Simba anaponguruma/angurumapo wanyama wote hawababaiki.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 11:37
- Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'(Solved)
Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.(Solved)
Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa
machifu.(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa
machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa
nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake.
Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka.
Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako,
Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake
halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa
hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao.
Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya
uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta
wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia
maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa
mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu,
kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski.
Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa
kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za
baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa
idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie
shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo
hiyo ibomolewe.
Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo
wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu,
wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza
kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia
za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na
vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani.
Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha
mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii
inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara
hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na
wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya
maeneo Bunge, pia hujadiliwa.
Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa
wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli.
Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa
mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha
mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya
serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika
maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza
kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti
ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi
kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa
wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na
polisi, chifu ndiye suluhisho.
Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni
mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga
sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi
vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko
wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru
kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira
yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi
sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili.
Maswali
a) Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60)
Matayarisho
Jibu
b) Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho.
Matayarisho
Jibu
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali
Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia.
Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...(Solved)
Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali
Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia.
Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia?
Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya
wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang‟anyiro kikubwa
katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza
kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa
kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo
zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge
vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia
alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga
damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu
na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu
kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya „ mkereketwa wa Uafrika akachanganua.
Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi
zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la
ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu
mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi
dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni
kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi
Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia
kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali„ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa
ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti
nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo
hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale
utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba
wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau.
Maswali
a) Binadamu amechanganyika kwa njia ipi?
b) Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa
c) Kwa nini inasemekana kuwa „Demokrasia ni mchezo wa mizengwe?
d) Ni athari gani hutokana na kinyang‟anyiro cha Demokrasia?
e) “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza.
f) Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa.
i) Mafahali
ii) Wanatupikia majungu
iii) Ukarabati
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo:
Laleni!(Solved)
Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo:
Laleni!
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani?
i. Nyasi
ii. Furaha(Solved)
Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani?
i. Nyasi
ii. Furaha
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano.
-baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)(Solved)
Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano.
-baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo.
i. Ningeenda leo ningefika mapema.
ii. Ningalienda ningalifika mapema.(Solved)
Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo.
i. Ningeenda leo ningefika mapema.
ii. Ningalienda ningalifika mapema.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Andika maana mbili za sentensi ifuatayo.
Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.(Solved)
Andika maana mbili za sentensi ifuatayo.
Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’
Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.(Solved)
Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’
Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Onyesha Nomino na ueleze aina katika sentensi ifuatayo:
Warembo walijifukiza manukato na kuvalia mavazi ya kupendeza.(Solved)
Onyesha Nomino na ueleze aina katika sentensi ifuatayo:
Warembo walijifukiza manukato na kuvalia mavazi ya kupendeza.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Sahihisha sentensi zifuatazo.
i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa.
ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.(Solved)
Sahihisha sentensi zifuatazo.
i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa.
ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Geuza kwa wingi.
i. Njia hii huenda Kisumu
ii. Wembe huu utafaa.(Solved)
Geuza kwa wingi.
i. Njia hii huenda Kisumu
ii. Wembe huu utafaa.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Kanusha sentensi ifuatayo:
Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo:
Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Sahihisha sentensi ifutayo.
Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.(Solved)
Sahihisha sentensi ifutayo.
Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani.
i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa.
ii. Hamisi ni daktari wa meno.(Solved)
Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani.
i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa.
ii. Hamisi ni daktari wa meno.
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Ainisha sentensi hii:
Kilichopikwa(Solved)
Ainisha sentensi hii:
Kilichopikwa
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo:
i. Silabi za irabu pekee
ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu
iii. Silabi za konsonanti pekee(Solved)
Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo:
i. Silabi za irabu pekee
ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu
iii. Silabi za konsonanti pekee
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
Malezi mema
Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza
Atafikia kilele, mzazi atampuza(Solved)
SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
Malezi mema
Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza
Atafikia kilele, mzazi atampuza
Utapiga makelele, wala hatasikiza.
Daima usikubali, kuridhi kumpendeza
Lazima uwe mkali, mengine kumkataza
Na wala usikubali, maneno kuyaigiza.
Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza
Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza
Ama dakika zapita,aje ikimpendeza.
Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza
Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza
Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza.
Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza
Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza
Lau usipomrudi, kosa taliendeleza.
Maswali
a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi.
b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda
c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto
d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili
e) Shairi hili lina mishororo ngapi
f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili
g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi.
i. kumdekeza
ii. kuginiza
iii. mdomo kufyata
iv. alofanyiza
v. lau usipomrudi
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)
- “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko"
i. tambua kipera hiki
ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla(Solved)
“nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko"
i. tambua kipera hiki
ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla
Date posted: November 25, 2022. Answers (1)