Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata: Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea kama moto nyikani msimu wa...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea
kama moto nyikani msimu wa kiangazi.
Mstahiki Salamwana Salamwene, maana hili ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mtu wa ajabu sana. Asili
yake yenyewe ilikuwa kitendawili. Inasemekana mamake alibeba mimba iliyopita miezi tisa. Na kila
aliposhangaa alisikia sauti tumboni ikisema. “Mama kuwa na subira, bado ninalainisha lugha yangu”
Baada ya muda mama alipolalamika alisikia, “Mama ninakaribia, ninamalizia kunoa ubongo wangu.”
Halafu siku moja ikanyesha mvua kubwa iliyoandamana na radi. Waliokuwepo wanasema waliona
mmweso mkali ulioangaza hata kwenye milima mikubwa. Salamwene akazaliwa. Moja ya sifa zake
kubwa ilikuwa hekima na maarifa ya ajabu. Hakuna tatizo la watu wake ambalo alishindwa kulitatua.
Watu wakawa wanafunga safari za siku nyingi kutoka mbali kuja kwenye ikulu yake. Wengi walienda kwa
shida za dhati lakini wengine walikuja kumjaribu.
Siku moja akaja mfanyabiashara tapeli na maua ya aina akamwambia, “Mstahiki mfalme, mtu wako
anataka kuniuzia maua haya kwa vipande vingi vya almasi name nina shaka kuwa moja ni la bandia
waweza kuniamulia?” Mfalme hakujibu. Naye inasemekana alipenda zaraa na hivyo alikuwa na miti na
mimea iliyozaa maua na kutoa harufu anuwai. Basi akaja nyulu na kutua kwenye ua moja. Mfalme
Salamwana akamtambulisha ua halisi.
Muda ukayoyoma huku wahitaji wakiingia ikulu na kutoka. Siku moja akaja Binti mfalme mmoja kutoka
nchi ya mbali na msafara mkubwa. Alipokewa kwa taadhima. Alikaa mwezi mmoja. Kila siku alikaa
kwenye baraza akishuhudia mfalme akiyatatua matatizo ya watu. Jioni walikaa na mfalme pamoja
wapambe wao akijifunza kutoka kwenye hazina kubwa ya busara ya Mstahiki Salamwana.
Usiku uliotangulia kuondoka kwa mgeni, Salamwana alitoa amri za ajabu. Kwanza, aliamuru magudulia
yote ya maji kwenye chumba cha kulala mgeni yabadilishwe. Pili, alimwamuru mpishi kupika chakula
kilichokolea viungo kutoka Bara Hindi. Tatu, aliwaamuru wapambe kuwa mgeni akiomba chochote
wasimpe ila wamfahamishe. Usiku huo, mgeni alihisi kiu kikali lakini aliponyanyua gudulia kumimima
maji kwenye bilauri ya dhahabu, halikuwa na maji. Akajaribu la pili, magudulia yote ya shaba yaliyokuwa
chumbani hayakuwa na maji. Alijitahidi kuvumilia lakini wapi! Ilibidi atafute msaada kwa wapambe nao
wakamweleza walivyoambiwa. Mwanzoni aliona ni kukosa fadhila kumsumbua mwenyeji mwenye
staha kama mfalme. Kiu ilipozidi kumkeketa koo alisalimu amri. Mfalme alifahamishwa. Na kama
aliyejua alichoitiwa akaja na kigudulia kidogo chenye nakshi ya dhahabu na kifuko cha hariri. Alikuwa
radhi kumpa mgeni sharubati ya kukata kiu ila kwa masharti. Anapokunywa maji ameze na zawadi
atakayompa ambayo angeitapika afikapo nyumbani.
Keshowe mgeni aliagwa kwa mbwewe na taadhima. Akaanza safari iliyochukua takriban mwezi mmoja.
Baada ya miezi kumi, Mstahiki Salamwana Salamwene alipata risala kuwa Binti wa Mfalme alikuwa
ameitapika zawadi aliyopewa kama alivyokuwa amekula yamini. Hicho kikawa kitendawili kwa watu
wengi. Wakabaki wakiulizana jibu la fumbo hilo.

Maswali
1. Ipe hadithi hii anwani mwafaka.
2. Kwa nini ilisemekana asili ya Mfalme Salamwana ilikuwa kitendawili?
3. Eleza sifa sita za mfalme zinazojitokeza kwenye kifungu.
4. Ni watu gani walikuja kwa mfalme.
5. Mfalme alitumia hekima gani kutambua ua la bandia.
6. Ni zawadi gani aliyopewa Binti mfalme aliyoitapika alipofika nyumbani?
7. Ni ujumbe upi unaopatikana kutoka na hadithi hii.
8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu.
i. Maguduli
ii. Sharubati
iii. Dhati
iv. yamini

  

Answers


Kavungya
1. Hekima ya mstahiki Salamwana

2. Alichukuwa muda mrefu kuzaliwa huku akiwasiliana na mamake akiwa tumboni

3. Alikuwa na hekima, maarifa, busara, alipenda zaraa,alipenda mafumbo,alikuwa
mjanja,alikuwa na utajiri mkubwa.

4. Watu kutoka mbali, wenye shida,wahuni, matajiri,vijana,wazee,maskini na
watoto wa kifalme.

5. Nyuki huvutiwa na ua halisi lenye chavua

6. Alipewa uja uzito

7. Maguduli-vibuyu vya maji
Sharubati-maji ya matunda
Dhati-kweli
Yamini-weka ahadi
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 05:25


Next: Identify the silent letters in the following wordsi) Honourii) Couldiii) Badgeiv) Receipt
Previous: Eleza sifa za sauti zifuatazo: /o/ /Sh/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions