Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’

      

Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’

  

Answers


Francis
Ufaafu wa Anwani ‘Mzimu wa Kipwerere’
Neno ‘Mzimu’ lina maana mbili. Kwanza, sehemu ambapo hufanyiwa matambiko na ambapo huaminika roho za waliofariki huishi, na kivuli cha mtu aliyeaga ambaye huwatokea walio hai. Kipwerere ni jina la mwanamke wa enzi za ujinga anayeaminiwa kuwa na nguvu za kimiujiza.
Jina hili linapatiwa msitu ulio katika kijiji hiki. Kwanza, msitu huo umezungukwa na makaburi pande zote. Lazima uyapite kabla ya kuufikia. Makaburi haya yanazikwa watu maarufu. Ndipo mizimu yao inaishi.
Msitu huu unapatiwa jina la mzimu kutokana na kutisha kwake. Una miti mikubwa iliyokua na kubanana, ikafanya kiza kikubwa. Unaaminika kuwa ulichipuka baada ya Kipwerere kuzikwa hapo. Mwanamke huyu aliaminiwa kuwa na nguvu za miujiza.
Msitu huu pia unaaminika kuwa makao ya mashetani na mizimu. Hivyo, watu hawaruhusiwi kupita hapo saa sita mchana na usiku. Wanaopita hapo wanatishiwa kuwa watatolewa kafara na kuondokea kuwa chakula cha Mzimu wa Kipwerere.
Mzimu huu(msitu) una maajabu yake. Usiku huonekana mwanga wa taa, na pia husikika mazungumzo ya watu. Isitoshe, harufu ya tumbaku na vileo vingine hutoka huko. Majibu ya masuala haya ni kuwa mashetani huzungumza, na pia hutumia mihadarati kama binadamu.
Salihina ndiye kiongozi wa mzimu. Kila kitu kuhusiana na mzimu lazima ahusishwe.
Anasemekana kuwa ndiye anaweza kuwasiliana na mizimu. Wakati wa tohara, matambiko na arusi ndiye hutoa maombi kwenye msitu ili mizimu ikubali masuala hayo yaendelee. Kuingia mzimuni pia kuna masharti yake. Kuna wimbo ambao yasemekana ndio ufunguo wa kuingia humo, na ambao lazima uimbe ndipo mashetani wakukubalie kuingia. Msimulizi anausikia kutoka kwa Salihina na Bishoo wanapoimba na kuingia.
Mwishoni, msimulizi anagundua kuwa Salihina ndiye ‘Mzimu wa Kipwerere’! Ndiye anazungumza huko usiku na mshirika wake, Bishoo. Ndio wanaowasha taa na kuvuta sigara. Wanatumia msitu ule kufanya biashara haramu ya usambazaji wa dawa za kulevya. Sheria zote na imani kuhusiana na msitu huo ni hila tupu.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:32


Next: Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina; (i) Sabina (ii) Yanuke
Previous: “Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions