Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo; (i) Utamaduni (ii) Usaliti

      

Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo;
(i) Utamaduni
(ii) Usaliti

  

Answers


Francis
1. Utamaduni
Jamii inategemea ufgaji na kilimo ili kujiendeleza kimaisha. Sabina analazimika kukama ng’ombe wa mjomba wake, kuwapeleka malishoni na kuuza maziwa sokoni kabla ya kwenda shule. Pia anatakiwa kutapakaza kisonzo shambani. Hata maripota wanapofika kumhoji, yuko kazini kwenye shamba. Anarejea bado akiwa na harufu ya samadi.
Kuna imani katika uganga na laana. Nyaboke anapopatwa na kipele shingoni, anapelekwa kwa mganga anayesema kuwa kimeletwa na laana. Hasemi ilikotoka. Watu wanakisia ni babake aliyemlaani kwa kuzaa kabla ya ndoa na kukataa wanaume wanaomposa wote. Wengine wanaamini ni Ombati kwa kukosa mahari yake. Hata Nyaboke anapofariki na hatimaye wazazi wake kumfuata, watu wanaanza kuambaa familia hiyo wakiamini wamelaaniwa.
Tamaduni za ndoa pia zimesawiriwa. Nyaboke anakataa posa ya wanaume wanaomtaka. Wanawake wanachukuliwa kama raslimali za kuzalisha mahari. Ombati anashukiwa kumlaani Nyaboke kwa kumkosesha mahari anapokataa kuolewa.
Isitoshe, Ombati anaamua kumwoza Sabina baada ya mtihani kutokana na visingizio vya Yunuke vya uzinzi.
Wakwezewatarajiwa wanakuja na kuleta mifugo, huku wakiandaa sherehe za kumlaki bi arusi wao. Wameandaa mapochopocho lakini yanakatizwa na mjo wa maripota.

2. Usaliti
Nyaboke anawasaliti wazazi wake kwa kuambulia uja uzito akiwa katika kidato cha pili. Wamejitolea kwa kila hali kumsomesha huku wakiwa na matumaini yake kuwafaa, yanayowatoka mara anapohimili na kukatiza masomo. ‘Babake’ Sabina naye anamsaliti Nyaboke kwa kumtelekeza baada ya kumpa uja uzito.
Yunuke anamsaliti Sabina. Badala ya kumtunza licha ya kujua ni yatima, anamtesa na kumdhalilisha. Anamlazimisha kukama ng’ombe, kupeleka kisonzo shambani na kuuza maziwa kabla ya kwenda shule. Anamfanyisha pia kazi zote za nyumba. Anapojaribu kusoma usiku, anamzimia kibatari anachotumia.
Anapofanya makosa madogomadogo, anamcharaza bila huruma na pia kumtukana vibaya, kila mara akimkumbusha kuwa yeye ni ‘kiokote’.
Ombati anamsaliti Sabina na Nyaboke pia. Kama mjomba, ni jukumu lake kumlinda na kumtunza Sabina. Badala yake, hafanyi lolote la kumfaa. Anaambia mwalimu mkuu kuwa nyumbani hakuna kazi zozote hali Sabina anatumikishwa sana. Anapanga njama ya kumwoza ili kufidia mahari aliyokosa kutoka kwa mamake, Nyaboke. Huu ni usaliti kwa Nyaboke, ambaye ni dadake. Anafaa kumtunzia mwana.
Binamu zake Sabina pia wanamsaliti. Wanapokuja likizo, wanamzidishia majukumu badala ya kumsaidia. Wanakaa tu na kubarizi huku wakimtumatuma, isipokuwa Mike anayejitolea kwenda naye machungani hata baada ya kuadhibiwa.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 07:57


Next: Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.
Previous: Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina; (i) Sabina (ii) Yanuke

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions