Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.

      

“Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.

  

Answers


Francis
Ni imani potovu kuhusiana na masuala ya ramli, uchawi, mizimu na masuala ya aina hiyo. Watu wengi wanatishwa na Mzimu wa Kipwerere kutokana na imani za kishirikina. Inaaminika kuwa msitu huo ulikua baada ya Kipwerere kuzikwa hapo, mwanamke anayesemekana kupata shetani aliyefichua damu.
Yasemekana baada ya kuzikwa hapo, mzimu huo unakua. Pia, anaaminika kuwa alikuwa mwanamke wa miujiza.
Mzimu wa Kipwerere pia una miiko yake. Watu hawaruhusiwi kupita pale muda wa jua mtikati au jua likishatua. Pia, hakuna anayeruhusiwa kuingia humo ila wale waitwao wahenga. Yeyote ambaye angefanya hivyo, basi anasemekana kuwa chakula cha mizimu, na atatolewa kafara.
Watu pia wanaamini kuwepo kwa mashetani na mizimu. Watoto wanapochezacheza nja ya msitu ule, wanasikia sauti za chinichini za watu wakiongea. Wazee wanawaeleza kuwa shetani ana mke na mara nyingi wanapozungumza, watoto wao huwa wamelala. Taa inayowaka inahusishwa na mashetani hao, sawa na mnuko wa tumbaku na mihadarati mingine.
Msimulizi anajawa na udadisi kuhusiana na mashetani hawa wanaozungumziwa kila mara. Anaamua kujaribu kuingia msituni na hata ikiwezekana kuwaona kwa macho! Kwake, ni kweli kwamba mashetani hawa wapo. Kuna wimbo unaoaminiwa kuwa ufunguo wa kuingia mzimuni. Anausikia kutoka kwa Salihina na kuuimba kisha kuingia. La kushangaza ni kuwa hamwoni shetani yeyote anavyotarajia.
Anagundua kuwa Salihina ndiye anaendesha shughuli zote wanazoshuhudia msituni humo.
Salihina na Bishoo wanatumia itikadi na imani potovu kuchuuza mihadarati. Bishoo anamweleza mpango wake wa kusafirisha dawa hizo kwa kubeba ndoo wanazodai kuwa wanaenda kuchotea shetani wa mzimu maji. Hata polisi wenyewe wanawaruhusu! Ndoo hizo hatimaye zinajazwa ‘mzigo’; mihadarati.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:35


Next: Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’
Previous: Eleza migogoro inayojitokeza katika hadithi ya ‘kila mchezea wembe’.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions