1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwa aje kabla ya Evelyn kupata kazi?
i. Walikua marafiki wa chanda na pete
ii. ii. Walishirikiana kwa kila njia
2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa namna gani?
i. Alikua mwenye ukarimu
ii. Alijawa na wema
iii. Alikua na mapenzi ya dhati
3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake.
i. Alimnunulia mahitaji kama nguo na viatu
ii. Alilipa kodi kwa niaba ya Evelyn
iv. Alimlipia faini alipokua kizuizini
4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa.
- La.
- Evelyn alifuatilia raha za jijini na kukosa kumsaidia Rita katika kazi na gharama za maisha
5.Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwanini alianza tabia
hiyo baada ya kuajiriwa?
- Aliona kuwa alikuwa na pesa zake na angeweza kujikimu mwenyewe
- Alidhani kuwa tayari alikuwa mtu mzima na hivyo hakuhitaji kuelekezwa
6. ‘Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusiana aje na Evelyn?
- Evelyn alikataakumskiza Rita nabaadayeakatendakosalililomtiakorokoroni
7. ‘Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusiana aje na Rita?
- Rita alimsadia rafikiye Evelyn alipokuwa mwanafunzi na hata baadaye alipokuwa korokoroni
8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu:
(a) marafiki wa chanda na pete- Marafiki wasioachana kwa vyovyote vile
(b) enda mrama -Kuharibika
(c) jitolea sabili –Kuamua kikamilifu
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 08:59
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa
amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika. Walitegemea
matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.
Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa. Ndovu aliathirika zaidi.Alijaribu kuinama majini
lakini hakuweza.Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka.
Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura.Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata.Alihofia kurudi
baharini na hadi wa leo yumo msituni.
Maswali
a. Tambua utanzu na kijipera chake.
b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki.
c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki.
d. Eleza sifa za kifungu hiki.
e. Eleza umuhimu wa fomyula ya Kuhitimisha
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
Kibiko: Hujambo dada Cheupe?
Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.(Solved)
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
Kibiko: Hujambo dada Cheupe?
Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.
Kibiko: Unaendelea namna gani?
Cheupe: Niko poa isipokuwa maumivu kidogo ya chest.
Kibiko: Usijali nitakupa pain relievers utakuwa sawa.
Cheupe: Asante sana, nashukuru.
Maswali
a) Mazungumzo haya yanapatikana wapi?
b) eleza sifa nne za lugha inayotumika katika mazungumzo haya
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.(Solved)
Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Tumia O’rejeshi badala ya amba-
Wachezaji ambao hucheza kwa bidi ndio ambao hufaulu maishani.(Solved)
Tumia O’rejeshi badala ya amba-
Wachezaji ambao hucheza kwa bidi ndio ambao hufaulu maishani.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji.
(Solved)
Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji.
(Anza: Katika bwawa............)
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi moja kudhihirisha maana ya vitate vifuatavyo:
Kesi/gesi(Solved)
Tunga sentensi moja kudhihirisha maana ya vitate vifuatavyo:
Kesi/gesi
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika matumizi mawili ya mshazari.(Solved)
Andika matumizi mawili ya mshazari.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika katika ukubwa.
Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.(Solved)
Andika katika ukubwa.
Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo:
Mtoto anapendezwa na ziwa.(Solved)
Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo:
Mtoto anapendezwa na ziwa.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Yakinisha katika wingi sentensi ifuatayo:
Mtu asiyeugua anahitaji daktari.(Solved)
Yakinisha katika wingi sentensi ifuatayo:
Mtu asiyeugua anahitaji daktari.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
Kulikuwa kioja kuona marafiki wakipigana.(Solved)
Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
Kulikuwa kioja kuona marafiki wakipigana.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Sahihisha sentensi hii.
Mfua ulionyesha ulisababisha mafuriko.
(Solved)
Sahihisha sentensi hii.
Mfua ulionyesha ulisababisha mafuriko.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika kinyume cha sentensi hii.
Ubane mlango kidogo na umtwike mchukuzi mzigo huu.(Solved)
Andika kinyume cha sentensi hii.
Ubane mlango kidogo na umtwike mchukuzi mzigo huu.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo ili kuonyesha viambishi awali ,mzizi na viambishi tamati.
Walioangaliana(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo ili kuonyesha viambishi awali ,mzizi na viambishi tamati.
Walioangaliana
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Weka Nomino hizi katika ngeli zake.
Raha
Kumbikumbi(Solved)
Weka Nomino hizi katika ngeli zake.
Raha
Kumbikumbi
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Akifisha sentensi hii:
alikufa siku ya jumapili tarehe 20 mwezi wa januari mwaka wa 2011.(Solved)
Akifisha sentensi hii:
alikufa siku ya jumapili tarehe 20 mwezi wa januari mwaka wa 2011.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha mianzo tofauti katika ngeli ya U-ZI.(Solved)
Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha mianzo tofauti katika ngeli ya U-ZI.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha irabu.(Solved)
Andika vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha irabu.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi
barabarani.(Solved)
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi
barabarani. Mara chachemawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya
michezo. Ni nadra sana watu kufikiraia kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinztokea.
Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wanapata
majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile
mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu
wazima hutokana na ajali kama hizi wasizofikiria wtu wengi.
Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali
hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza wengine bila kujua.
Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubebe mizigo yenye uzani wasiokadiria. Madhara huwa
kuteguka viungo na kuchanika misuli. Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya
siku moja alipanda kibao kuangika picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma
kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo
hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya. Kuvunjika jino na hata kuzirai. Bahati ni kuwa alikuwepo
mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini.
Hat hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi,
mashine zinazotumia umeme na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata
kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata
waliokulia katika makasri ya fahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi
yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je una kovu lolote?
Unakumbuka ulivyolipata?
Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa
waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa
mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto
mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri
kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirudisha ipasavyo.
Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.
Inawezekana kuokoa maisha au kuounguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.
Maswali
1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’
2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo?
3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani?
4. Onyesha vile invyowezekana kupunguza ajali nyumbani.
5. Eleza maana ya:
(i) Jazba
(ii) Makasri
(iii) Makovu
(iv) Kuepua
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.(Solved)
Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)