W na y
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 05:30
- Eleza sifa za sauti zifuatazo:
/o/
/Sh/(Solved)
Eleza sifa za sauti zifuatazo:
/o/
/Sh/
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea
kama moto nyikani msimu wa...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea
kama moto nyikani msimu wa kiangazi.
Mstahiki Salamwana Salamwene, maana hili ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mtu wa ajabu sana. Asili
yake yenyewe ilikuwa kitendawili. Inasemekana mamake alibeba mimba iliyopita miezi tisa. Na kila
aliposhangaa alisikia sauti tumboni ikisema. “Mama kuwa na subira, bado ninalainisha lugha yangu”
Baada ya muda mama alipolalamika alisikia, “Mama ninakaribia, ninamalizia kunoa ubongo wangu.”
Halafu siku moja ikanyesha mvua kubwa iliyoandamana na radi. Waliokuwepo wanasema waliona
mmweso mkali ulioangaza hata kwenye milima mikubwa. Salamwene akazaliwa. Moja ya sifa zake
kubwa ilikuwa hekima na maarifa ya ajabu. Hakuna tatizo la watu wake ambalo alishindwa kulitatua.
Watu wakawa wanafunga safari za siku nyingi kutoka mbali kuja kwenye ikulu yake. Wengi walienda kwa
shida za dhati lakini wengine walikuja kumjaribu.
Siku moja akaja mfanyabiashara tapeli na maua ya aina akamwambia, “Mstahiki mfalme, mtu wako
anataka kuniuzia maua haya kwa vipande vingi vya almasi name nina shaka kuwa moja ni la bandia
waweza kuniamulia?” Mfalme hakujibu. Naye inasemekana alipenda zaraa na hivyo alikuwa na miti na
mimea iliyozaa maua na kutoa harufu anuwai. Basi akaja nyulu na kutua kwenye ua moja. Mfalme
Salamwana akamtambulisha ua halisi.
Muda ukayoyoma huku wahitaji wakiingia ikulu na kutoka. Siku moja akaja Binti mfalme mmoja kutoka
nchi ya mbali na msafara mkubwa. Alipokewa kwa taadhima. Alikaa mwezi mmoja. Kila siku alikaa
kwenye baraza akishuhudia mfalme akiyatatua matatizo ya watu. Jioni walikaa na mfalme pamoja
wapambe wao akijifunza kutoka kwenye hazina kubwa ya busara ya Mstahiki Salamwana.
Usiku uliotangulia kuondoka kwa mgeni, Salamwana alitoa amri za ajabu. Kwanza, aliamuru magudulia
yote ya maji kwenye chumba cha kulala mgeni yabadilishwe. Pili, alimwamuru mpishi kupika chakula
kilichokolea viungo kutoka Bara Hindi. Tatu, aliwaamuru wapambe kuwa mgeni akiomba chochote
wasimpe ila wamfahamishe. Usiku huo, mgeni alihisi kiu kikali lakini aliponyanyua gudulia kumimima
maji kwenye bilauri ya dhahabu, halikuwa na maji. Akajaribu la pili, magudulia yote ya shaba yaliyokuwa
chumbani hayakuwa na maji. Alijitahidi kuvumilia lakini wapi! Ilibidi atafute msaada kwa wapambe nao
wakamweleza walivyoambiwa. Mwanzoni aliona ni kukosa fadhila kumsumbua mwenyeji mwenye
staha kama mfalme. Kiu ilipozidi kumkeketa koo alisalimu amri. Mfalme alifahamishwa. Na kama
aliyejua alichoitiwa akaja na kigudulia kidogo chenye nakshi ya dhahabu na kifuko cha hariri. Alikuwa
radhi kumpa mgeni sharubati ya kukata kiu ila kwa masharti. Anapokunywa maji ameze na zawadi
atakayompa ambayo angeitapika afikapo nyumbani.
Keshowe mgeni aliagwa kwa mbwewe na taadhima. Akaanza safari iliyochukua takriban mwezi mmoja.
Baada ya miezi kumi, Mstahiki Salamwana Salamwene alipata risala kuwa Binti wa Mfalme alikuwa
ameitapika zawadi aliyopewa kama alivyokuwa amekula yamini. Hicho kikawa kitendawili kwa watu
wengi. Wakabaki wakiulizana jibu la fumbo hilo.
Maswali
1. Ipe hadithi hii anwani mwafaka.
2. Kwa nini ilisemekana asili ya Mfalme Salamwana ilikuwa kitendawili?
3. Eleza sifa sita za mfalme zinazojitokeza kwenye kifungu.
4. Ni watu gani walikuja kwa mfalme.
5. Mfalme alitumia hekima gani kutambua ua la bandia.
6. Ni zawadi gani aliyopewa Binti mfalme aliyoitapika alipofika nyumbani?
7. Ni ujumbe upi unaopatikana kutoka na hadithi hii.
8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu.
i. Maguduli
ii. Sharubati
iii. Dhati
iv. yamini
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika visawe vya viwakifishi hivi.
(i)Nukta-
(ii)Koma –
(iii)Mkwaju-
(iv)Mtajo-(Solved)
Andika visawe vya viwakifishi hivi.
(i)Nukta-
(ii)Koma –
(iii)Mkwaju-
(iv)Mtajo-
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.(Solved)
Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi.
(i) Mwalimu anaandika .
(ii) Mwalimu anaandika ubaoni.(Solved)
Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi.
(i) Mwalimu anaandika .
(ii) Mwalimu anaandika ubaoni.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Kamilisha methali.
Mgagaa na upwa(Solved)
Kamilisha methali.
Mgagaa na upwa
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili.(Solved)
Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Tofautisha sauti
/r/ na /l/(Solved)
Tofautisha sauti
/r/ na /l/
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Sahihisha sentensi hizi
(i)Mtoto amerara usingizi mnono.
(ii)Papu yangu ni mzee kiazi.(Solved)
Sahihisha sentensi hizi
(i)Mtoto amerara usingizi mnono.
(ii)Papu yangu ni mzee kiazi.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Tenga silabi na uainishe katika neno
Muhtasari
(Solved)
Tenga silabi na uainishe katika neno
Muhtasari
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Weka shadda neno barabara kuonyesha maana ya shwari na baraste.(Solved)
Weka shadda neno barabara kuonyesha maana ya shwari na baraste.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu.(Solved)
Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- UFAHAMU
Ajira ya watoto
Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa
karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.(Solved)
UFAHAMU
Ajira ya watoto
Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa
karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.Fauka ya hayo,walininginia katika umaskini
uliokithiri.Hivyo,wengi waliselea katika kazi za kijungu jiko.Watot wa umri wa kwenda shule
walikosa elimu na kuzurura mitaani.Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu,tajiri mmoja aliyemiliki
shamba kubwa.Aliwaajiri watoto hao.
Mwakisu alikuwa mkwasi alietononoka si haba.Kama ni senti ,alikuwa nazo.Kilichotia doa
jina lake ni kiburi.Mbali na kiburi hicho,yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu.
Hakubarikiwa kuwa mwema .Maadili hutuongoza kila mara kuwa ‘wema hauozi’.
Kwa Mwakisu,wema ulioza na kuvunda .Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na
ukawa msamiati aliouchukia.Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule.Tabia
yake hiyo ndiyo iliyowafanya Wavuruni kumtoa katika orodhayao ya watu wema.
Mwakisu alistaajabisha!Hakutaka kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa
alikuwa nao uwezo.Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu.Mkwasi huyu alifurahia
kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa
ujira mdogo.
Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote ,kwani tuna shida
nyumbani.” Mwasiku alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza.Hapo alimchomolea mwajiriwa
wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua.Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi
kulisahau.Lilikaririwa akilini mwake kwa sonono.Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na
Mwakisu ni kufadhiliwa u chini.
Kiburi cha mwakisu kilidhihirika kila mara .Kila alipomwona motto akilia kwa uchovu au
maumivu ,ungemsikia akimfokea ,”Chapa kazi!Unalilia nani hapa?Kama humudu kazi rudi kwa
mamako ukanyonye.”
Kazi nyingi zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo.Si kipupwe, si
kaskazi,si vuli,si kiangazi ,si kusi:kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto.Kingi,kwa
mfano,alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa .Kisha
angewakatia mg’ombe nyasi na kuwasafisha .Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.
Msimu wa kipupwe uliwadia.Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingin
aliugua.Watoto wengi wakapatwa na maradhi.Wawili wakaaga dunia.Wazazi walipoona maisha ya
watoto wao yamo hatarini,wakaandamana hadi kwa Mwakisu.tajiri huyo aliwajia kwa meno ya
juu,’msiniitie kibuhuti.Mimi niliwaajiri watoto,sio watoto na wazazi wao”.Wazazi wakatanabahi
kuwa , ‘Pa shoka hapaingii kisu’.Waliandamana hadi kwa chifu.Chifu alipoyaona yamempita
kimo,akafululiza hadi kituo cha polisi.
Mwakisu akakamatwa ,akashtakiwa na kuhukumiwa .Alipatikana na makosa ya kuwaajiri
watoto wenye unri mdogo na kusababisha vifo vya wawili hao.
Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni.Ikatoa pia misaada ya
kuendeleza elimu;elimu ya bure kwa shule za msingi.Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo
kikuu.Akawa daktari.
Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu.Kingi akampa huduma mzee
aliyejawa mvi na kukoboka meno.Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.
Mwakisu akabahatisha,”sura yako….ni kama Kingi…”Kingi akamjibu,”Mimi ndiye
Kingi.”Wakakondoleana macho, huku machozi yakimtiririka Mwakisu.
Maswali
1.Toa kichwa kingine kwa habari hii.
2.Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni.
3.Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao?
4.Taja kazi alizofanya Kingi.
5. Mwasiku alishtakiwa kwa makosa gani?
6.Eleza maana ya semi hizi.
(a)Kazi ya kijungu jiko.
(b)Tononoka si haba.
(c)Kodolea macho.
7.Toa maana ya methali hizi:
(a)Wema hauozi.
(b)Pa shoka hapaingii kisu.
8.Toa maana ya msamiati huu kama ulivyoptumiwa katika makala:
(a)Fauka ya
(b)Alistahabu
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Taja mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha.
(Solved)
Taja mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Onyesha silabi inayowekewa shadda kwenye maneno yafuatayo.
Karatasi –
Shairi –
Barabara(njia kuu)
Mto –(Solved)
Onyesha silabi inayowekewa shadda kwenye maneno yafuatayo.
Karatasi –
Shairi –
Barabara(njia kuu)
Mto –
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Toa neno kwa kila moja ya sauti ambatano zifuatazo.
Nyw –
Nd –
Ngw –(Solved)
Toa neno kwa kila moja ya sauti ambatano zifuatazo.
Nyw –
Nd –
Ngw –
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Onyesha Nomino (N), kitenzi , kielezi (E) Kiunganishi (U), na kivumishi (v) katika sentensi hizi.
(i) Mtoto anacheza vizuri.
(ii) Utacheza au utasoma?
(iii) Wanafunzi wawili wanalala.(Solved)
Onyesha Nomino (N), kitenzi , kielezi (E) Kiunganishi (U), na kivumishi (v) katika sentensi hizi.
(i) Mtoto anacheza vizuri.
(ii) Utacheza au utasoma?
(iii) Wanafunzi wawili wanalala.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Kanusha sentensi zifuatazo.
(i) Mkulima analima shamba.
(ii) Mwanafunzi anasoma kitabu.(Solved)
Kanusha sentensi zifuatazo.
(i) Mkulima analima shamba.
(ii) Mwanafunzi anasoma kitabu.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:-
(i) Mama anaanika nguo
(ii) Baba anaenda sokoni.
(Solved)
Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:-
(i) Mama anaanika nguo
(ii) Baba anaenda sokoni.
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)
- Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi?
Ngoma –
Ukuta –
MachoUgonjwa –
Mmea –
Maiti –(Solved)
Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi?
Ngoma –
Ukuta –
MachoUgonjwa –
Mmea –
Maiti –
Date posted: November 21, 2022. Answers (1)