kucheza kirumbizi katika harusi. Wanawake huwa kwenye jukwaa lilositiriwa na uwa wa makuti. Wale wanawake huwa wanawaona wanaocheza kirumbizi lakini wachezao na wanaume
wengine hawaoni wale wanawake. Wale wanawake husherekea nakushangilia kwa kupiga vugo na kwa
nyimbo.

b) Kawaida ya kirumbizi inategemea Yule mwenye kuitayarisha, kuna wanao cheza kwa siku moja,
siku tatu au siku saba. HIvi inatagemea mfuko wa Yule mwenye kutayarisha au mwenye kuweka
kirumbizi na kuandaa.
c) Siku ya mwisho ya kirumbizi, ni siku ambayo Bwana harusi huja uwanjani na yeye kushiriki.Hapo huwa ndio kilele cha sherehe hio. Bwana harusi – yeye huwa amepambwa kwa mashada, viluwa na makoja. Yeye huinuliwa na baba mkwe na kucheza nae. Kucheza kwao huwa ni kwa taratibu na heshima pamoja na taadhima kubwa. Huko wanawake wakishangilia zaidi ya siku zilio pita.
Wakati bwana harusi akicheza watu hugaiwia maji ya sharebati na tambuu. Tambuu hizi ni tafauti kwa vile huwa zina pambwa kwa karafuu.

d) Uchezaji wa kirumbizi huchezwa kwa watu kutumia fimbo au Bakora, mchezaji huchukuwa
fimbo au bakora na kuingia uwanjani na kumrushia fimbo au bakora Yule atakae cheza nae.
e) Wakiisha ingia kiwanjani huwa wanacheza kwa upole n atarabibu kwa kufuatao mdundo wa
ngoma. Wachezaji huzunguka wakicheza kwa mfano wa koo la tausi au bata mzinga anapo mtaka tausi
au bata mzinga jike. Huzunguka wakicheza kwa haiba na utaribu wenye kupendeza sana. Ngoma
ikitangwanya na kulia kwa sauti kubwa, sasa wachezaji kurushiana fimbo au bakora moja moja. Wala hakuna kurushiana kwa nguvu za kupita kiasa bali kwa nguvu ya wastani kwa haiba na madaha.
Yule aliorushiwa bakora au fimbo mara ya kwanza ataichukuwa fimbo au bakora ya mwenzie amrushie
mwengine na hivi mchezo uanandelea.
f) Ngoma zinao tumika ni ngoma za kawaida na msondo, tasa, zumari au tarumbeta.

3. GOMA

Goma hii huchezwa sana na Wabajuni. Ngoma yenyewe ni ngoma ambayo huchezwa bila vishindo
wala harakati nyingi. Ni ngoma inayochezwa kwa ustarabu na haiba ya juu.
Wachezaji hucheza kwa makini wakifuatia mdundo wa ngoma. Huechezwa kwa makini sana ya hali ya
juu ya utilivu kutaka kuona harakati zao za kucheza ni lazima uwe na makini kutizama ndio utaona harakati za kucheza.
Wachezaji huwa wamevaa kanzu nyeupe na kofia za vito, bakora mkono wa kulia. Bakora huwa
imewekwa begani na huwa inainuliwa mara moja moja kufuatana na mdundo wa ngoma. Wachezaji
huwa wamepambwa kwa mashahada ya maua na pengine kosaja la pesa.
Wapigaji ngoma huwa wanaelekea wale wachezaji. Ngoma zenyewe ni zile za kawaida kama a
kirumbizi, tasa na zumari. Goma inaweza kuchezwa kwa muda mrefu na huku watu wengine wakiimba
nyimbo tofauti tofauti.

4. VUGO
Hii ni ngoma inayochezwa na wanawake wa Kibajuni na Wakiswahili. Ngoma yenye hutumika katika
sherehe nyingi kama nilivyo eleza hapa nyuma katika kirumbizi na kupeleka bi harusi na shrehe
nyinginezo.

Ngoma huchezwa na wanawake, wakiwa wameshika pembe na kigongo kidogo cha kumpigia pembe.
Pembe hupigwa kufuata mlio wa ngoma na mara moja moja huuinuliwa juu kichwani zikipigwa kwa
nguvu huku wakiemba mashairi mengi mazuri
Ngoma hii huchezwa na mchanganyiko wa wanawake lakini zaidi ni Wabajuni na Waswahili.

5. LELEMAMA
Hii pia ni ngoma ambayo Huchezwa na Wabajuni, Waswahili na wazaliwa wa Kiarabu. Ngoma hii sana
huchezwa siku za harusi. Pia hii inategemea wezo wa mtu anae cheza au anaendaa harusi, yaani kucheza kwa siku moja au tatu au zaidi lakini hazipitishi saba.
Ngoma yenyewe huchezwa na wanawake wanao vaa kanga peikee. Kanga ndio nguo rasmi ya kucheza
lelemama, kawaida lelemama huchezwa ndani ya uwa yaani boma liljengwe kwa makuti wanaohudhuria
ni wanawake pengine isopokuwa wale wapigaji ngoma huwa waume.
Lelemama huchezwa na wanawake wakiwa juu ya mabao wakiwa wamevalia leso zao (kanga) zilio safi
na mara nyingi huvaa sare, wachezaji huwa wamejipamba kwa vilua, mashada ya asmini yalio fungwa
vichwani. Kila mchezaji huwa ana vigongo viwii ambavyo urefu ni kama inchi 6.

Lemamama huchezwa kwa makini na kuyumba yumba kulia na kushoto kwa kufuata mlio wa ngoma,
lelemama pia huchezwa kwa makini na utulivu wa hali ya juu. Wanawake wengine huwa wamekaa chini
kwenye majamvi wakipiga makofi na kuimba. Kufuata sauti ya zumari au tarumbeta.
6. MWARIBE
Mwaribe haswa ni ngoma ya Kiswahili lakini huchezwa na makabila kadhaa. Kawaida huchezwa na
wanaume na wanawake. Waume wakiwa upande mmoja na wake wakiwa upande mwingine wakiwa
wameangaliana uso kwa uso.
Ngoma zinaotumika ni za kwaida lakini hutumika na msondo (msondo ni ngoma ndefu) mwenye kupiga
huwa amesimama na ngoma ameitia katikati ya miguu ikizuiliwa na magoti mawili. Pia hutumika na
zumari.
Ngoma ikianza kuchezwa na watu hucheza na kuimba mwanmke huja katikati akicheza kwa muda kisha
akaenda upande wa wanaume akamtowa mwanamume kucheza nae, watacheza pamoja kwa muda pale
katikati. Kiasha yule mume wa atamtowa mwamke mwengine naye watacheza pamoja kwa muda pale
kati kisha yule mke atamutowa mwamume mwingine na wataendelea kucheza yule mwanamke wa
kwanza atatoka katikati ya uwanja. Mwanamke wa pili atacheza kwa muda wa baadae kumtowa
mwanamume mwengine msitari wa waume na ngoma kunaendelea. Ngoma itaeendelea hivi hadi
kuvunjika.

7. GONDA
Gonda ni ngoma ya Kimijikenda ambayo huchezwa sana na Wagiriama. Ngoma hii kuchezwa kwa utulivu
sana na ngoma yeyenye kuchezwa kwa mdundo mzuri hasa kwa wanaume. Wanaume wanaocheza
Gonda huvaa shuka ndefu yenye maridadi ya matavuo chini ukingoni. Kifua huwa wazi lakini huwa
kimepitishwa na ukanda wa nguo iliofungwa kwa umeridadi kutoka bega hili kushuka katikati ya mwili hushukia kiunoni upande mwengine yaani hutoka bega la kulia ikishuka upande wa kiuno wa kushotoni, nguo zenyewe huwa zinatiwa maridadi mazuri. Pia ukanda mpana ambao hufungwa kiunoni namna ya pekee. Kichwani wanavaa kofia za tarbushi nyekundu.

Ngoma hii huchezwa sana na wazee ambao hucheza kwa madaha na Makini huku wakirusha migwisho
na kupiga firimbi gonda ni ngoma yenye haiba sana na huchezwa sana na wazee katika sherehe
maalumu.
Wanawake kama kawaida huwa wamevaa mahando yalio malkubwa, huku wakicheza na kuimba na
kupiga vigelegele.

Waume hucheza na wanawake wakiimba, huku waume wakicheza miguuni huwa wamefunga njuga na
mikononi wamevaa meridadi ya ngozi. Wakicheza hutetemesha mikono na kupiga miguu yao chini ili zile njuga zipate kulia.
Ngoma zake ni za kawaida na msondo na kupiga debe kwa vifimbo pia huvuvia pembe na kupiga zumari Ngoma hii huchezwa hadi wenyewe kuchoka.
Titany answered the question on December 6, 2021 at 12:27


Next: Eleza dini ya Waswahili
Previous: What is Business Research?

View More Utamaduni Wa Waswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions