Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza

      

Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali
CHEMA HAKIDUMU
Chema hakidumu, kingapendekeza,
Saa ikitimu, kitakuteleza
Ukawa na hamu, kukingojeleza,
Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza
Chema sikiimbi, kwamba nakitweza
Japo mara tumbi, kinshaniliza,
Na japo siombi, kipate n’ongeza,
Mtu haniambi, pa kujikimbiza
Chema mara ngapi, kinniondoka,
Mwanangu yu wapi? Hakukaa mwaka,
Kwa muda mfupi aliwatilika,
Ningefanya lipi, ela kumzika?
Chema wangu babu, Kibwana Bashee,
Alojipa tabu, kwamba anilee
Na yakwe sababu, ni nitengenee,
Ilahi Wahhabu, mara amtwee.
Chema wangu Poni, kipenzi nyanyangu,
Hadi siku hini, yu moyoni mwangu,
Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
Ningamtamani, hatarudi kwangu.
(Abdalla, Abdilatif, Sauti ya Dhiki)

MASWALI:
(a) Hili ni shairi la aina gani?
(b) Taja na ueleleze aina zozote mbili za bahari katika shairi hili.
(c) Eleza umbo la shairi hili.

  

Answers


Kavungya
(a) Hili ni shairi la aina gani?
Shairi hili ni la tarbia kwa kuwa lina mishororo minne katika kila ubeti.

(b) Taja na ueleleze aina zozote mbili za bahari katika shairi hili.
- Ukaraguni – Vina vya ukwapi na utao vinabadilika.
- Kikwamba – Ambapo neno “chema” limeanza beti zote.
- Ukara – Kina cha ukwapi kinabadilika bali cha utao hakibadiliki
- Mathnawi – limegawika katika vipande viwili.

(c) Eleza umbo la shairi hili.
- Shairi hili lina mishororo minne katika kila ubeti.
- Shairi hili lina vipandeviwili katika kila mshororo
- Shairi hili lina mizani sita katika kipande cha kwanza na sita katika kipande cha
pili.
- Shairi hili lina vina vina vya kati ni vya mwisho ambavyo vinabadilika kutoka ubeti
mmoja hadi mwingine.
- Shairi hili lina kichwa/mada ambayo ni “chema hakidumu.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 05:37


Next: Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa. Mtakula nini?
Previous: Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (i) Nazali ya kaa laini (ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno (iii) Irabu ya nyuma wastani (iv) Kimadende

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions