Nilitazama jua likichwa Matumaini yangu yakizama pamoja Na miale miekundu Nilidhani lilikuwa jinamizi tu Kwamba ulikuwa kesha n’acha

      

Nilitazama jua likichwa
Matumaini yangu yakizama pamoja
Na miale miekundu
Nilidhani lilikuwa jinamizi tu
Kwamba ulikuwa kesha n’acha
Walikuwa wameisha n’ambia
Walimwengu
Ela nilikataa katakata walosema
Nikajitia kuamini waloamba yalikuwa
Uzushi
Hadi siku hii nilopokea waraka,
Waraka ambao ulikuwa jeneza ka kuzikia
Pendo letu la miongo miwili.

a. Taja aina ya wimbo ufuatao.
b. Taja sifa tano za utanzu huu wa fasihi simulizi.
c. Eleza umuhimu wa utanzu huu.
d. Taja na ueleze aina zingine tano za nyimbo.

  

Answers


Kavungya
a. Mbolezi/mbolezo

b.
- Huimbwa wakati wa maafa,kifo au makumbushoa
- Huimbwa kwa sauti ya chini
- Hutofautiana katika jamii moja hadi nyingine
- Huwa na mapigo ya polepole/taratibu
- Huimbwa kwa toni ya huzuni/uchungu
- Haziandamani na ala

c.
- Kufariji waliofiwa
- Kusifu aliyekufa
- Kubembeleza roho za wafu ili kusitoke maafa mengine
- Kuonyesha msimamo wa jamii kuhusu matokeo ya kifo-husababishwa na pepo
- Kukejeli kifo
- Kueleza kutoepukika kwa kifo

d.
- Sifo
- Bembelezi
- Za watoto
- Hodiya
- Wawe
- Dini
- Nyiso
- Za mapenzi
Kavungya answered the question on November 26, 2022 at 08:08


Next: Soma makala haya kisha ujibu maswali. Kwani mnauza salamu? Sina time ya kuwaste hapa. Am a busy person leta order yako haraka... Nimesema samaki wa kupaka. Mimi...
Previous: What are the factors affecting Weather and Climate?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions