Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza

SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
Malezi mema
Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza
Atafikia kilele, mzazi atampuza
Utapiga makelele, wala hatasikiza.
Daima usikubali, kuridhi kumpendeza
Lazima uwe mkali, mengine kumkataza
Na wala usikubali, maneno kuyaigiza.
Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza
Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza
Ama dakika zapita,aje ikimpendeza.
Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza
Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza
Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza.
Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza
Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza
Lau usipomrudi, kosa taliendeleza.

Maswali
a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi.
b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda
c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto
d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili
e) Shairi hili lina mishororo ngapi
f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili
g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi.
i. kumdekeza
ii. kuginiza
iii. mdomo kufyata
iv. alofanyiza
v. lau usipomrudi

Answers


Kavungya
a)
i. Kuwa mkali na kumkataza mtoto atendapo maovu
ii. Mtoto kuitika aitwapo la sivyo aadhibiwe
iii. Kuchunguza kila unapolalamikiwa kumhusu
iv. Kumrudi mwanao kila anapotenda kosa

b)
Kutomdekeza mwanaa
Wasikubali kumpendeza mtoto
Wasiwaruhusu watoto kupuuza waitwapo
Kamwe wasiwatetee watoto wao wakati wengine wanalalamika
Wasikose kuwarudi wanao wanapotenda makossa.

c) Mtoto yule : atampuuza mzazi
Atazoea kupewa kile atakacho
Hatatu wala kuitika aitwapo
Atakuwa mzoefu wa kurudia makossa

d) Mchelea mwana kulia hulia yeye
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

e) Mitatu

f) Vina vya kati vinabadilika kila ubeti na vya mwisho vinafanana katika kila ubeti.
Vipande ni viwili kwa kila mshororo-ukwapi na utao
Mizani ni 8,8 jumla ni 16 kila mshororo

g) Kumzoesha kutendewa kila atakalo
Kujibu,kuitika
Kufunga mdomo, kutojibu
Jambo alilotenda
Kama hutamkemea/kama hutamrekebisha
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 08:35

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions