Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo; (i) Dayolojia (ii) Kinaya

      

Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo;
(i) Dayolojia
(ii) Kinaya

  

Answers


Francis
1. Dayolojia
Mazungumzo kati ya Kikwai na mkewe kabla Mercy hajawakatiza kuhusu suala la upishi. Kikwai anapomsaili, mkewe anamweleza kuwa hakupika kwani hakuna chakula na hapendi kukopa.
Mazungumzo kati ya Kikwai na mkewe, Mama Mercy, akimweleza jinsi hali ilivyo ngumu, na kuwa anafaa kuvulia, mambo yatakuwa mazuri. Inatuonyesha ugumu anaopitia Kikwai, migogoro na matatizo ya ndoa.
Kuna mazungumzo kati ya Kikwai na bintiye, Mercy, anapomwamsha asubuhi kwa kilio. Anamshatakia kuwa analia sababu ya njaa, naye anamwahidi kumnunulia kitu ale. Dayolojia hii inatuonyesha matatizo ya malezi na dhiki za maisha ya Kikwai.
Mazungumzo kati ya Kikwai na Bosi kuhusu Nilakosi na kandarasi yake inayokamilika, na pia kuhusiana na gari la kampuni, anapomtaka aende nalo kupeleka mwanawe hospitali, hali ameliacha nyumbani.
Inaonyesha migogoro, udhalimu na matatizo ya kazini. Mazungumzo kati ya Kikwai na Bishop anapoenda kumwomba msaada wa chakula, wakijuliana hali na Bishop kumkidhia haja. Yanaonyesha nafasi ya dini katika jamii na umuhimu wa utu.
Mazungumzo kati ya Bosi na Kikwai anapomfuta kazi, akilalamikia mazoea yake ya kuacha gari la kampuni nyumbani. Anasema kuwa atamwondolea taabu ya kucheleweshwa mshahara kwa kumwachisha kazi. Yanadhihirisha migogoro na udhalimu kazini.

2. Kinaya
Mama Mercy anampigia Kikwai simu kulalamikia mwana yuaelekea kulala. Amehiari kumweka Mercy na njaa hadi babake arudi, badala ya kukopa.
Bosi anamwambia Kikwai kuwa gari la kampuni linafaa kuwepo kwa ajili ya dharura kama inayomkumba ya mwanawe kuwa mgonjwa. Ukweli ni kuwa hii ni shughuli ya kibinafsi.
Bosi anamwambia Kikwai kuwa haoni kwa nini haji kwa gari la kampuni, licha yake kumweleza kuwa hana pesa za mafuta. Anadai kuwa anathamini pesa zaidi ya kampuni, pesa ambazo hata hana!
Bosi anamwambia Kikwai atamwondolea taabu kwa kumwachisha kazi ili asikumbwe na suala la kucheleweshwa mshahara. Ukweli ni kuwa anamweka katika taabu ya kutafuta kazi nyingine.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:41


Next: Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.
Previous: Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions