Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata Leo hii suala la kuwaonyesha watoto mapenzi ni suala la ziada. Kuna mambo mengine mengi maishani mwetu ambayo tunayachukulia kuwa...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata
Leo hii suala la kuwaonyesha watoto mapenzi ni suala la ziada. Kuna mambo mengine mengi
maishani mwetu ambayo tunayachukulia kuwa muhimu zaidi. Ni vizuri tuwaokoe watoto
wetu, tusije tukawalilia baadaye. Kuna vitendo vya ukatili ambavyo watoto hutendewa.
Hivi majuzi tumekuwa na visa vya vilenge kung’olewa mimbani viumbe hawa
walipokatiziwa uhai, maiti zao zilitupwa kama takataka. Hiyo ni miili ambayo ilipatikana je,
ni maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa? Hii tu ilikuwa tone ndogo tu la
bahari ya dhambi ambazo zote tunaogelea ndani.
Mambo kama haya ni mazao ya mimea yetu ambayo tulipanda sisi ambao hatuchelewi kujiita
watu walio huru, walio na maendeleo na wa kisasa. Tumekuwa watu wa kupuuza mambo ya
kimapokeo ya kuzingatia utu na kuficha aibu aghalabu tumejitia usasa kwa kutazama filamu
na video chafu, kusikiliza muziki wenye maneno machafu. Tunapoona watoto wetu
wakitembea nusu uchi, hatushughuliki hata kidogo kuwakanya.
Kama ni kosa, sisi sote tumehusika kwa njia moja au nyingine kwa njia tofauti. Ni vizuri
tuelewe kuwa sisi ni wakuuzaji na walizi wa ndugu zetu kwa kila njia.
Tutawaokoa watoto kwa kukataa mambo yote yanayowanyanyasa. Lazima tuwaonyeshe
watoto mapenzi, mapenzi si chakula, mavazi na makazi tu. Mapenzi si kuwaachia vijana
uhuru watende watendavyo. Mapenzi sio kuwanunulia watoto vitu vya bei ghali au kuacha
kuwakemea wanapokosa mwelekeo.
Mapenzi kwa watoto ni kuwaheshimu na kuwatendea kama binadamu yeyote. Lazima mzazi
akumbuke kwamba mtoto hujifunza kutoka kwake. Mtoto atakutendea isitoshe jinsi
unavyomtendea. Isitoshe jinsi unavyomtendea mtoto wako ndivyo atakavyowatendea watoto
wake na wale wote ambao atapata kuhusiana nao kwa njia moja au nyingine.
Tuwaokoe watoto wetu katika viwango vyote vya ukuaji. Kusiwe na mwanya baina ya mzazi
na mtoto. Watoto wawe kutuambia yote yanayowahangaisha mioyoni mwao, na hali hii
itawapa wazazi fursa ya kuwasaidia. Mtoto anapokosa, tuwe tayari kumwonyesha kosa lake
na kumwadhibu kwa mapenzi.
Mtoto wa mwenzetu akipotoka pia tuwe tayari kumkosoa na kuwaarifu wazazi wake.
Tuwache ubinafsi wetu kumbuka kuwa mwana wa mwenzio ni wako. Ni jambo la busara
kuhakikisha kuwa kama wazazi, tuzingatie haki zote za watoto.

Maswali
1. Kwa nini suala la kuwaonyesha watoto mapenzi limekuwa la ziada.
2. Ni mambo gani ambayo yanaweza kutufanya tuwalilie watoto wetu baadaye?
3. Toa sababu zinazowafanya watu kuavya mimba.
4. Ni mambo yapi ambayo yanachangia kupotoka kwa jamii?
5. Mwandishi ametumia tamathali za usemi. Zitaje huku ukitoa mifano kwa kila mojawapo.
6. Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari.
(a) Vilenge
(b) Mwanya

  

Answers


Kavungya
1. Kwa nini suala la kuwaonyesha watoto mapenzi limekuwa la ziada ?
- Kuna mambo mengine ya muhimu ambayo hushughulikiwa katika maisha yao.

2. Ni mambo gani ambayo yanaweza kutufanya tuwalilie watoto wetu baadaye?
- Watoto wetu wanaweza kupotoka kisha sisi wazazi tujute.

3. Toa sababu zinazowafanya watu kuavya mimba .
- Msichana ambaye hajaolewa
- Wasichana wanapopata mimba wakiwa shuleni
- Wanawake wanaonajisiwa
- Msichana anapokataliwa na mpenziwe
- Mama anapougua na maisha yake kuwa hatarini

4. Ni mambo yapi ambayo yanachangia kupotoka kwa jamii?
- Wazazi kuwa na shughuli nyingi
- Kutowapenda watoto wao
- Kutowatendea kama binadamu na kutowaheshimu watoto
- Mzazi kutokuwa kielelezo chema kwa watoto
- Kukiwa na mwanya baina ya mzazi na mtoto
- Kukiwa na ubinafsi wa kutomkosoa mtoto wa mwenzetu anapokosa na kuarifu.

5. Mwandishi ametumia tamathali za usemi. Zitaje huku ukitoa mifano kwa kila mojawapo.
- Tashbihi – Maiti zilitupwa kama takataka
- Maswali ya balagha – Je, ni maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa ?
- Jazanda – Mambo kama haya ni mazao ya mimea yetu ambayo tulipanga sisi

6. Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari.
(i) Vilenge – Vijusi / watoto wasiofikia umri wa kuzaliwa
(ii) Mwanya – Pengo / nafasi
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 07:01


Next: Kamilisha au kuanzisha methali zifuatazo: i. Fumbo mfumbie……………… ii. Baniani mbaya …………… iii. …………….si kazi kudamirika iv. ………… Sanda.
Previous: Sauti hizi hutamkiwa wapi? /d/ /k/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions