Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia.

      

Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia.

  

Answers


Francis
1. Hadithi ndani ya Hadithi
Tunasimuliwa kisa cha msitu na shoka. Miti katika msitu iliangamizwa na makali ya shoka huku ikifurahia eti kwa kuwa mpini wa shoka ulitokana na mmoja wao. Ilidhani shoka ni mwenzao. Kisa hiki kinafananishwa na Wanamatopeni wanaomchagua kiongozi kwa misingi ya kikabila ila anawadhulumu wakidhani ni mmoja wao

2. Tashbihi
Maisha kati ya makundi haya mawili, yaani mpiga kura na mpigiwa kura, yametengana kama mbingu na ardhi.
Anasimama pale kama kigingi Zuhura na Machoka walikuwa kama fahali wawili-hawakai katika zizi moja.
Maisha ya Wanamatopeni yalikuwa kama mchezo wa karata, hawajui leo wala kesho. Wanamatopeni walipotathmini hali zao, walijifananisha na panya walionaswa kwenye mtego wa uhitaji. Fumo aliona hali ya Matopeni kama kisa cha msitu na shoka.
Wakishapata walichokitaka, walijitenga na umma kama wagonjwa wa ukoma.

3. Majazi
Machoka- mhusika huyu amechoshwa na maisha ya umaskini. Ametoka kutafuta kibarua mchana kutwa huku amechoka. Yuko tayari kutua mzigo aliotwishwa, ambao umemchosha.
Zuhura- ni sayari ya pili kutoka kwenye jua. Anajiona kuwa karibu na jua(uongozi), eti kwa sababu kiongozi anatoka kabila lake. Yuko kwenye mstari wa mbele kupiga kura na pia katika sherehe za kuapishwa kwa Sugu Junior.
Chuku- taswira ya chumba chake ingeweza kumliza kipofu. Hata hina aliyokuwa amejiremba Zuhura mikononi na wanja aliokuwa amejipaka imekwishaanza kudondoka kwa makali ya jua.

4. Kejeli
Mzigo wa maisha haukuwatisha wala kuwakosesha usingizi viongozi wao Ndoto anayozidi kuiota akiwa mle kaburini!
Pale Matopeni, siku hizi hata wafu hupiga kura na kurejea maziarani!
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 06:54


Next: Jadili maudhui yoyote matatu yanayojitokeza katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia
Previous: Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia i. Sugu Junior ii. Machoka iii. Zuhura

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions