Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa
machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa
nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake.
Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka.
Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako,
Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake
halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa
hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao.
Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya
uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta
wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia
maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa
mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu,
kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski.
Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa
kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za
baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa
idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie
shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo
hiyo ibomolewe.
Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo
wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu,
wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza
kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia
za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na
vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani.
Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha
mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii
inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara
hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na
wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya
maeneo Bunge, pia hujadiliwa.
Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa
wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli.
Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa
mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha
mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya
serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika
maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza
kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti
ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi
kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa
wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na
polisi, chifu ndiye suluhisho.
Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni
mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga
sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi
vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko
wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru
kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira
yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi
sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili.

Maswali
a) Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60)
Matayarisho
Jibu
b) Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho.
Matayarisho
Jibu

  

Answers


Kavungya
a) i) Matajiri wengi mijini hawajui juu ya utawala wa chifu hadi watakapokuwa na kesi mbele
ya chifu
ii) chifu ni muhimu na huunganisha jamii
iii) watu wengi huwapuuza
iv) chifu huunda baraza ambazo hujadili maswala muhimu kijijini
v) kazi ya chifu ni ngumu haswa katika kufanya uamuzi muhimu

b) i) Tatizo la chifu ni kutafutia watoto wa barabarani makazi na vituo vya kurekebisha tabia
ii) chifu lazima atunze mazingira ya lokesheni kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa
iii) ahakikishe kuna usawa katika ugawaji wa pesa za maendeleo ya maeneo bunge
iv) kuwasilisha sera na mipango ya serikali kwa wananchi
v) huongeza miradi ya maendeleo katika lokesheni
vi) hutatua ugomvi na kesi za sheria kwa wasioweza kulipa wakili
vii) machifu wengine hawafanyi kazi yao vyema
viii) kutokana na umuhimu wa chifu serikali yafaa kuinua hali yake
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 11:30


Next: Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...
Previous: Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions