Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali. Kibiko: Hujambo dada Cheupe? Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.

      

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
Kibiko: Hujambo dada Cheupe?
Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.
Kibiko: Unaendelea namna gani?
Cheupe: Niko poa isipokuwa maumivu kidogo ya chest.
Kibiko: Usijali nitakupa pain relievers utakuwa sawa.
Cheupe: Asante sana, nashukuru.
Maswali
a) Mazungumzo haya yanapatikana wapi?
b) eleza sifa nne za lugha inayotumika katika mazungumzo haya

  

Answers


Kavungya
a. Hospitalini/zahanatini

b.
- Sentensi fupi fupi.
- Kuchanganya ndimi mfano: chest, pain relievers
- Lugha haizingatii kanuni za kisarufi mfano: niko poa
- Lugha ni ya udadisi
- Msamiati maalum mfano: Pain relievers
- Lugha ya unyenyekevu hasa kwa upande wa mgonjwa
mfano: Asante sana, nashukuru
- Lugha ya matumaini mfano: utakuwa sawa.
- Lugha ya majibizano – Kibiko na Cheupe.
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 08:50


Next: Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.
Previous: Rewrite the following sentences according to the instructions, given without changing the meaning. i) You are asked not to make your work dirty (Rewrite using...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions