Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...

      

Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali
Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia.
Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia?
Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya
wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang‟anyiro kikubwa
katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza
kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa
kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo
zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge
vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia
alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga
damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu
na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu
kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya „ mkereketwa wa Uafrika akachanganua.
Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi
zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la
ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu
mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi
dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni
kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi
Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia
kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali„ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa
ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti
nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo
hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale
utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba
wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau.

Maswali
a) Binadamu amechanganyika kwa njia ipi?
b) Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa
c) Kwa nini inasemekana kuwa „Demokrasia ni mchezo wa mizengwe?
d) Ni athari gani hutokana na kinyang‟anyiro cha Demokrasia?
e) “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza.
f) Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa.
i) Mafahali
ii) Wanatupikia majungu
iii) Ukarabati

  

Answers


Kavungya
a) Ameshindwa kuielewa dhana ya demokrasia. Dhana hii ina fasiri nyingi kutegemea lengo la
mtu/kundi la watu/mahali wanapoishi

b) i) Pale umma utakapojikomboa kimawazo
ii) Kwa ujasiri kudai huduma bora
iii) Uajibikaji pamoja na kuheshimiwa kwa mkataba wa kijamii

c) i) Kinyang’anyiro cha madaraka
ii) Wasio na madaraka watumia kila mbinu kuyapata
iii) Walio madarakani hawataki kubanduka-hutafuta visababu vya kusalia madarakani

d) i) Maafa
ii) Uharibifu wa mali
iii) Majeraha
iv) Ukimbizi wa raia nje na ndani ya mataifa husika
v) Dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake
vi) Uhasama wa kikabila
vii) Kuzagaa kwa aina mbalimbali ya magonjwa

e) i) Hutumiwa na tabaka la viongozi kujinadi/hasa wakati wa uchaguzi
ii) Wanasiasa hujifanya kuwa wanayajali masilahi ya wanajamiii kumbe huruma zao ni kilio
cha mamba

f) i) Mafalahi-wachochole, maskini, raia, penye ukavu
ii) Wanatupikia majungu-wanatufitini au wanatukosanisha
iii) Ukarabati-Urekebishaji, utengenezaji, kubambanya
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 11:16


Next: Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!
Previous: Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions