Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.

      

Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.

  

Answers


Francis
Mapambazuko ni wakati wa asubuhi inapoingia na jua kuchomoza. Machweo nao ni wakati wa jua kutua na giza kuingia. Mada hii inaweza kufasiriwa kuwili; mapambazuko yanayotokea wakati wa machweo, au mapumbazuko yaliyo katika machweo.
Dhana hizi, mapambazuko na machweo pia zimetumiwa kwa maana nyingine. Mapambazuko yanawakilisha wakati wa ujana, huku machweo yakiwakilisha uzee. Pia, mapambazuko yanaashiria mwangaza(fanaka) huku machweo yakiashiria giza(taabu/mashaka).
Makutwa anawashangaza wengi kwa kuwa anashinda na vijana kila wakati licha ya kuwa ni mzee. Hashirikiani na wazee wenzake hata kidogo. Anaonekana kama ujana wake umeingia akiwa mzee, yaani mapambazuko yake yanamjia akiwa katika machweo.
Mzee Makucha anafanya biashara ya kuuza vitafunio. Japo Mzee Makutwa anamkejeli, yeye anaiona kuwa ndio tumaini lake baada ya kufutwa kazi kwenye shirika la reli. Machweo yanaingia kwa kuachishwa kazi, na anaiona biashara hii kuwa mapambazuko yake. Binti yake Makucha, Riziki, anaolewa na kigogo Mhindi baada ya kushindwa kuvumilia dhiki. Kutokana na machweo ya umaskini, anaonelea ndoa hiyo kama mapambazuko kwake.
Mzee Makucha anamweleza Mzee Makutwa kuwa siku moja, jua la macheo(Mapambazuko) litambishia mlango japo anaelekea machweo. Yaani, ipo siku atafanikiwa licha ya uzee wake.
Sai na Dai wanaeleza taabu ya maisha yao. Ni miongoni mwa vijana waliohitimu kutoka chuo kikuu na kukosa kazi. Wanazurura tu mitaani. Wako karibu kukata tamaa. Machweo yameanza kuwaingilia katika maisha hali bado wako wakati wa mapambazuko. Wanaona shughuli za probox ya Makutwa kama nafuu ya pekee, yaani mapambazuko ya kuwatoa katika machweo waliyomo.
Mzee Makucha anapofuata gari la Makutwa kwa teksi, linawaongoza hadi kwenye mgodi mkubwa, ambapo vijana na watoto wadogo wanafanya kazi ya kusaka vito vya thamani. Wanapata taabu nyingi, na wengi wao wanakosa hata fursa ya masomo. Machweo yameshaingia katika maisha yao hali wako katika mapambazuko.
Mzee Makutwa amewatesa vijana wengi kwa kuwaingiza katika machweo ya kumfanyia kazi ya kinyama ya kusaka vito. Hawana imani ya maisha bora. Kukamatwa kwake na polisi ni mapambazuko ya machweo, kwani uovu wake unafikia kikomo.
Mzee Makucha anapata zawadi ya hundi kutoka kwa tajiri mmoja anayeendeleza miradi ya kuwainua vijana kimaendeleo. Amekuwa akiishi kwa taabu kwa kuuza vitafunio kando ya barabara. Haya ni mapambazuko(mafanikio) ambayo yanamwangukia katika machweo ya maisha yake(uzee na taabu).
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:03


Next: Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia i. Sugu Junior ii. Machoka iii. Zuhura
Previous: Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions