Vijijusi/vijusi vilivyokuwa na vijicho vilianguka vijitoni
Kavungya answered the question on November 24, 2022 at 06:50
- Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
Ritifaa(Solved)
Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
Ritifaa
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
(i) Nafsi viambata
(II) Visisitizi(Solved)
Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
(i) Nafsi viambata
(II) Visisitizi
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
Mtoto mbaya aliadhibiwa(Solved)
Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
Mtoto mbaya aliadhibiwa
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo.
(i) Anayetaka chakula kitamu ni nani?
(ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio. (Solved)
Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo.
(i) Anayetaka chakula kitamu ni nani?
(ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio.
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
(i) shuka
(ii) suka (Solved)
Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
(i) shuka
(ii) suka
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Eleza maana ya misemo ifuatayo.
(i) kupiga domo
(ii) kupiga kijembe(Solved)
Eleza maana ya misemo ifuatayo.
(i) kupiga domo
(ii) kupiga kijembe
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo.
(i) Nyanchama hakufika mkutanoni
(ii) Horukut amerudi kutoka masoni(Solved)
Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo.
(i) Nyanchama hakufika mkutanoni
(ii) Horukut amerudi kutoka masoni
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
(i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
(ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.(Solved)
Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
(i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
(ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa. (Solved)
Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa.
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Eleza tofauti kati ya:
(i) Mofimu huru
(ii) Mofimu tegemezi (Solved)
Eleza tofauti kati ya:
(i) Mofimu huru
(ii) Mofimu tegemezi
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/ (Solved)
Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/
Date posted: November 24, 2022. Answers (1)
- Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani
madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe...(Solved)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani
madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe kumwadhibu kwa makosa aliyofanya bali iwe kumtibu na kujaribu
kumrekebisha tabia yake ili awe raia mwema.
Zamani wahalifu waliadhibiwa kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya. Mhalifu aliyefanya makosa
madogo madogo alifungwa lakini mtu aliyeua naye aliuawa. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa mhalifu
akiadhibiwa anapokuwa kifunguno,basi akitoka hurejea tena kufanya uhalifu. Madhumuni ya kumtia jela iwe si
kumwadhibu bali kumfunza tabia njema. Wanatuambia kuwa makosa afanyayo mhalifu yanatokana na
matatizo ya jamii kwa jumla,nayo ni matatizo kama ya umaskini, msongamano wa watu, kosa afanyalo mhalifu
si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii nzima.
Jitu lilizoea kuua halioni kitu kumpiga mtarimbo au rungu la kichwa na kumyang’anya kila alicho
nacho. Siku hizi,jitu kama hili baadhi ya wataalamu husema lisiuawe lifungwe maisha tu. Lakini ‘kifungo cha
maisha’ ni kama tunavyokijua. Muuaji hufungwa pengine miaka kumi tu kisha husamehewa muda uliobaki.
Hapo tena huwa huru ama kuifichua mali aliyoiiba na kuistarehea raha mustarehe au kurejea tena kufanya
uhalifu.
Haya ni kinyume kabisa na mambo yalivyokuwa zamani. Aliyeua aliuawa kwa hivyo watu waliogopa
kuua. Raia na pia askari waliokuwa wakiwasaka wahalifu walinusurika vifo kwani wahalifu wengine
walichukua silaha za hatari kama bastola na bunduki.
Sasa wale wahalifu wabaya sana – mijizi, minyang’anyi na wauaji ndio wanaotukuzwa. Magazeti
huwashawishi makatili hawa na kuwapa mapesa chungu nzima waeleze maisha yao ya kikatili. Magazeti haya
sasa ndiyo yanayopata wasomaji wengi. Pia wachapishaji vitabu vya hadithi zinazohusikia na uhalifu, biashara
zao zinazidi kustawi. Kadhalika sinema zinazoonyesha picha za ukatili; wizi na mauji hujaa watazamaji
wanaoshangilia uhalifu ufanywao.
Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na masinema vitabu na magazeti na kwa upande mwingine
“haki” zao zinapiganiwa na baadhi ya wataalamu. Watu wanaowalaani wahalifu ni wale waliohasirika tu na
kuteswa na wahalifu . Baadhi yao hata kulaani hawawezi kwa sababu wameshauawa,hawana tena kauli.
MASWALI
(a) Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno 50.
Matayarisho
Nakala safi
(b) Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno kati ya 45-50
Matayarisho
Nakala safi
Date posted: November 23, 2022. Answers (1)
- Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
UKANDAJI
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi?(Solved)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
UKANDAJI
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
mbalimbali mwilini.
Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
chembechembe za sumu mwilini.
Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
hayapendekezwi.
Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
mikononi.
Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
maradhi ya ngozi.
MASWALI
(a) Ukandaji ni nini?
(b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
(c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
(d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
(e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
(f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
(i) ufunguzi
(ii) auni
(iii) maradufu
(iv) maji vuguvugu
(v) shinikizo la damu
Date posted: November 23, 2022. Answers (1)
- Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka
kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja......
a....(Solved)
Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka
kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja......
a. Je, sajili hii inapatikana wapi?
b. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo:
Jembe lililonunuliwa limepotea.(Solved)
Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo:
Jembe lililonunuliwa limepotea.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.(Solved)
Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Sahihisha sentensi ifuatayo.
Ukienda mle pao atakuweko.
(Solved)
Sahihisha sentensi ifuatayo.
Ukienda mle pao atakuweko.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya:
Paka na baka(Solved)
Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya:
Paka na baka
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Akifisha sentensi ifuatayo:
mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema(Solved)
Akifisha sentensi ifuatayo:
mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)
- Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.(Solved)
Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.
Date posted: November 22, 2022. Answers (1)