Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi barabarani.

      

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi
barabarani. Mara chachemawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya
michezo. Ni nadra sana watu kufikiraia kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinztokea.
Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wanapata
majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile
mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu
wazima hutokana na ajali kama hizi wasizofikiria wtu wengi.
Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali
hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza wengine bila kujua.
Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubebe mizigo yenye uzani wasiokadiria. Madhara huwa
kuteguka viungo na kuchanika misuli. Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya
siku moja alipanda kibao kuangika picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma
kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo
hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya. Kuvunjika jino na hata kuzirai. Bahati ni kuwa alikuwepo
mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini.
Hat hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi,
mashine zinazotumia umeme na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata
kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata
waliokulia katika makasri ya fahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi
yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je una kovu lolote?
Unakumbuka ulivyolipata?
Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa
waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa
mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto
mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri
kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirudisha ipasavyo.
Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.
Inawezekana kuokoa maisha au kuounguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.

Maswali
1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’

2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo?

3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani?

4. Onyesha vile invyowezekana kupunguza ajali nyumbani.

5. Eleza maana ya:
(i) Jazba
(ii) Makasri
(iii) Makovu
(iv) Kuepua

  

Answers


Kavungya
1. Ajali hutokea bila kutarajia

2.
- Hutokana na ajali wasiofikiria watu wengi kama vile kuteleza msalani.
- Aidha wengine huteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni.
- Watu wazima na watotohulemazwa na ajali hizi.

3.
- Watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba ya kutenda kazi
- Kuubeba mzigo wenye uzani usiokadiriwa.
- Ukiwa umepanda juu ya kibao kuangika picha ukutani
- Ajali kutokana na vifaa vya nyumbani k.v. visu, meko ya gasi, mashine zinazotumia umeme n.k.

4.
- kukuza tabia na mazoea ya kuwa waangalifu nyumbani
- Ni vizuri kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirusha ipasavyo
- Kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.

5. (i) Jazba - Msisimko/ msukumo / hamu kuu
(ii) Makasri- Majumba ya kifahari
(iii) Makovu - Alama / mabaki yatokayo na majeraha
(iv) Kuepua - Kutoa kitu mekoni
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 08:19


Next: Read the excerpt below and answer the questions that follow. ‘Ne-yeiyo-ai nanyorr,” he called her pleasantly, his voice warm and cordial. “Yeoo,” she answered, greatly surprised by...
Previous: Read the poem below and answer the questions that follow Mid -Term Break (Seamus Heaney)I sat all morning in the college sick bay Counting bells...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions