Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo. i. majazi ii. kinaya iii. jazanda

      

Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo.
i. majazi
ii. kinaya
iii. jazanda

  

Answers


Francis
i. Majazi;
Makutwa. Ina maana mbili, mchana mzima(kutwa) au kupatikana. Mzee Makutwa anazurura na gari lake mchana kutwa kwa shughuli ambazo hazieleweki. Pia, anakutwa katika uhalifu wake na kutiwa ndani.
Makucha. Ina maana mbili pia, usiku mzima au kupambazuka(kucha), na pia kucha kubwa. Kila kuchapo, yuko mbioni kunogesha biashara yake. Pia ana ‘Makucha’, yaani uwezo mkubwa wa kupata atakacho. Makucha yake yanadhihirika kupitia bidii zake. Anatafuta haki anapofutwa kazi na pia kumnasa Makutwa.
Macheo. Ina maana ya wakati wa jua kuchomoza, ishara ya matumaini. Ni ‘macheo’ katika maisha ya mumewe. Anamsaidia kuzumbua riziki na kumshauri panapohitajika.
Riziki. Ni bintiye Makucha anayetoroka kuolewa na Mhindi. Neon hili lina maana ya uwezo wa kujikimu au baraka kutoka kwa Mungu. Anaamua kusaka riziki yake kupitia kuolewa na Mhindi na pia anapata baraka za mume.
Kazakamba. Mji wanakoishi kina Makucha. Kila mtu huku amekaza kamba, yaani kujitolea, ili kuboresha maisha. Kuna wanaochuuza bidhaa na wanaofanya uhuni.
Sai na Dai. Sai ina maana ya kuudhi au kuwa mshindani. Dai nalo lina maana ya kutoa maoni au kupendekeza jambo. Sai anajibu maswali ya Dai kwa ushindani huku naye Dai akimtolea pendekezo la kupanda kwenye gari la Makutwa.

ii. Kinaya;
Mzee Makutwa anasemekana kuwa anashinda tu kujumuika na vijana, hata wazee wenzake hana muda wa kubarizi au kuongea nao.
Makutwa anaposimamisha gari kwenye biashara ya Makucha, anamwambia kuwa hakukusudia kumwudhi. Tendo la kutapakaza vumbi kwenye bidhaa zake na kejeli kuhusu bintiye ni wazi kwamba ananuia kumwudhi.
Makutwa anamwambia kuwa atawarejesha vijana wale katika kazi hiyo katika uwepo wa askari. Tayari ana makosa na anaongezea mengine. Makutwa anamwambia Makucha kuwa alidhani ni rafiki wa dhati. Ni kinaya kwa kuwa Makutwa mwenyewe si rafiki wa dhati hata kidogo. Hakumsaidia akiwa waziri na kila mara humkejeli.

iii. Jazanda
Shirika la reli alilohudumia tangu macheo ya maisha yake. Tayari alikuwa katika magharibi ya maisha yake Huu sio wakati wa kujenga kichunguu bali wa kustarehe ndani ya kichunguu. Heri wewe unayestaladhi katika machweo ambayo sasa ni mapambazuko kwako.
Ukiumwa na nyuki, hauna haja ya kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali. Hujui faida ya nyuki ulimwenguni? Uliamua kurina asali ya nchi.
Magharibi ikamkuta akigaragara kwenye sakafu baridi huku akisubiri kufunguliwa mashtaka. Mkono wa sheria nao ukamsukuma kuyakabili machweo ya maisha yake kifungoni.
Ingawa nimefikia magharibi ya maisha yangu, sudi hii imenipa tumaini la mapambazuko mapya maishani. Nahisi kwamba jua la asubuhi limeniangazia miale ya matumaini mapya, hata kama machweo yako karibu!
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:20


Next: Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.
Previous: Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions