Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa
amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika. Walitegemea
matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.
Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa. Ndovu aliathirika zaidi.Alijaribu kuinama majini
lakini hakuweza.Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka.
Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura.Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata.Alihofia kurudi
baharini na hadi wa leo yumo msituni.

Maswali
a. Tambua utanzu na kijipera chake.
b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki.
c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki.
d. Eleza sifa za kifungu hiki.
e. Eleza umuhimu wa fomyula ya Kuhitimisha

  

Answers


Kavungya
a) i) Hadithi
ii) Hurafa

b) i) Hadithi hadithi …… hadithi njoo.
ii) paukwa pakawa

c)
- huburudisha wanajamii
- huhifadhi historia ya jamii.
- Hukuza lugha miongoni mwa wanajamii.
- Huleta wanajamii pamoja.
- Huhifadhi utamaduni wa wanajamii.
- Hukuza ujasiri wa kuzungumza.
- Hukuza uwezo wa kukumbuka
- Huelimisha wanajamii

d)
- Wahusika huwa ni wanyama.
- Wahusika huwa na tabia za binadamu.
- Huhusisha kazi ya ubunifu.
- Hutoa mafunzo kwa njia ya kuchekesha.
- Hutumia mbinu ya uaishaji / tashihisi.
- Hatoa matumaini kwa wanyonge.

e)
- Hutangaza funzo kwa wasikilizaji/ hadhira.
- Humpisha mtambaji anayefuata.
- Hupisha shughuli inayofuata ikiwa kipindi cha utambaji kimekwisha.
- Baadhi ya viishio huwapa hadhira changamoto ya kuwa watambaji mashuhuri wa ngano.
- Huitoa hadhira katika ulimwengu wa ubunifu.
- Huashiria mwisho wa hadithi.
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 08:53


Next: Rewrite the following sentences according to the instructions, given without changing the meaning. i) You are asked not to make your work dirty (Rewrite using...
Previous: Explain the differences between the following sentences i) She paid him to do the work. ii) She paid him for doing the work.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions