Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.

      

Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.

  

Answers


Francis
1. Ndoa
Kuna ndoa kati ya Kikwai na Mama Mercy inayodhihirisha misukosuko tele. Wanapooana, mambo yamenyooka kwani mshahara wa Kikwai unawakimu japo ni mdogo. Kisha Mama Mercy anapata mimba na kujifungua Mercy, anayekuja na mambo yake. Mafua, meno na kutia punje za mahindi kwenye pua na masikio. Sasa anahitaji karo, sare, madaftari na kalamu.
Mama Mercy anaanza kumlalamikia mumewe kila mara baada ya suala la kuchelewa kwa mishahara. Anamlaumu wala haamini anapomweleza hali ilivyo. Anasusia kupika kwa kuwa hakuna chakula wala hapendi kukopa. Kikwai analazimika kumshughulikia mtoto wao, Mercy, mwenyewe.
Ndoa hii pia inadhihirisha umenke. Mama Mercy anashinda nyumbani mchana kutwa lakini Kikwai anapotoka kazini, analazimika kuja kupika. Mama Mercy pia anamfokea kila mara, baada yake kufokewa na Bosi huko kazini.

2. Malezi
Kikwai na mkewe wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kumlea mwana wao, Mercy. Awali, mambo yako sawa hadi anapozaliwa Mercy. Anakuja na mahitaji ya hapa na pale ambayo yanamhanagaisha Kikwai. Mara ana mafua na matatizo ya meno, kasha atie punje za mahindi kwenye pua na masikio na kulazimu miadi na daktari. Sasa anahitaji sare, karo, madaftari na kalamu. Mama Mercy anamtoa Kikwai ofisini akimweleza kuwa mtoto karibu analala. Analazimika kuacha kazi kwenda kumshughulikia. Anapofika, anamshtakia njaa. Analazimika kwenda kukopa chakula na kuja kumpikia. Anamlisha na kumpeleka kulala. Mercy anamwamsha tena asubuhi kwa kilio kingine cha njaa.
Anamwahidi kumnunulia kitu huku akijiandaa kwenda kazini. Anaporudi, anaambiwa kuwa alikula ndizi mbili tu kutoka kwa shangazi, baada ya kukataa ugali wenye ladha ya mafutataa.
Kikwai anamkimbilia Bishop kwa msaada wa chakula kulisha familia yake. Siku inayofuata, anapigwa kalamu, lakini analipwa mshahara wake wa awali. Ananunua chakula kingi na kurejea nyumbani.
Anapikia familia yake na wanapokula, anaanza kuipiga msasa tawasifu kazi, tayari kutafuta ajira nyingine kukidhi mahitaji yao.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:38


Next: Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’
Previous: Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo; (i) Dayolojia (ii) Kinaya

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions