UFAHAMU Ajira ya watoto Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.

      

UFAHAMU
Ajira ya watoto
Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa
karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.Fauka ya hayo,walininginia katika umaskini
uliokithiri.Hivyo,wengi waliselea katika kazi za kijungu jiko.Watot wa umri wa kwenda shule
walikosa elimu na kuzurura mitaani.Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu,tajiri mmoja aliyemiliki
shamba kubwa.Aliwaajiri watoto hao.
Mwakisu alikuwa mkwasi alietononoka si haba.Kama ni senti ,alikuwa nazo.Kilichotia doa
jina lake ni kiburi.Mbali na kiburi hicho,yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu.
Hakubarikiwa kuwa mwema .Maadili hutuongoza kila mara kuwa ‘wema hauozi’.
Kwa Mwakisu,wema ulioza na kuvunda .Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na
ukawa msamiati aliouchukia.Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule.Tabia
yake hiyo ndiyo iliyowafanya Wavuruni kumtoa katika orodhayao ya watu wema.
Mwakisu alistaajabisha!Hakutaka kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa
alikuwa nao uwezo.Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu.Mkwasi huyu alifurahia
kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa
ujira mdogo.
Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote ,kwani tuna shida
nyumbani.” Mwasiku alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza.Hapo alimchomolea mwajiriwa
wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua.Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi
kulisahau.Lilikaririwa akilini mwake kwa sonono.Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na
Mwakisu ni kufadhiliwa u chini.
Kiburi cha mwakisu kilidhihirika kila mara .Kila alipomwona motto akilia kwa uchovu au
maumivu ,ungemsikia akimfokea ,”Chapa kazi!Unalilia nani hapa?Kama humudu kazi rudi kwa
mamako ukanyonye.”
Kazi nyingi zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo.Si kipupwe, si
kaskazi,si vuli,si kiangazi ,si kusi:kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto.Kingi,kwa
mfano,alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa .Kisha
angewakatia mg’ombe nyasi na kuwasafisha .Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.
Msimu wa kipupwe uliwadia.Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingin
aliugua.Watoto wengi wakapatwa na maradhi.Wawili wakaaga dunia.Wazazi walipoona maisha ya
watoto wao yamo hatarini,wakaandamana hadi kwa Mwakisu.tajiri huyo aliwajia kwa meno ya
juu,’msiniitie kibuhuti.Mimi niliwaajiri watoto,sio watoto na wazazi wao”.Wazazi wakatanabahi
kuwa , ‘Pa shoka hapaingii kisu’.Waliandamana hadi kwa chifu.Chifu alipoyaona yamempita
kimo,akafululiza hadi kituo cha polisi.
Mwakisu akakamatwa ,akashtakiwa na kuhukumiwa .Alipatikana na makosa ya kuwaajiri
watoto wenye unri mdogo na kusababisha vifo vya wawili hao.
Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni.Ikatoa pia misaada ya
kuendeleza elimu;elimu ya bure kwa shule za msingi.Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo
kikuu.Akawa daktari.
Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu.Kingi akampa huduma mzee
aliyejawa mvi na kukoboka meno.Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.
Mwakisu akabahatisha,”sura yako….ni kama Kingi…”Kingi akamjibu,”Mimi ndiye
Kingi.”Wakakondoleana macho, huku machozi yakimtiririka Mwakisu.

Maswali
1.Toa kichwa kingine kwa habari hii.
2.Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni.
3.Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao?
4.Taja kazi alizofanya Kingi.
5. Mwasiku alishtakiwa kwa makosa gani?
6.Eleza maana ya semi hizi.
(a)Kazi ya kijungu jiko.
(b)Tononoka si haba.
(c)Kodolea macho.
7.Toa maana ya methali hizi:
(a)Wema hauozi.
(b)Pa shoka hapaingii kisu.
8.Toa maana ya msamiati huu kama ulivyoptumiwa katika makala:
(a)Fauka ya
(b)Alistahabu

  

Answers


Kavungya
1.Toa kichwa kingine kwa habari hii.
Anwani mf.
Udhalimu wa Mwakisu.
Shida za wanakijiji wa Vuruni.
Tajiri Mwakisu.

2.Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni.
a) Walikuwa maskini.
b) Waliikosa elimu.
c) Watoto wao walizuru mitaani.
d) Walikosewa heshima na Mwakisu.
e) Aliwadhulumu wanakijiji.

3.Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao?
a) Mwakisu alikosa utu, huruma na alijaa kiburi.
b) Mwakisu aliwaumikisha watoto

4.Taja kazi alizofanya Kingi.
(a)Kuwakama ng’ombe kumi kila siku
(b)Kubeba maziwa hayo hadi kwenye tangi kubwa.
(c)Kuwataftia ng’ombe nyasi.
(d)Kuwasafisha ng’ombe.
(e)Kuzoa samadi.

5. Mwakisu alishtakiwa kwa makosa gani?
Aliwaajiri watoto wenye umri mdogo na kusababisha vifo vya wawili wao.

6.Eleza maana ya semi hizi.
(a)Kazi ya kijungujiko.
Kazi ya malipo haba mno.
(b)Tononoka si haba.
Kuwa tajiri sana.
(c)Kodolea macho.
Tazama kwa mshangao

7.Toa maana ya methali hizi:
(a)Wema hauozi.
Matendo mema daima hudumu
(b)Pa shoka hapaingii kisu.
Kutafta mbinu au njia bora ya kutatua tatizo

8.Toa maana ya msamiati huu kama ulivyotumiwa katika makala:
(a)Fauka ya
Zaidi ya/juuyahayo

(d)Alistahabu
Alipendelea/alionelea
Kavungya answered the question on November 21, 2022 at 13:08


Next: Fill in the blank with the correct forms of the words in brackets.i) The tragedy was beyond everyone’s ……… (comprehend)ii) The driver of the lorry...
Previous: Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions