Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina; (i) Sabina (ii) Yanuke

      

Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina;
(i) Sabina
(ii) Yanuke

  

Answers


Francis
i. Sabina
Ni mwenye bidii. Anatia bidii katika masomo na pia katika kazi za nyumbani anazofanya. Kabla ya kwenda shuleni, anatakiwa kukama ng’ombe, kutapakaza kisonzo shambani na kuuza maziwa. Licha ya yote haya, anafaulu vizuri katika masomo yake.
Ni mtiifu. Anafuata maagizo ya Yunuke na kumtii bila maswali. Anatapakaza kisonzo shambani anavyoagizwa na kukama ng’ombe na kuuza maziwa kabla ya kwenda shule. Anapoitwa na Yunuke, anatoka alipo upesi na kuelekea malishoni kuwaleta mifugo.
Ni mkakamavu. Anajitolea kwa kila hali kutimiza azma yake katika elimu. Baada ya kumaliza kazi zake, anatumia mwanga wa kibatari kusoma japo Yunuke anakizima. Licha ya kazi zote, bado anafaulu katika masomo yake.
Ni mwerevu. Akiwa katika umri wa miaka saba, anaungana na wenzake wanaotoka chekechea kwa wepesi wake wa kuelewa mambo. Baada ya matokeo kutoka, ndiye mwanafunzi wa nane bora nchini.
Ni mwenye maono. Hata baada ya mamamke kufariki, anaazimia kutia bidii ili kuwasaidia babu na bibi. Azma yake kuu katika siku za usoni ni kuwa daktari.

Umuhimu wa Sabina
Ni kiwakilishi cha dhiki ambayo watoto yatima hupitia katika maisha baada ya kuachwa na wazazi wao. Kupitia kwake, umuhimu wa bidii na matunda yake yanabainika.
Ametumika kuonyesha umuhimu wa elimu na nafasi yake katika kujenga jamii. Kupitia kwake, nafasi ya wazazi katika malezi na maisha ya wanao inadhihirika.


ii. Yunuke
Ni katili. Anamtumikisha Sabina bila huruma. Anamlazimisha kukama ng’ombe, kupeleka kisonzo shambani na kuuza maziwa kabla ya kwenda shule. Anapokawia kwenye ofisi ya mwalimu mkuu, anamvamia na kumtandika kwa bakora.
Ni mpyaro. Kinywa chake kinadondoka kila aina ya matusi bila haya. Anamwambia Sabina anaandama wanaume kama mamake na anajua matokeo yake. Anamwita mjalaana na baradhuli. Kila mara anamkumbusha kwamba yeye ni ‘kiokote’.
Ni dhalimu. Anatumia uyatima wa Sabina kumtumikisha nyumbani. Sabina anafanya majukumu yote ya nyumba huku yeye ameketi tu na kufurisha shingo. Hata wanawe wanapokuja likizo, hawamsaidii bali kumzidishia dhiki.
Ni mfitini. Anamwambia mumewe kuw Sabina ameanza kuwa na tabia za uzinzi na kumfanya kuandaa mipango ya kumwoza katika umri mchanga.

Umuhimu wa Yunuke
Kupitia kwake, udhalimu unaotendewa matoto mayatima katika jamii unadhihirika. Ni kiwakilishi cha nafasi ya mwanamke katika jamii.
Anadhihirisha nafasi ya ndoa na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii Kupitia kwake, watesi wa wasiojiweza wanapata funzo kuwa wanaowatesa wanaweza kufanikiwa na kuwafaa watesi hao.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:18


Next: Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo; (i) Utamaduni (ii) Usaliti
Previous: Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions