Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda

      

Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda

  

Answers


Francis
Mwanamke katika jamii hii amepatiwa nafasi finyu sana, licha ya kuwa na mchango wa kipekee. Kwanza, mwanamke anadhihirika kuwa mpenzi wa dhati ya moyo. Mhubiri anamkumbuka mkewe waliyependana kwa dhati na ambaye anapofariki, anashindwa kabisa kuoa mke mwingine wa kujaza pengo lake. Anashinikizwa na wahubiri wenzake, wazee wa kanisa na hata washirika wake lakini anashindwa kabisa kumwoa mwingine.
Lilia anapomwona Luka mara ya kwanza tu, anampenda kwa dhati hasa kutokana na sauti yake ya kupendeza. Anamshinikiza babake hadi anapompa mamake kazi ya kusafisha kanisa na hata kumpeleka Luka shule. Majaribio ya babake kuwatenganisha hayazai matunda kwani Lilia yuko mstari wa mbele kumpigania Luka wake hadi wanaporuhusiwa kuoana na baba kuwapa baraka zake.
Hata Luka anapoingilia siasa, Lilia anamsaidia licha ya kutopenda siasa. Anamvumilia na ukware wake na kubaki kuwa mwaminifu siku zote.
Anampiga mara kwa mara, lakini anazidi kumshughulikia kama mumewe hadi anampiga na kumsababisha kulazwa hospitalini. Wanakutana huko baada ya Luka kupata ajali ya barabarani na kupoteza uwezo wa kutembea. Hatujui ndoa yao inachukua mkondo gani.
Mamake Luka pia ana mapenzi ya kipekee. Anampenda mwanawe Luka na anajitolea kumlea vyema licha ya umaskini wake. Lilia anapopoteza fahamu baada ya kipigo, anachukua simu na kumpigia. Anafika mara moja na kumhudumia. Anampigia mwanawe na kumlazimisha kutuma ambulensi, kisha kumpeleka Lilia hospitalini na kumuuguza.
Mwanamke pia anachukuliwa kama kiumbe dhaifu cha kuendeshwa na kuelekezwa na mwanamume. Luka anampa mkewe maagizo anayotaka kila mara. Anamkataza kujumuika na marafiki na anapofanya hivyo anampiga vibaya. Anamlazimisha kukaa nyumbani kama mtawa na kumtaka kumpigia simu akitaka kufika ofisini. Anapokosa simu yake akioga, anaingiwa na hofu kuu, kwani anajua yatakayofuatia. Luka anampiga mara kwa mara hadi mwisho anapolazwa hospitalini.
Mwanamke pia anasawiriwa kama chombo cha kumstarehesha mwanamume. Luka anamwambia mkewe kuwa wanawake ni wengi anapokataa kuandamana naye katika kampeni. Kulingana naye, ni rahisi kwake kupata wanawake wengine. Anapokuwa gavana, ana vimada wengi wala hajali hili linavyomwathiri mkewe. Anapomtembelea anampata na mwanamke mwingine. Badala ya kuwa na haya anamfokea na kumlaumu. Mwanamke yule naye pia anaendelea kuhusiana na Luka kimapenzi licha ya kujua ana mke.
Mwanamke pia anachorwa kama msaliti. Kimada wa Luka anajua kuwa ana mke lakini bado anasuhubiana naye na hata kuandamana naye katika shughuli rasmi. Hajali machungu anayomletea mkewe Luka. Isitoshe, anamtoroka Luka anapomhitaji zaidi, pale anapopata ajali na kupoteza uwezo wa kutembea.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 06:13


Next: Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi ya Fadhila za Punda. i. Luka ii. Lilia iii. Babake Lilia
Previous: Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi ya Fadhila za Punda. i. Luka ii. Lilia iii. Babake Lilia(Solved)

    Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi ya Fadhila za Punda.
    i. Luka
    ii. Lilia
    iii. Babake Lilia

    Date posted: January 30, 2023.  Answers (1)

  • Kwa kutaja mifano mitano kutoka kwenye hadithi, Eleza ni kwa nini hadithi hii ikapewa anwani ya “Fadhila za punda’’(Solved)

    Kwa kutaja mifano mitano kutoka kwenye hadithi, Eleza ni kwa nini hadithi hii ikapewa anwani ya “Fadhila za punda’’

    Date posted: January 30, 2023.  Answers (1)

  • Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny? Eleza muktadha wa dondoo hili.....(Solved)

    Chozi la heri
    Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?
    Eleza muktadha wa dondoo hili.
    Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili.
    Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo, inavyojitokeza katika Chozi la Heri.

    Date posted: April 1, 2020.  Answers (1)

  • "...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..." a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze. c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna...(Solved)

    "...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..."

    a. Eleza muktadha wa dondoo hili.

    b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze.

    c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna maudhui uliyotaja hapo juu (2b) yanavyojitokeza katika riwaya.

    d. Eleza sifa nne za msemaji

    Date posted: October 15, 2019.  Answers (1)

  • "Na mwamba ngoma huvuta wapi?" a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo. c. Fafanua sifa za msemewa wa...(Solved)

    "Na mwamba ngoma huvuta wapi?"

    a. Eleza muktadha wa dondoo hili.

    b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo.

    c. Fafanua sifa za msemewa wa maneno.

    d. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo.

    Date posted: October 15, 2019.  Answers (1)

  • Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo, Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo, Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo, Tabia...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

    Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo,
    Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo,
    Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo,
    Tabia njema ni utu.

    Walezi nawaambia, wafunze tabia wana,
    Ili wanapokua, wenye heshima maana,
    Mtu kukosa tabia, ni kama mti bila shina,
    Tabia njema ni utu.

    Hutuzidisha hisia, kufurahisha roho,
    Gumu tuepushia, linalotumiza roho,
    Mtu kukosa twabia, nikiumbe bila roho,
    Tabia njema ni utu.

    Wanafunzi nao pia, shuleni sizushe bala,
    Ili masomo kubia, bila mambo ya kifala,
    Mtu kukosa twabia, dereva toroli bila,
    Tabia njema ni utu.

    Mahabani walioa, sio urembo mwingi,
    Bali hasa ni tabia, utu mapenzi mengi,
    Mtu kukosa tabia, kama nyumba bila msingi,
    Tabia njema ni utu.

    Shuleni vijijinia, amani dumu kujali,
    Sababu kuwa tabia, lizingatiwa aali,
    Mtu kukosa tabia, ni kisu bila makali,
    Tabia njema ni utu.

    Rafiki kukupendea, sio kwa uzuri eti,
    Bali ni hasa tabia, ndani yako wima uti,
    Mtu kukosa tabia, ni kiumbe bila uti,
    Tabia njema ni utu.

    Tamati kuachia, kwamba jambo aali,
    Mengi ningewambia, lakini metoshekali,
    Mtu kukosa tabia, ni kiatu bila soli,
    Tabia njema ni utu.

    Maswali
    1.Pendekeza kichwa mwafaka cha ushairi uliosoma.
    2.Toa bahari tatu tofauti za ushairi huu na uzifafanue.
    3.Fafanua muundo wa shairi hili.
    4. Onyesha jinsi idhini ya mshairi imetumika.
    5. Taja na ueleze mbinu za lugha zilizotumika katika shairi hili.
    6. Andika ubeti wa sita katika lugha ya tutumbi.
    7. Eleza maana ya maneno haya kwa mujibu wa shairi ulilosoma.
    i) Shina.
    ii)Wima.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani(Solved)

    Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa(Solved)

    Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • Ken Walibora na Said A. Mohamed: Damu Nyeusi “Hapa huingii bila kuninyoshea mkono…”(Solved)

    Ken Walibora na Said A. Mohamed: Damu Nyeusi
    “Hapa huingii bila kuninyoshea mkono…”

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza sifa nne za mzungumziwa.
    c) Kwa kurejelea muktadha wa hadithi nzima. Thibisha ukweli wa kauli kuwa mkono mtupu haulambwi

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii(Solved)

    Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea(Solved)

    Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”(Solved)

    “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo.
    c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea tamthilia nzima.

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?(Solved)

    …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?

    a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
    c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji.

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa, Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa, (Solved)

    Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
    Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
    Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
    Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
    Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
    Una macho kutazama, na akili umepewa,
    Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Dunia haishi njama, sijione umepewa,
    Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
    Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
    Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
    Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.


    Maswali
    a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
    b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
    d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
    e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
    f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
    g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
    h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
    i) Uhasama
    ii) Umepowa

    Date posted: October 5, 2019.  Answers (1)

  • Tafautisha kati ya; Ngonjera za ushairi na za maigizo.(Solved)

    Tafautisha kati ya;
    Ngonjera za ushairi na za maigizo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.(Solved)

    Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jana ilikuwepo, ikapita(Solved)

    Soma shairi ifuatalo kish aujibu maswali.
    Jana ilikuwepo, ikapita
    Kwenye giza la sahau
    Jana ilipiga kuathiri
    Athari ijayo leo
    Leo tunajua kesho tunaibashiria
    Kesho ipapo na hatuijui
    Kesho, itapiga au itapuliza?
    Au itapita pasi na chochote
    Kama moshi usio mashiko?
    Kesho hatuioni
    Lakini yaja ...
    Twaihisi
    Twaihisi
    Twaimaizi
    Ipo,

    Yajongea
    Hiyo na taathira zake
    Inakuja
    Yasogea
    Yaja mbio
    Yafikia upeo unaoitwa leo
    Basi kumbuka
    Maisha ni ubishi, yakabili!
    Maisha ni jasiri, jusurisha!
    Maisha ni huzuni, yashinde!
    Maisha ni msiba, uweze!

    Maisha ni wajibu, tekeleza!
    Maisha ni ni fumbo, liague!
    Maisha ni tatizo, litatue!
    Maisha ni ahadi, itemize!
    Maisha mapambano, wana nayo!
    Maisha ni zawadi, ipokee!
    Maisha ni mchezo, uchezee!
    Maisha ni nyimbo, iimbe!
    Maisha ni fursa, itumie?
    Maisha ni ureda, furahia!
    Maisha maumbile, changamkie!
    Maisha ni lengo, lifike!
    Maisha ni mwendo, yaendee!
    Maisha ni uzuri, ustarehee!
    Maisha liwazo, yapumzikie!
    (a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili.
    (b) Fafanua maudhui ya shairi hili.
    (c) Onyesha muundo wa shairi hili.
    (d) Taja na ueleze tamathali tatu za semi alizotumia mwandishi wa shairi hili.
    (e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumia katika shairi.
    Twaimaizi
    Yajongea

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Angaza, mtazame mlimwengu(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Angaza, mtazame mlimwengu
    Bidii, nayo matokeo chungu
    Wezesha, kuishi bila uchungu
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, zitazame barabara
    Aenda, kwa kasi pia salama
    Bidhaa, sokoni upesi fika
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, majokofu majumbani
    Vyakula, na vinywaji hifadhika
    Nafuu, zizima maji ridisha
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, leo pote madukani
    Mikebe, vyakula vinywaji tiwa
    Mimea, huwawirishwa haraka
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, nguo kwa mashine stimu
    Upesi, runinga na simu juza
    Angani, burudika eropleni
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, tarakilishi nguzoye
    Mauzo, mawasiliano kwayo
    tibani, ni mwenzi kwake tabibu
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, mja hajakoma katu
    Shughuli, kila uchao shajara
    Apate, tulia kwa ufanisi
    Teknolojia maendeleo.

    (a) Eleza dhamira ya msanii katika shairi hili.
    (b) Onyesha mifano mitano ya maendeleo katika maisha ya binadamu.
    (c) Eleza umbo la shairi hii.
    (d) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari.
    (e) Eleza kwa kifupi mtazamo wa mshairi kuhusu teknolojia.
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo;
    (i) Majokofu
    (ii) Hunawirisha
    (iii) Shajara

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja mfano mmoja wa tamathali ya usemi kwenye dondoo.
    (c) Dhihirisha jinsi utu ulivyotoka pahali pake, ukirejelea riwaya nzima.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)