Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.

      

Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.

  

Answers


Francis
Jamii hii ina imani katika usemi wa kuwa elimu ndio ngao ya maisha. Kila mzazi/mlezi anatia bidii kuvumisha elimu katika maisha ya mwanawe. Wanaamini kuwa mwenye elimu atapata mafanikio katika maisha.
Nyaboke, mamake Sabina, anasoma hadi kidato cha pili anapoambulia uja uzito. Analazimika kuacha masomo kuingilia ulezi. Hatua hii inawakera wazazi wake na kuwakatiza tamaa, kwani waliamini atasoma ili awe mtu wa maana maishani.
Sabina anadhihirisha nafasi ya elimu kwa kutia bidii za mchwa katika masomo. Yuko katika darasa la nane akijiandalia mtihani wa mwisho. Licha ya kazi nyingi anazofanya, bado analazimika kufika shuleni na kuendelea na masomo. Kwa sasa, anajiandalia mtihani, akijua kwamba akifaulu atapata ufadhili katika shule ya upili ya bweni.
Sabina anaanza masomo katika shule ya msingi ya Utubora katika darasa la kwanza akiwa na miaka saba kwa sababu ya ushupavu wake. Anaongoza katika darasa lake kwenye mitihani yote. Licha ya kufiwa na mamake, bibi na babu yake, halegezi kamba masomoni. Analazimika kuishi na Yunuke, mke wa mjomba ambaye anamtesa lakini anazidi kufana masomoni.
Binamu zake Sabina wanasoma katika shule ya upili ya Golden Heart. Wanaonana na Sabina wakati wa likizo tu. Ombati na Yunuke wanaona juhudi za Sabina kuwa kazi bure, lakini hakati tamaa. Nia yake kuu ni kujiunga na shule ya upili ya bweni.
Mwalimu mkuu anamsaidia Sabina kwa kuwaandikia wapishi barua wapokee maziwa yake. Anapata nafasi ya kufika katika mtihani kwa wakati na kuufanya bila tatizo. Matokeo yanapokuja, ndiye wa nane bora nchini. Ombati na Yunuke hawataki kujitenga naye wakati maripota wanapokuja kuwahoji. Kijiji kizima kinajaa habari za ufanisi wake kwa takriban wiki nzima.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:53


Next: Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo; (i) Dayolojia (ii) Kinaya
Previous: Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo; (i) Utamaduni (ii) Usaliti

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions