Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.

      

Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.

  

Answers


Kavungya
i) Kuburudisha/kustarehesha/kufurahisha/ kuchangamsha/kusisimua na kupumbaza akili
na kiwiliwili – ujumbe huwasilishwa kwa njia ya kuvutia na kuleta ucheshi
ii) Kuadilisha /kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na
kukataa sifa hasi za wahusika.
iii) Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
iv) Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi
wa fasihi andishi.
v) Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.hizi hupitishwa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
vi) Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
vii)Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v
kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ - Mtu
hawezi kumwoa dadake.
viii) Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma,
kuimba, utambaji, n.k.
ix) Kukuza lugha k.v. ulumbi na misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika
lugha sanifu.
x) Kukuza ubunifu k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.
xi) Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa
au watu waliotendea jamii makuu.
xii)Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 07:44


Next: Sanaa ni nini?
Previous: Read the passage below and then answer the questions that followQuestions abound concerning the sharp increase of low grades in the 2021 KCSE examination results....

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions