Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’

      

Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’

  

Answers


Francis
Ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’.
Harubu ina maana ya taabu anayopata mtu. Maisha yamejaa harubu katika hadithi hii. Simu ya Mama Mercy ndiyo inamtoa Kikwai ofisini, huku akilalamika kuwa mtoto atalala. Ni wazi kwamba mambo si mazuri upande huo. Anapofika, anapata kuwa Mama Mercy hajapika kwa kuwa hataki kukopa. Mercy anamshtakia njaa mfululizo.
Mama Mercy anamzidishia Kikwai harubu kwa malalamishi yake kila mara. Analalamika kuwa Kikwai anamtelekeza na kuwa hawajibikii wajibu wake. Anasema kuwa yeye alikuja likizo hali mambo yako hivyo, hawapati muda wa kuwa pamoja. Hata anamtaka mumewe aandamane na Mercy kazini.
Kikwai analazimika kulala njaa kwa kuwa mkewe hajala. Haoni haja ya kula mkewe akiwa humo humo hali yeye hali. Isitoshe, chakula chenyewe kina ladha ya mafutataa. Wanaendelea kuzozana kwenye kitanda. Kikwai anapokumbuka kumpigia mamake, anampasha taarifa ya harubu walio nayo, angaa awasaidie. Anamweleza kuwa fundi wa nyumba anatishia kutwaa mbuzi wao ili awauze ajilipe deni ambalo limecheleweshwa karibu mwezi mzima. Hii ni harubu nyingine kwa upande wa Kikwai, kwani hana la kuwafaa, ila anaahidi kumtumia hela mwisho wa mwezi akipata mshahara. Kikwai anaamshwa na kilio cha Mercy asubuhi, ambaye analalamikia njaa. Anajiandaa kwenda kazini huku akikumbuka harubu alizokuja nazo Mercy. Mahitaji mengi, mara mafua na meno, mara atie punje za mahindi sikioni au puani na kulazimu kiadi na daktari, hadi sasa anapohitaji sare za shule, kalamu, madaftari, karo na mengine.
Kazini, Nilakosi pia ana harubu yake. Mkataba wake wa miezi miwili unafupishwa kuwa mmoja, na pia anapata matatizo ya nyumba. Mpangishaji wake anatisha kumfungia nyumba kwa kuwa hajalipa kodi, anadhani anataka kumlaghai. Japo Bosi anatoa ahadi kutoa jibu, hafanyi hivyo.
Bosi analalamika kuwa Kikwai hafai kuacha gari la kampuni, ilhali hana pesa za kulitia mafuta. Anamtaka pia kwenda kwake kupeleka mtoto wake hospitalini kwa gari hilo. Siku inayofuata, haji kazini. Kikwai na Nilakosi wanalazimika kutembea kwani hawana hela za kupanda gari. Tatizo kuu la Kikwai ni Mercy ambaye hawezi kuelewa hali ilivyo.
Kikwai anafika nyumbani na kuambiwa kuwa Mercy alikataa kula ugali wenye ladha ya mafutataa. Alibahatika tu kupata ndizi mbili kutoka kwa shangazi yake aliyekuja kuwatembelea. Yanapomzidia, anaamua kwenda kwa Bishop ambaye anawaauni kwa chakula cha siku hiyo.
Nilakosi anazidiwa na kushindwa kabisa kufika ofisini. Kikwai anapofika anapata wito wa Bosi kufika ofisini mwake. Bosi analalamika kuwa anajali pesa kuliko kampuni, eti sababu haji kwa gari la kampuni kwa kukosa pesa za mafuta. Hivyo, anaafutwa kazi na kulipwa mshahara anaodai.
Huu unaondokea kuwa mwisho wa harubu ya maisha, lakini ukawa mwanzo wa nyingine. Analazimika kuishughulikia tawasifu kazi yake ili kuanza kusaka ajira mpya.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:33


Next: Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.
Previous: Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions