Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. Ni zimwi linalotesa na kufisha wazee kwa vijana.

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. Ni zimwi linalotesa na kufisha wazee kwa vijana.
Halichagui jinsia, tabaka, rangi wala umri. Uraibu wa dawa hizi hauna faida yoyote. Wanaotumia dawa
za kulevya huzitia mwili kwa kunusa, kuvuta, kumeza na kujidunga sindano. Zinapoingia katika miili ya
watu madhara huwa mengi.
Kuna wale wanaokosa hamu ya kula, wengine huambukizwa maradhi kama vile ukimwi
wanapotumia sindano zilizotumiwa na watu wenye virusi vya maradhi hayo kujidunga sindano na kutia
dawa mwilini.
Mihadarati pia inaweza kufanya mtu awe mwendawazimu. Vifo pia hutokea ikiwa uraibu utazidi
na mtu akose kupata matibabu. Mtu anayetumia dawa za kulevya huathirika akili. Yeye huwa hana
uamuzi wenye hekima katika maisha yake .wengi wao hushiriki katika vitendo vya uhayawani. Wao
hukosa fikra za utu. Baadhi yao wamebaka kina mama na watoto wadogo na wengine wamezua vita
katika familia na kusababisha madhara makubwa katika jamii zao kwa sababu ya ulevi.
Familia za wanaotumia mihadarati hazina amani. Jamaa zao hutumia hala nyingi kuwalipia ada
ya hospitali ili wapate matibabu baada ya kuzidiwa na uraibu. Mali hufujwa na watu wenye uraibu wa
dawa hizo pale wanapohakikisha hawazikosi kila siku. Mzazi kwa mfano anaweza kutumia hela kununua
dawa za kulevya badala ya kumlipia mwanawe karo. Kuna wale wanaowaibia majirani na marafiki ili
wakidhi mahitaji yao.
Ajali barabarani pia husababishwa na malevi. Dereva yeyote awe wa matatu au gari la kibinafsi
anapoedesha gari akiwa mlevi huwa anahatarisha maisha yake mwenyewe, abiria na wananchi
wanaopiga miguu barabarani .Uchumi wa taifa huzorota baada ya wananchi kutumia mihadarati. Watu
wenye uraibu hukaa mbumbumbu bila kufanya lolote hasa kutokana na kudhoofika kwa afya yao au
ulegevu unaosababishwa na ulevi. Watu wa aina hiyo huwa wanamchango haba katika ukuzi wa
uchumi wa taifa.
Dawa hizi zimesambaa kila mahali utapata zinauzwa masokoni, shuleni, njiani na hata pahali
popote pale penye watu. Dawa za kulevya haziuzwi hadharani nchini Kenya kwa sababu serikali imepiga
marufuku uuzaji wa bidhaa hiyo. Waja wanaoziuza hufanya hivyo kisiri. Walanguzi wa mihadarati
aghalabu hutumia watu wengine kuuza kwa niaba yao. Kuna wale wanaotumia watoto ,
wanaorandaranda almaarufu chokoraa na wengine hutumia vijana katika shule za misingi, upili na vyuo
vikuu kama mawakala.
Vijana hasa wamejipata katika mtego huu kwa kuwafanyia walanguzi biashara hii haramu hili
waweze kupata hela za kukidhi matakwa yao ukweli ni kuwa pesa wanazo patiwa na waajiri wao ni
chache mno na hatimaye wao hutumia daw zile na kuishia kuwa na uraibu unaosababisha wao wenyewe
kuwa wateja wa mabwenyenye hao wasio na utu.
Watu maarufu kama vile wafanyabiashara, wanamuziki na wanasiasa wametuhumiwa kushiriki
katika biashara hii . washukiwa hawa mara nyingi hukosa kufikishwa mahakamani kwa sababu jamii
hukosa ushahidi wa kutosha dhidi ya tabia hiyo. Ni nani hasa muhusika katika kuingiza sumu hii katika
nchi yetu ? hakuna mtu anayeweza kusimama kadamnasi na kusema hiyo ndiyo kazi yake. Mbona
tushiriki katika biashara tusiyoweza kujivunia?
Ni mwito wangu kwa kila mwananchi mzalendo kuungana na wenzake ili kupinga biashara hii haramu.
Tuhubiri makanisani, shuleni misikitini, hekaluni na mahali popote pale. Tukemee adui huyu, wa afya na
mali. Washauri nasaha washike usukani wawashauri wazee kwa vijana, wakubwa kwa wadogo, weusi
kwa weupe tuizike mihadarati katika kaburi la sahau.

Maswali
1. Yape makala haya anwani mwafaka.
2. Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa
letu.
3. Taja namna ambavyo dawa za kulevya zinavyotumiwa.
4. Eleza athari ya dawa za kulevya kwa familia za wanaotumia .
5. Kuna changamoto gani katika kupiga vita matumizi ya mihadararati.
6. Eleza sera ya serikali kuhusu dawa za kulevya.
7. Msamiati ufuatao umetumika kumaanisha nini kwa mjibu wa taarifa.
i. mawakala
ii. kadamnasi
iii. washauri nasaha

  

Answers


Kavungya
1. Dawa za kulevya / mihadarati.

2. zinatesa na kufisha wazee kwa vijana na kuwa zinaathiri bila kuchagua jinsia, tabaka , rangi
wala umri.

3. i) kunusa
ii) kuvuta
iii) kumeza
iv) kujidunga sindano.

4. kukosa amani
Kutumia hela nyingikuwalipia ada ya hospitali.

5. washukiwa mara nyingi hukosa kufikishwa mahakamani kwa sababu jamii hukosa ushahidi wa
kutosha dhidi ya tabia hiyo.

6. serikali imepiga marufuku uuzaji wa mihadarati.

7.
i) mawakala – wnaotimiwa kuuza mihadarati kwa niaba ya wengine.
ii) Kadamnasi – wazi, hadharani, mbele ya watu.
iii) washauri nasaha – wanaelekeleza / kutoa mawaidha kwa waathiriwa wa dawa za kulevya.
Kavungya answered the question on November 26, 2022 at 07:46


Next: Eleza sifa za sajili ya maabadani.
Previous: Andika sifa za sauti zifuatazo: /m/ /gh/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Eleza sifa za sajili ya maabadani.(Solved)

    Eleza sifa za sajili ya maabadani.

    Date posted: November 26, 2022.  Answers (1)

  • Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo. i) -f- ii) -l-(Solved)

    Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo.
    i) -f-
    ii) -l-

    Date posted: November 26, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi hizi. i) Nguo aliyonunua mzazi ni mpya. ii) Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.(Solved)

    Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi hizi.
    i) Nguo aliyonunua mzazi ni mpya.
    ii) Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.

    Date posted: November 26, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi. i) Kiambishi kiwakilishi cha kiima ii) Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo iii) Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa iv) Shina la...(Solved)

    Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi.
    i) Kiambishi kiwakilishi cha kiima
    ii) Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
    iii) Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa
    iv) Shina la kitenzi
    v) Kiambishi cha kauli ya kutendesha
    vi) Kiishio

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tumia neno dhahiri katika setensi kulingana na maagizo Kama: i) Kiambishi ii) Kivumishi(Solved)

    Tumia neno dhahiri katika setensi kulingana na maagizo
    Kama:
    i) Kiambishi
    ii) Kivumishi

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi hii. Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie mjini.(Solved)

    Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi hii.
    Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie mjini.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi __ingine i) dau ii) urembo(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi __ingine
    i) dau
    ii) urembo

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika katika usemi taarifa. “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.(Solved)

    Andika katika usemi taarifa.
    “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa wingi. Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.(Solved)

    Andika katika ukubwa wingi.
    Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi. Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi.
    Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Yakinisha sentensi hii. Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.(Solved)

    Yakinisha sentensi hii.
    Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'(Solved)

    Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.(Solved)

    Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
    Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa
    machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa
    nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake.
    Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka.
    Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako,
    Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake
    halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa
    hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao.
    Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya
    uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta
    wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia
    maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa
    mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu,
    kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski.
    Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa
    kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za
    baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa
    idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie
    shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo
    hiyo ibomolewe.
    Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo
    wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu,
    wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza
    kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia
    za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na
    vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani.
    Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha
    mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii
    inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara
    hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na
    wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya
    maeneo Bunge, pia hujadiliwa.
    Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa
    wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli.
    Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa
    mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha
    mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya
    serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika
    maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza
    kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti
    ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi
    kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa
    wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na
    polisi, chifu ndiye suluhisho.
    Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni
    mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga
    sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi
    vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko
    wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru
    kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira
    yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi
    sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili.

    Maswali
    a) Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60)
    Matayarisho
    Jibu
    b) Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho.
    Matayarisho
    Jibu

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali
    Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia.
    Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia?
    Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya
    wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang‟anyiro kikubwa
    katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza
    kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa
    kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo
    zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge
    vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia
    alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga
    damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu
    na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu
    kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya „ mkereketwa wa Uafrika akachanganua.
    Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi
    zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la
    ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu
    mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi
    dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni
    kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi
    Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia
    kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali„ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa
    ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti
    nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo
    hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale
    utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba
    wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau.

    Maswali
    a) Binadamu amechanganyika kwa njia ipi?
    b) Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa
    c) Kwa nini inasemekana kuwa „Demokrasia ni mchezo wa mizengwe?
    d) Ni athari gani hutokana na kinyang‟anyiro cha Demokrasia?
    e) “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza.
    f) Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa.
    i) Mafahali
    ii) Wanatupikia majungu
    iii) Ukarabati

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!(Solved)

    Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo:
    Laleni!

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? i. Nyasi ii. Furaha(Solved)

    Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani?
    i. Nyasi
    ii. Furaha

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano. -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)(Solved)

    Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano.
    -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. i. Ningeenda leo ningefika mapema. ii. Ningalienda ningalifika mapema.(Solved)

    Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo.
    i. Ningeenda leo ningefika mapema.
    ii. Ningalienda ningalifika mapema.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.(Solved)

    Andika maana mbili za sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)