1. Utabaka
Jamii ya jimbo la Matopeni imegawanywa katika makundi mawili makuu kwa kutegemea hali ya kiuchumi. Kuna wenye hadhi na kina yakhe kwa kutegemea hadhi yao katika jamii. Wananchi ambao ndio wapiga kura na watozwa ushuru wako katika kundi la chini linalohangaikia maisha kila uchao.
Maisha kati ya makundi haya mawili tunaambiwa kuwa yametengana kama mbingu na ardhi. Baada ya ahadi za uongo, viongozi wanatwaa nyadhifa zao na kujiendea kuishi kwa fahari.
Zuhura na Machoka wanalazimika kurejelea uhusiano wao mzuri baada ya uchaguzi. Tunaambiwa kuwa dhiki ndiyo inayorejesha uhusiano wao ambao unavurugwa awali na misimamo yao inayokinzana kuhusiana na viongozi wanaopendelea. Wanagundua kuwa wako katika kundi moja kijamii, kundi la wasakatonge wala viongozi wanaopigania hata hawayajali maslahi yao.
Utabaka pia unadhihirika katika safu ya uongozi. Inavyooonekana, ni kana kwamba kuna wale waliozaliwa kuongoza huku wengine wakiwa wafuasi. Katika jimbo la Matopeni, Sugu Junior na Fumo Matata ndio wanaozozania nafasi ya kuongoza. Nafasi hizi wanaridhi kutoka kwa wazazi wao. Sugu Senior, babake Sugu Junior ndiye alikuwa kiongozi wa matopeni baada ya walowezi kuondoka, hali Zuzu Matata, babake Fumo Matata akiwa mpinzani wake. Yashangaza kuwa ni familia hizo mbili tu zinazozozania uongozi hadi sasa.
Hali ya utabaka pia inaonekana katika mkutano wa kumwapisha Sugu Junior. Kiwanja kimegawanywa mara mbili. Kuna upande uliotengewa wenye ulwa katika jamii kama mawaziri, viongozi wa serikali na viongozi wa majimbo jirani. Upande huu umewekwa hema la kuwazuia jua, kuna vinywaji na walinzi pia. Upande wa pili ni ule wa raia wa kawaida. Huko, jua linawateketeza inavyofaa. Isitoshe, wanalazimika kufika mapema kusubiri kiongozi wao, ambaye anafaa kuwasili mwisho wa wote. Anapofika, yuko na walinzi wanaoimarisha usalama wake, tena anafika saa sita.
2. Usaliti
Jimbo la Matopeni linadhihirisha usaliti wa viongozi waliochaguliwa kwa matumaini ya kuboresha maisha ya wananchi. Wakati wa kupiga kampeni, wanatoa ahadi si haba ambazo wanaahidi kutimiza pindi tu wakiingia mamlakani. Wanaaahidi kuimarisha sekta ya afya, kutengeneza barabara, kuimarisha ukulima, elimu na kuwapa kina mama mikopo ya kuanzisha biashara pamoja na ajira kwa vijana. Hata hivyo, wanasahau ahadi hizi zote wanapoingia mamlakani na kuwatelekeza wananchi waliowachagua.
Zuhura na Machoka wanasaliti demokrasia, jimbo lao na kujisaliti wenyewe wanapochagua viongozi wasiofaa. Zuhura anamwambia Machoka kuwa wanafaa kumchagua mtu wao, awe anafaa au la.
Wanazozana kutokana na misimamo yao inayotofautiana kuhusiana na viongozi wanaotaka. Ajabu ni kuwa viongozi hao hawawafaidi kwa lolote. Zuhura anakiri kwamba walikosea kwa kuwachagua viongozi kwa misingi ya kikabila na pia kwa kuwaziba macho kwa vijizawadi vidogovidogo. Hatimaye wanabaki katika dhiki na kurejesha ujirani wao.
Wahesabu kura pia wanasaliti demokrasia na wapiga kura kwa kuwalimbikiza viongozi wasiotaka. Tunaambiwa kuwa pale Matopeni kupiga kura na kutopiga ni mamoja kwani uamuzi wa mwananchi hauheshimiwi. Tunaambiwa kuwa zoezi la kuhesabu kura ndilo muhimu, na kuwa hata wafu hutoka maziarani wakapiga kura na kurejea huko huko. Ina maana kuwa uamuzi wa wananchi unapuuziliwa mbali na kupatiwa viongozi wasiowafaa.
Viongozi wa majimbo jirani wanamsaliti Sugu Junior kwa kususia sherehe yake ya kuapishwa, licha yake kugharamia nauli zao za ndege. Sugu anawasili saa sita, kwani ndiye anatarajiwa kufika wa mwisho kulingana na itifaki. Anashangaa kuwa ukumbi wa viongozi ukona watu wachache tu, licha ya kuwa amewalipia nauli ya ndege. Nauli ambayo anawalipia kufuta shauku yao kuwa alipata uongozi kupitia mlango wa nyuma. Nauli ya pesa za wananchi, wapiga kura, watozwa ushuru.
3. Ukabila na Unasaba
Wakati wa kampeni, Zuhura anamwambia Machoka kuwa wanastahili kumchagua mtu wao, awe mzuri au mbaya, awe amesoma au la. Hoja yake ni kuwa wanastahili kuchagua mtu kwa kuwa anatoka kabila lao tu. Mfumo uu unawaletea matatizo mengi kwani huyo mtu wao hajali maslahi yao hata kidogo.
Anatarajia kuwa serikali ya mtu wao itawafaa lakini wapi, wanabakia katika lindi la umaskini bado.
Zuhura anakiri makosa yake ya kumchagua kiongozi kwa kuwa ni wa kabila lao. Bado matatizo yanawazidi. Mahitaji yanazidi kuwakaba huku mapato yao yakimegwa na ushuru unaopanda kila uchao.
Katika mahojiano na Radio Salama iliyopo Matopeni, kiongozi wa upinzani Fumo Matata anawakanya wanannchi dhidi ya mfumo wa kupiga kura kwa kuegemea kwenye misingi ya kijinsia. Anawaeleza kuwa mfumo huo umepitwa na wakati na bado wataendelea kutaabika chini ya uongozi wa mtu huyo licha ya kuwa wa jamii yao.
Fumo anawaona kama miti ambayo inakubali kuangamizwa na shoka huku ikidhani na mwenzao kwa kuwa mpini wake umetokana nao. Wananchi wanapuuzilia mbali usemi wake na kuendeleza mtindo huo wa uchaguzi, hali ambayo inawaletea matatizo mengi. Wanazidi kutaabika.
Ni wazi kwamba suala la ukabila lilianza pindi tu baada ya kuondoka kwa walowezi wala si jambo geni. Tunaambiwa kuwa baada ya walowezi kuondoka, Zuzu Matata anaazimia kuchukua uongozi na kupendekezwa na walowezi. Hata hivyo, anasisitiza kwamba Mzee Sugu Junior aachiliwa kutoka jela alikofungwa. Anapoachiliwa, anapata umaarufu kumliko. Tunaambiwa kuwa Sugu alitwaa uongozi kwa shuruti za wazee wa kabila lake.
Hali ya unasaba pia inadhihirika katika uongozi wa jimbo la Matopeni. Mzee Sugu Senior anatwaa uongozi huku Zuzu Matata akiwa mpinzani wake. Baada yao kufariki, wanao wanachukua nafasi zao katika taifa. Sugu Junior, mwanawe Sugu Senior, anatwaa uongozi huku Fumo Matata, mwanawe Zuzu Matata akiwa mpinzani wake wa karibu.
Inastaajabisha kuwa ni familia mbili tu ambazo zinazozania uongozi wa Matopeni, ni kana kwamba ndizo zilizaliwa kuongoza na hakuna familia nyingine inayoweza kuchukua uongozi huo.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 06:47
- Mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda ameagazia vipi suala la migogoro katika jamii.(Solved)
Mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda ameagazia vipi suala la migogoro katika jamii.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda(Solved)
Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda(Solved)
Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi ya Fadhila za Punda.
i. Luka
ii. Lilia
iii. Babake Lilia(Solved)
Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi ya Fadhila za Punda.
i. Luka
ii. Lilia
iii. Babake Lilia
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Kwa kutaja mifano mitano kutoka kwenye hadithi, Eleza ni kwa nini hadithi hii ikapewa anwani ya “Fadhila za punda’’(Solved)
Kwa kutaja mifano mitano kutoka kwenye hadithi, Eleza ni kwa nini hadithi hii ikapewa anwani ya “Fadhila za punda’’
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny? Eleza muktadha wa dondoo hili.....(Solved)
Chozi la heri
Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?
Eleza muktadha wa dondoo hili.
Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili.
Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo, inavyojitokeza katika Chozi la Heri.
Date posted: April 1, 2020. Answers (1)
- "...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..."
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze.
c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna...(Solved)
"...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..."
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze.
c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna maudhui uliyotaja hapo juu (2b) yanavyojitokeza katika riwaya.
d. Eleza sifa nne za msemaji
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- "Na mwamba ngoma huvuta wapi?"
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo.
c. Fafanua sifa za msemewa wa...(Solved)
"Na mwamba ngoma huvuta wapi?"
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo.
c. Fafanua sifa za msemewa wa maneno.
d. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo, Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo, Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo, Tabia...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo,
Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo,
Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo,
Tabia njema ni utu.
Walezi nawaambia, wafunze tabia wana,
Ili wanapokua, wenye heshima maana,
Mtu kukosa tabia, ni kama mti bila shina,
Tabia njema ni utu.
Hutuzidisha hisia, kufurahisha roho,
Gumu tuepushia, linalotumiza roho,
Mtu kukosa twabia, nikiumbe bila roho,
Tabia njema ni utu.
Wanafunzi nao pia, shuleni sizushe bala,
Ili masomo kubia, bila mambo ya kifala,
Mtu kukosa twabia, dereva toroli bila,
Tabia njema ni utu.
Mahabani walioa, sio urembo mwingi,
Bali hasa ni tabia, utu mapenzi mengi,
Mtu kukosa tabia, kama nyumba bila msingi,
Tabia njema ni utu.
Shuleni vijijinia, amani dumu kujali,
Sababu kuwa tabia, lizingatiwa aali,
Mtu kukosa tabia, ni kisu bila makali,
Tabia njema ni utu.
Rafiki kukupendea, sio kwa uzuri eti,
Bali ni hasa tabia, ndani yako wima uti,
Mtu kukosa tabia, ni kiumbe bila uti,
Tabia njema ni utu.
Tamati kuachia, kwamba jambo aali,
Mengi ningewambia, lakini metoshekali,
Mtu kukosa tabia, ni kiatu bila soli,
Tabia njema ni utu.
Maswali
1.Pendekeza kichwa mwafaka cha ushairi uliosoma.
2.Toa bahari tatu tofauti za ushairi huu na uzifafanue.
3.Fafanua muundo wa shairi hili.
4. Onyesha jinsi idhini ya mshairi imetumika.
5. Taja na ueleze mbinu za lugha zilizotumika katika shairi hili.
6. Andika ubeti wa sita katika lugha ya tutumbi.
7. Eleza maana ya maneno haya kwa mujibu wa shairi ulilosoma.
i) Shina.
ii)Wima.
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani(Solved)
Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa(Solved)
Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Ken Walibora na Said A. Mohamed: Damu Nyeusi
“Hapa huingii bila kuninyoshea mkono…”(Solved)
Ken Walibora na Said A. Mohamed: Damu Nyeusi
“Hapa huingii bila kuninyoshea mkono…”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza sifa nne za mzungumziwa.
c) Kwa kurejelea muktadha wa hadithi nzima. Thibisha ukweli wa kauli kuwa mkono mtupu haulambwi
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii(Solved)
Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea(Solved)
Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”(Solved)
“Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo.
c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea tamthilia nzima.
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?(Solved)
…unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji.
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
(Solved)
Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Dunia haishi njama, sijione umepewa,
Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
i) Uhasama
ii) Umepowa
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Tafautisha kati ya;
Ngonjera za ushairi na za maigizo.(Solved)
Tafautisha kati ya;
Ngonjera za ushairi na za maigizo.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.(Solved)
Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Jana ilikuwepo, ikapita(Solved)
Soma shairi ifuatalo kish aujibu maswali.
Jana ilikuwepo, ikapita
Kwenye giza la sahau
Jana ilipiga kuathiri
Athari ijayo leo
Leo tunajua kesho tunaibashiria
Kesho ipapo na hatuijui
Kesho, itapiga au itapuliza?
Au itapita pasi na chochote
Kama moshi usio mashiko?
Kesho hatuioni
Lakini yaja ...
Twaihisi
Twaihisi
Twaimaizi
Ipo,
Yajongea
Hiyo na taathira zake
Inakuja
Yasogea
Yaja mbio
Yafikia upeo unaoitwa leo
Basi kumbuka
Maisha ni ubishi, yakabili!
Maisha ni jasiri, jusurisha!
Maisha ni huzuni, yashinde!
Maisha ni msiba, uweze!
Maisha ni wajibu, tekeleza!
Maisha ni ni fumbo, liague!
Maisha ni tatizo, litatue!
Maisha ni ahadi, itemize!
Maisha mapambano, wana nayo!
Maisha ni zawadi, ipokee!
Maisha ni mchezo, uchezee!
Maisha ni nyimbo, iimbe!
Maisha ni fursa, itumie?
Maisha ni ureda, furahia!
Maisha maumbile, changamkie!
Maisha ni lengo, lifike!
Maisha ni mwendo, yaendee!
Maisha ni uzuri, ustarehee!
Maisha liwazo, yapumzikie!
(a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili.
(b) Fafanua maudhui ya shairi hili.
(c) Onyesha muundo wa shairi hili.
(d) Taja na ueleze tamathali tatu za semi alizotumia mwandishi wa shairi hili.
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumia katika shairi.
Twaimaizi
Yajongea
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)