Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.

      

Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.

  

Answers


Francis
Nafasi ya Vijana Katika Jamii.
Vijana wamepatiwa nafasi changamano katika hadithi hii. Makucha anawachukulia vijana kuwa watumwa. Anawabeba na kuwapeleka katika mgodi wake kumfanyia kazi ya kutafuta vito vya thamani. Vijana hawa wanakosa nafasi ya kujiendeleza kielimu na kuyafurahia maisha yao pamoja na kutumikia jamii. Isitoshe, wanakumbwa na hali ngumu ya kimaisha, kwani huko wanakoishi hakuna hali nzuri. Hewa si safi na kazi wafanyazo ni za sulubu.
Sai na Dai pia wanawakilisha hali ya vijana wengi katika jamii. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, hawajapata kazi wala hawana matuamini. Wanashinda kuzurura mitaani. Dhiki inapowafika shingoni, wanaamua kujaribu bahati kwa Makutwa, bila kujua wanaelekea kujiuza kwa utumwa. Hata hivyo, Makucha anawaopoa kabla hawajazama huko.
Makucha anaamini kuwa vijana ndio raslimali kuu ya jamii. Baada ya kuwaokoa vijana wale kutoka mikononi mwa Makutwa, anawaonea imani. Anafahamu kuwa wengi wao wanafaa kuwa katika shule wakiandama elimu na hata wengine katika vyuo vikuu. Isitoshe, anapokea zawadi ya hundi ya pesa kutoka kwa tajiri mmoja ambaye anaendeleza miradi ya kimaendeleo kwa vijana. Bila shaka, anaelewa fika kuwa vijana wana jukumu kubwa katika jamii.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:22


Next: Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo. i. majazi ii. kinaya iii. jazanda
Previous: Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions