Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi?

      

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
UKANDAJI
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
mbalimbali mwilini.
Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
chembechembe za sumu mwilini.
Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
hayapendekezwi.
Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
mikononi.
Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
maradhi ya ngozi.

MASWALI
(a) Ukandaji ni nini?
(b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
(c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
(d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
(e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
(f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
(i) ufunguzi
(ii) auni
(iii) maradufu
(iv) maji vuguvugu
(v) shinikizo la damu

  

Answers


Kavungya
(a) Ni shughuli ya kusugua na kubinyabinya viungo vya mwili kwa mikono au mashine.

(b)(i) Hufungua vitundu vya ngozi,jambo ambalo husaidia kuondoa sumu mwilini kupitia kwa
utokaji jasho.
(ii) Kupunguza mikazo ya misuli. Mikazo ya misuli mwilini kwa muda mrefu huleta
ulundikaji wa asidi mwilini; jambo ambalo ni hatari.
(iii) Huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi.
Hii hurahisisha virutubishi vya mwili kufika sehemu zote mwilini
(iv) Huondoa uchovu na kuleta uchangamfu mwilini.
(iv) Ukandaji huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wa neva hizo.

(C) Ukandaji unatakiwa kufanywa kwa kutumia mafuta,hasa ya ufuta au simsim kisha mtu
aanzie mikononi na miguuni,aingie kifuani,tumboni,mgongoni na makalioni.
Hatimaye,aingie usoni na kumalizia kichwani,iwapo anayehusika ana tatizo la shinikizo
la damu,utaratibu auazie kichwani kisha aelekee usoni,kifuani,tumboni na kumalizia
mgongoni.

(D) Unatakiwa kufanywa na mtu mwenyewe. Hii ni kwa kuwa atakuwa akijikanda vizuri na
pia atakuwa akifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

(E) -Wakati mtu anaugua maradhi yoyote.
-wakati mwanamke ni mjamzito
-wakati mtu anaendesha,asikande tumbo au akiwa na vidonda vya tumbo
-wakati mtu ana maradhi yoyote ya ngozi

(F)(i) kufungua
(ii) kusaidia,msaada
(iii) Mara mbili
(iv) Maji yasiyo baridi wala moto sana
(v) Mpumuko wa damu au moyo kupiga sana kwa kasi isiyokuwa ya kawaida
Kavungya answered the question on November 23, 2022 at 07:29


Next: David Mulwa, Inheritance “Lacuna represents the evil that bedevils our leaders.” With reference to David Mulwa’s Inheritance, write an essay to support this statement.
Previous: Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja...... a....(Solved)

    Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka
    kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja......
    a. Je, sajili hii inapatikana wapi?

    b. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo: Jembe lililonunuliwa limepotea.(Solved)

    Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo:
    Jembe lililonunuliwa limepotea.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.(Solved)

    Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi ifuatayo. Ukienda mle pao atakuweko. (Solved)

    Sahihisha sentensi ifuatayo.
    Ukienda mle pao atakuweko.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya: Paka na baka(Solved)

    Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya:
    Paka na baka

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo: mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo:
    mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.(Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tambua aina za maneno katika sentensi zifuatazo: Msichana mrembo amechora haraka sana. Yeye ataenda sokoni.(Solved)

    Tambua aina za maneno katika sentensi zifuatazo:
    Msichana mrembo amechora haraka sana.
    Yeye ataenda sokoni.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.(Solved)

    Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi: Silabi funge Silabi wazi Silabi mwambatano(Solved)

    Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi:
    Silabi funge
    Silabi wazi
    Silabi mwambatano

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Eleza sifa za sauti zifuatazo: /e/ /p/(Solved)

    Eleza sifa za sauti zifuatazo:
    /e/
    /p/

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FADHILA ZA PUNDA Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu.(Solved)

    Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali
    FADHILA ZA PUNDA
    Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu. Waliishi katika mtaa wa Kibokoni
    jijini Mombasa. Evelyn alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uhazili katika chuo kimoja pale mjini. Naye
    Rita alifanya kazi ya ukarani papo hapo mjini. Waliishi kidugu katika chumba kimoja walichopanga pale
    mtaani. Ingawa marafiki hawa walishirikiana kwa kila njia katika shughuli za upishi, kupiga deki, kufagia,
    kufua na kazi nyinginezo za nyumbani, aliyekuwa akitoa msaada mkubwa zaidi alikuwa ni Rita. Rita
    alikuwa na mazoea ya kutunza pesa zake vyema. Aidha alijua maana ya haba na haba hujaza kibaba.
    Alijua kuwa Evelyn, kama mwanafunzi, hakuwa na uwezo wa kuyakidhi baadhi ya mahitaji yake.
    Alijitolea sabili hata kumnunulia Evelyn nguo, viatu na vim vingine alivyohitaji. Mara nyingine ilibidi Rita
    kulipa kodi ya nyumba peke yake kwa vile mwenzake hangeweza kupata pesa kwa wakati. Hakuwahi
    hata siku moja kumkera wala kumtesa Evelyn kwa jinsi yoyote ile. Fauka ya hayo, hakuwahi
    kumsemesha vibaya wala kuonyesha dharau kwake. Aliamini kama wanavyosema watu kuwa dunia
    rangi rangile, huenda siku moja atahitaji kusaidiwa yeye pia. Siku kama hiyo atamtegemea Evelyn,
    mwandani wake. Evelyn alipomaliza masomo yake alikuwa na bahati ya mtende. Alipata kazi nzuri mara
    moja katika kampuni moja ya maffita papo hapo jijini. Lakini muda si muda, mambo ya ajabu yalianza
    kutokea. Baada ya kupata kazi yenye kipato kizuri, kichwa cha Evelyn kilianza kufura mfano wa kaimati.
    Badala ya kunisaidia mwenzake katika kazi za pale nyumbani pamoja na gharama za maisha, alifhatilia
    raha za jijini kwa kuamini ule msemo wa ponda raha kufa kwaja. Rita alipomwuliza alimjibu kwa ukali,
    “Nikusaidie nini? Sasa si kama wakati nilipokuwa mwanafunzi. Kila mtu ana pesa zake.Ala!” Rita
    hakumwelewa tena Evelyn.Isistoshe, alianza kumwibia Rita vitu vyake wakati alipokuwa hayupo
    nyubani. Mara kwa mara Rita aligundua kuwa pesa alizokuwa ameficha sehemu Fulani nyumbani
    zimedokolewa. Alipomwuliza, Evelyn alikujajuu, “Unafikiri mimi sina pesa? Unadhani ni wewe tu
    uliyeajiriwa?” Rita alizidi kushangaa, Muda wote alioishi na kumfadhili rafiki yake aliamini kuwa atamlipa
    mema. “Kumbe fadhila za punda ni mateke?” Alijiuliza Rita. Baada ya muda, urafiki wao ulivunjika na
    Evelyn akahamia mtaa wa Furaha alikoendelea na maisha yake ya starehe na ureda. Hata hivyo mambo
    yalianza kumwendea mrama Evelyn. Wakubwa wake kazini hawakupendezwa najinsi alivyoendesha
    shughuli zake pale ofisini. Mara nyingi alifika kazini akiwa amechelewa na kila wakati alitoa vijisababu
    mbalimbali ambavyo havikumridhisha yeyote. Aidha, alipokuwa ofisini hakufanya mengi isipokuwa
    kutembea kutoka ofisi hii hadi nyingine akiwasumbua watu kazini mwao. Mara kwa mara alionekana
    akisinzia wakati wenzake walipokuwa wakichapa kazi. Lakini lililowakera zaidi wakuu wa kampuni hiyo
    ya mafuta ni jambo fulani lililoanza kutendeka pale. Vitu vya watu vilianza kupoteapotea.Mara
    mfanyikazi huyu anapoteza saa yake, mara mwingine anapoteza pesa, mara hiki mara kile. Wakuu
    walipoyatupa mawazo yao nyuma wakagundua kuwa mambo haya yalianza kutendeka mara tu
    alipowasili Evelyn. Wakaamua kumwekea mtego. Evelyn alioshikwa kimasomaso akidokoa mkoba wa
    msichana mwenzake. Mkoba huo ulikuwa umeaehwa juu ya dawati kimakusudi ili kumvuta Evelyn.
    Evelyn alifutwa kazi papo hapo. Fauka ya hayo, alitiwa mikononi na kukabidhiwa poisi waliomtupa
    korokoroni. Kesho yake Evelyn alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la wizi. Alitozwa faini ya
    shilingi elfu tano au kifungo cha miezi sita. Hakuwa na pesa zozote za kulipia faini hii. Akawekwa
    rumande. Hata rafiki mmoja hakuwa naye wa kumuauni katika wakati huo wa majaribu. Kwa bahati, Rita
    alisikia kuhusu kadhia hiyo.Hakupoteza muda. Akashika njia moja kwa moja hadi kituo cha polisi.
    Mpango ukafanywa na akamlipia. Evelyn ile faini. Evelyn alipoachiliwa hum akashangaa. “Yaani
    nimesamehewa ama nini?”Aliuliza.“La. Hujasamehewa.Faini uliyotozwa imelipwa na msichana yule.”
    Evelyn akageuka na kumwona Rita. Alimtazama kwa muda bila kujua la kusema. Mwishowe alimsogea
    kisha wakakaribiana polepole na kukumbatiana. Machozi yakaanza kumdondoka Evelyn, nde! Nde! Nde!
    Akalia kilio cha uchungu na soni. Akamwomba Rita msamaha, “Nisamehe, sikujua nililokuwa
    nikifanya.Nilidhani kuwa baada ya kupata kazi sitahitaji tena urafiki wako. Haya yaliyonipata
    yamenifunza,” alisema kwa masikitiko. “Evelyn, kijengacho mtu ni uth na tabia,” alisema Rita.“Ni kweli
    rafiki yangu” alitamka Evelyn, Sasa nimejitia kwenye shida.Hata kazi yangu nzuri nimeipoteza.Sina
    mahali pa kuishi. Itabidi nirudi kijijini kwa baba na mama. Kwaheri rafiki yangu naasante kwa yote
    uliyofanya.”“La! Hutaondoka”. Rita alimwambia lcwa dhati, “Tutakwenda nawe nyumbani mwangu
    tukaishi pamoja kama zamani. Nitayagharamia mahitaji yako yote hadi utakapopata kazi”. Basi Rita na
    Evelyn wakaungana tena na kuishi vizuri katika nyumba ile ile mtaani Kibokoni. Kweli akufaaye kwa dhiki
    ndiye rafiki.

    MASWALI:
    1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi?
    2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa ama gani?
    3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake.
    4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa.
    5. Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwa nini alianza tabia
    hiyo baada ya kuajiriwa?
    6. ‘Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusianaje na Evelyn?
    7. ‘Akufaaye ukiwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusianaje na Rita?
    8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu: (alama 3)
    (a) marafiki wa chanda na pete
    (b) enda mrama
    (c) jitolea sabili

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa
    amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika. Walitegemea
    matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.
    Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa. Ndovu aliathirika zaidi.Alijaribu kuinama majini
    lakini hakuweza.Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka.
    Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura.Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata.Alihofia kurudi
    baharini na hadi wa leo yumo msituni.

    Maswali
    a. Tambua utanzu na kijipera chake.
    b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki.
    c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki.
    d. Eleza sifa za kifungu hiki.
    e. Eleza umuhimu wa fomyula ya Kuhitimisha

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali. Kibiko: Hujambo dada Cheupe? Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.(Solved)

    Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Kibiko: Hujambo dada Cheupe?
    Cheupe: (Akikohoa) Sijambo ndugu Kibiko.
    Kibiko: Unaendelea namna gani?
    Cheupe: Niko poa isipokuwa maumivu kidogo ya chest.
    Kibiko: Usijali nitakupa pain relievers utakuwa sawa.
    Cheupe: Asante sana, nashukuru.
    Maswali
    a) Mazungumzo haya yanapatikana wapi?
    b) eleza sifa nne za lugha inayotumika katika mazungumzo haya

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.(Solved)

    Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tumia O’rejeshi badala ya amba- Wachezaji ambao hucheza kwa bidi ndio ambao hufaulu maishani.(Solved)

    Tumia O’rejeshi badala ya amba-
    Wachezaji ambao hucheza kwa bidi ndio ambao hufaulu maishani.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa. Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji. (Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
    Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji.
    (Anza: Katika bwawa............)

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kudhihirisha maana ya vitate vifuatavyo: Kesi/gesi(Solved)

    Tunga sentensi moja kudhihirisha maana ya vitate vifuatavyo:
    Kesi/gesi

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika matumizi mawili ya mshazari.(Solved)

    Andika matumizi mawili ya mshazari.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa. Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.(Solved)

    Andika katika ukubwa.
    Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)