Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia i. Sugu Junior ii. Machoka iii. Zuhura

      

Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia
i. Sugu Junior
ii. Machoka
iii. Zuhura

  

Answers


Francis
1. Sugu Junior
- Ni fisadi. Anawaacha wananchi waliompa wadhifa kutaabika wala hajali maslahi yao. Anatwaa uongozi kwa njia za kifisadi kwani siye chaguo la wananchi
- Ni mbadhirifu. Anatumia visivyo hela za jimbo la Matopeni. Anawalipia nauli viongozi wa majimbo jirani kuja katika sherehe za kuapishwa kwake, sherehe ambazo hata hawaji.
- Ni mwenye tamaa. Ana tamaa ya uongozi. Anatumia kila njia kuhakikisha kuwa ametwaa uongozi japo siye chaguo la wananchi.
- Ni mnafiki. Wakati wa kampeni, anajinasibisha na watu na hata kuwa karibu nao ili kupata kura zao. Anapopata mamlaka, anajitenga nao kama mbingu na ardhi.

Umuhimu wa Sugu
Ni kiwakilishi cha viongozi wasiojali maslahi ya umma uliowachagua. Kupitia kwake, hali ya mvutano katika uongozi inadhihirika na jinsi hali hiyo inavyoathiri maendeleo Ni kiwakilishi cha unafiki wa viongozi wengi katika jamii
Ni kiwakilishi cha ukoloni mamboleo katika jamii ya sasa.


2. Machoka
- Ni mwenye bidii. Anarauka asubuhi na mapema kwenda kusaka kibarua ili kukidhi mahitaji yake. Hakati tamaa hadi jioni anapokosa kabisa.
- Ni mkakamavu. Anaposhikilia lake, habanduki. Ana msimamo wake katika uchaguzi wala kauli ya Zuhura haibadilishi msimamo wake. Anahiari kukosana naye badala ya kufuata ushawishi wake.
- Ni mzalendo. Siku ya kupiga kura, anaungana na Wanamatopeni wengine kwenda kupiga kura kwa nia ya kumteua kiongozi wao.
- Ni mwenye kumbumkumbu. Anapokinai hali yake, anakumbuka shairi alilowahi kusoma kuhusiana na msiba wa kujitakia lililoandikwa na mshairi mwenye lakabu ya Malenga Mteule.

Umuhimu wa Machoka
Ni kiwakilishi cha mateso wanayopitia raia chini ya utawala mbaya
Ni kielelezo cha bidii na kujituma katika shughuli licha ya matatizo ya maisha. Anadhihirisha mgawanyiko uliopokatika jamii kwa misingi ya kiuchumi na mamlaka.


3. Zuhura
- Ni mzalendo. Siku ya kupiga kura, anrauka bukrata na wenzake kwenda kupanga foleni na kusubiri hadi zamu yao kupiga kura ili kumteua kiongozi wao.
- Ni mshawishi. Anamsisitizia Machoka kuwa wanafaa kumchagua kiongozi kutoka kabila lao. Anapokataa wanazozana.
- Ni mkabila. Ananuia kuteua kiongozi kutoka kabila lake. Hajali iwapo kiongozi huyo ni mzuri au mbaya, amesoma au la.
- Ni mvumilivu. Ni mmoja wa wale wanaosubiri ujio wa Sugu Junior katika sherehe za kuapishwa kwake. Anaunguzwa na jua na kusubiri, hata hina mikononi na wanja machoni unaanza kuyeyuka lakini anangoja hadi kiongozi anapofika.
- Ni mkakamavu. Anapofanya uamuzi hatetereki. Anakata kauli kumteua kiongozi kutoka katika kabila lake. Anangoja hadi kiongozi anapofika katika sherehe za kuapishwa kwa Sugu Junior.

Umuhimu wa Zuhura.
Anadhihirisha jinsi raia wanavyochangia katika matatizo yanayowakumba kwa kuwachagua wasiofaa. Ni kiwakilishi cha ukabila na mchano wake katika kuiangusha jamii.
Kupitia kwake, mgawanyiko wa kijamii kwa misingi ya kiuchumi unadhihirika. Ni kiwakilishi cha matatizo wanayopitia raia wa kawaida katika nchi.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:00


Next: Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia.
Previous: Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions