Kuta zilizojengwa zimebomoka.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 06:39
- Kamilisha methali ifuatayo.
Asiye na nadhari...(Solved)
Kamilisha methali ifuatayo.
Asiye na nadhari...
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Andika kwa wingi.
Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.(Solved)
Andika kwa wingi.
Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi.
Mvule alikuwa akilala bwenini.(Solved)
Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi.
Mvule alikuwa akilala bwenini.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa.
Uteo alionunuliwa umezeeka sana.(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa.
Uteo alionunuliwa umezeeka sana.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Yakinisha:
Usipolipa usiingie ndani.(Solved)
Yakinisha:
Usipolipa usiingie ndani.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya
i. Posa
ii. Poza(Solved)
Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya
i. Posa
ii. Poza
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.
Kimbia haraka –
Amka -(Solved)
Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.
Kimbia haraka –
Amka -
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.(Solved)
Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.(Solved)
Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja.
Nywele zenu hukatika mnapoachana.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja.
Nywele zenu hukatika mnapoachana.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.(Solved)
Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani?
i. / f /
ii. / l /(Solved)
Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani?
i. / f /
ii. / l /
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali
Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili
awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali
Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili
awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.
Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima
nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na
kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.
Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika.
Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa kilimo alitangazaa bei mpya , shilingi 1,500 kwa kila
gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu.
Baada ya taarifa, nilioga nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi
ulinichukuwa mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa
kulima nilitenga hekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima
ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi
1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Mechi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya
shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu
kumi na tatu kupiga shamba lote haro.
Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500
kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa
kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda ili nipate mazao
bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada
ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii
iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu
mchangani.
Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo
yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa
yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo
‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo , nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia
kumi na matano.
Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi
yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia
waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa
kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu
mavuno nitakayopata na kukadiri faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani,
mnyama hajauawa.’
Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza
kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu
vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.
Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha , muda si
muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililowavunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua
kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa
limetapakaa barafu nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi
yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.
Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kasha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu
wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000 kuvuna kusafirisha
kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo
nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya
dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi
yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona
gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa ‘MAHINDI GUNIA 900/=’ Niligutuka usingizini.
MASWALI
a) Ni changamoto zipi zinazokumba kilimo.
b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika?
c) Eleza maana ya methali zifuatazo kwa mujibu wa makala.
i. Usikate majani, mnyama hajauawa.
ii. Muumba ndiye Muumba.
d) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.
e) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu?
f) Eleza maana ya:
i. Kiinua mgongo
ii. Manyakanga wa kilimo.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Bainisha nomino katika utungo huu.
Watoto wameenda kucheza.(Solved)
Bainisha nomino katika utungo huu.
Watoto wameenda kucheza.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake. (Solved)
Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Andika udogo wa:
Anacheza ngoma.(Solved)
Andika udogo wa:
Anacheza ngoma.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi.
Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.(Solved)
Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi.
Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii.
Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.(Solved)
Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii.
Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu. (Solved)
Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani.
(i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu.
(ii) Kitabu cha Musa hakipo(Solved)
Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani.
(i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu.
(ii) Kitabu cha Musa hakipo
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)