Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.

      

Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.

  

Answers


Francis
1. maskini
Mzee Makucha anaanguka kwenye lindi la umaskini baada ya kuachishwa kazi katika shirika la reli bila marupurupu, kwani shirika hilo linasambaratika pia. Analazimika kuchuuza vitafunio kando ya barabara kujipatia riziki. Mkewe naye anauza kaimati na vitumbua kwenye veranda ya nyumba yao.
Umaskini unawazidi kiasi kwamba binti yao wa pekee, Riziki, anawatoroka na kuolewa na Mhindi ili kuepuka urumo. Hata hivyo, umaskini huo unaondoka baada ya kitendo cha kishujaa cha Makucha kinachowaletea hundi ya pesa kutoka kwa tajiri mmoja anayethamini tendo lake.
Vijana maskini wanajipata taabani mikononi mwa Mzee Makutwa. Anawasomba kwenda kuwafanyisha kazi ya kusaka vito vya thamani
katika mgodi wake. Wanafanya kazi hii katika mazingira mabovu na kufungiwa mle ndani, wasiwe na nafasi ya kutokea.

2. Ukoloni Mamboleo
Ukoloni huu unaendelezwa na Mzee Makutwa baada ya kustaafu uwaziri. Makutwa anaonekana akizurura huku na huko na gari lake huku akiwabeba vijana kutoka mitaani wala hakuna anayejua shughuli ambazo anaendeleza wala anakoelekea, hadi Makucha anapofuata gari lake kwa teksi likiendeshwa na kijana mwingine. Anafika kwenye mgodi wa Makutwa wanakofanya kazi vijana hawa.
Wanateremka bonde ambalo limejificha kabisa, hata miale ya jua haionekani. Wanaingi a kwenye tambarare kubwa lenye vuduta vya mchanga ambapo vijana kadhaa, ikiwemo watoto wadogo wanafanya kazi. Wanadondoa vijiwe vidogovidogo vinavyong’aa. Wanasimamiwa na wanyapara wanaowaamrisha kwa sauti za kutisha. Makucha anapoingia ndani ya pango, anapata taa za vibatari za kuzuia giza lililomo. Vijana wanachimba madongo ya mchanga na kuyatia ndani ya mikokoteni. Wamelowa jasho kutokana na upungufu wa hewa ndani ya mgodi huo.

3. Kazi
Mjini Kazakamba, kila mmoja anajikaza vilivyo kujitafutia riziki kupitia kazi hii au nyingine. Mzee Makucha kila asubuhi anarauka kuuza bidhaa zake kwenye makutano ya njia akiwa na uhakika wa kunasa wateja wengi iwezekanavyo. Dhihaka za Mzee Makutwa hazibadilishi mtindo wake wa kujitafutia riziki. Mkewe naye anachuuza kaimati na vitumbua kwenye veranda ya nyumba yao.
Kabla ya kuanza kuchuuza vitafunio hivi, Mzee Makucha anafanya kazi na shirika la reli ambalo linamtimua kwa ajili ya kupunguza idadi ya wafanyakazi wake. Baadaye linasambaratika, hivyo anakosa marupurupu yake.
Makutwa naye anafanya kazi kama waziri hadi anapostaafu. Kazi hii inampa majivuno na anapostaafu, anadharau kazi ya Makucha ya kuuza vitafunio. Anajigamba na kazi yake anayofanya ambayo haieleweki, kwani anaonekana kila siku akiwabeba vijana huku na huko, wala hakuna ajuaye wanaenda wapi.
Baadaye tunafahamu kuwa ni kazi haramu ya kuwatumikisha kwenye mgodi.
Sai na Dai wanawakilisha vijana wengi wanaopata elimu hadi vyuo vikuu lakini wanakosa kazi. Vijana hawa wanaishia kuwa wakizurura mitaani na hatimaye kupata kazi za kidhuluma kama ile ya Mzee Makutwa ya mgodi.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:16


Next: Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.
Previous: Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo. i. majazi ii. kinaya iii. jazanda

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions