Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali. Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa isiyo na kifani.

      

Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa
isiyo na kifani.
Alipokuwa katika shule ya msingi, walimu na wazazi walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili.
Isitoshe, alifunzwa masomo vyema lakini akili yake ilikuwa butu. Akawa haingizi chochote cha maana ila
uchafu wa fikira. Nyumbani nako hakuzingatia maonyo. Alikuwa hatulii.
Wakati fulani wa krismasi, Beata alipomaliza tu shule ya msingi, alikutana na mwanamume mmoja
mliliwa na wasichana wengi; mtajika kwa mali na jina lake ni Mshikaji . Beata akadanganywa akadanganyika.
Akatorokea kwa huyu Mshikaji ambaye alikuwa ameshawataliki wake wawili tayari. Akawa mke mlezi. Ikabidi
awalee watoto waliobaki na baba yao baada ya mamazao kutanzuka. Beata mwanzoni aliona raha, ingawa
alikereka kuitwa mama kabla hata ya kumpokea mwana wake mwenyewe. Aliwabeza waliokuwepo awali na
akajiona kuwa yeye ndiye mchukuzi bora. Akadharau kuwa pakacha likivuja, nafuu huwa ni kwa yule
mchukuzi. Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua.
Muda si muda, akajikuta ana wana watatu kwa kipindi kifupi. Mumewe naye hakutulia na mambo ya
nje. Akaimarisha nyendo zake za kiguu na njia, akipochoka, akiingia garini na kuikata mitaa. Beata aende wapi?
Alifungika nyumbani ndi ndi Akamlea mwana huyu na yule; wake na wale wa kambo. Vijisenenesenene
vikazidi. Lakini akajaribu kuvumilia akidhani atazila mbivu, wapi! Alipoligema ilibidi alinywe. Siku zikaja na
kupita. Beata akajuta kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri.
Pesa na raha alizokuwa amezikimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni. Kwao nako kukawa hakurudiki.
Beata akawa majamzito tena kama kawaida akawa anaenda kliniki za wajawazito. Alipopimwa ikabainika
kuwa ana ukimwi. Mtoto alipozaliwa akafariki. Yule mumewe akaanza kumnyanyasa.
Baada ya miaka mitatu, bwana Mshikaji, aliyekuwa akijitapa kwa unene na mali, akaanza kupotelewa na
kiriba chake cha tumbo. Homa za hapa na pale zikaanza kumyemelea. Vipelevipele vikamsambaa mwilini. Hata
akamsingizia Beata kuwa ni yeye aliyeuleta huo ukimwi Ilikuwa ni wazi kuwa msambazaji alikuwa ni yeye
bwana. Waliokuwa pembe za chaki waliujua ukweli ulipokuwa . Baadhi ya vidosho wake walishaanza
kupukutika kama majani yafanyavyo wakati wa mapukutiko. Isitoshe, wengine walikuwa hoi vitandani wakiwa
hawajui waingiao wala watokao. Ugonjwa wa kamata ulishawakamata. Mwisho akawa ni wa kulazwa na
kutoka hospitali hizi na zile. Pesa zikawaishia, wakawa waya. Beata akawa hana budi kuviuguza vidonda
ndugu vyake na vya mumewe. Hatimaye, mumewe akabwagwa chini na ukimwi na akafafo!
Si ndugu si marafiki, hawakumuelewa Beata. Waliamuona kama pweza aliyejipalia makaa makubwa ya
moto makali. Ada za shule zikawa ni shida. Huruma ikwaingia watu. Watu wakasema. “Lisilobudi hutendwa.”
Wakaubeba mzigo kwa hiari yao. Wakawafanyia watoto harambee ya ada na peza za matibabu. Mwishowe
Beata naye aliaga dunia akiwa bado mbichi kwa umri. Hata miaka ishirini alikuwa bado hajafikisha. Watoto
ikabidi walelewe na wahisani.
Hapo walimwengu wakaja kutambua ukweli kwamba, uzuri si hoja hoja ni tabia. Isitoshe mtu
akikimbiliwa na kila mtu, ukimwi hatauepuka. Mtu akiupata, hufa. Anadidimiza watu wengi pamoja na familia
yake. Jamii ilifunzwa pia kuwa unene si hoja. Hata watu vibonge huweza kuleta ukimwi. Basi, jamii hiyo
ikaazimia kuwa wao hawatakuwa watumwa wa tabia iletayo ukimwi. Walitambua kuwa ukimwi unarudisha
nyuma maendeleo na kuipakaza jamii mizigo isiyo tarajiwa. Nasi tutahadhari kabla ya hatari

1. Andika kichwa kifaacho kisa hiki
2. Ni jambo gani lililomkera Beata baada ya kuolewa na Mshikaji?
3. Toa sababu moja iliyomfanya Beata kuwadharau wenzake waliomtangulia kwa mshikaji?
4. Ni kwa nini Beata alianza kujuta?
5. Toa sababu moja kuonysha kuwa Mshikaji ndiye aliyeusambza ukimwi
6. Kulingana na kifungu hiki taja hasara zinazoletwa na ukimwi.
7. Kwa nini walimu na wazazi hawangelaumiwa kwa yale yaliyompata Beata?
8. Andika maana ya:
i) butu
ii) Kope zikawa si zake
iii) Akiwa bado mbichi
iv) Kuzanzuka
v) Vijisenensenene.

  

Answers


Kavungya
[1] [i] Asiyesikia na mkuu huvunjika guu
[ii] umekuwa pweza kujipalia makaa?
Sahihisha kichwa kingine chochote kinachoafiki kifungu hiki

[2] Kuitwa mama kabla ya kumkopoa mwana wake mwenyewe

[3] -Alijiona kuwa yeye ndiye mcukuzi bora
- Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua

[4] -kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri
- pesa na raha alizokimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni

[5]- mumewe hakutulia mambo ya nje , alikuwa kiguu na njia
-Alikuwa na wanawake wengi nje ya ndoa

[6] –kukonda
-homa hapa na pale
-vipelevipele mwilini

[7] –walikuwa walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili

[8] [i] isiyo na makali
[ii] kuona aibu, soni, fedheha, haya
[iii] -akiwa bado mdogo
-Bado hajakomaa
[iv] kuondoka mahali kwa haraka
[v] vijinenoneno
Kavungya answered the question on November 21, 2022 at 11:20


Next: Read the following narrative and answer the questions that follow. One afternoon, a big wolf waited in a dark forest for a little girl to come...
Previous: Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions