Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza migogoro inayojitokeza katika hadithi ya ‘kila mchezea wembe’.

      

Eleza migogoro inayojitokeza katika hadithi ya ‘kila mchezea wembe’.

  

Answers


Francis
Nia kuu ya Tembo ni kumwomba msamaha mkewe kwa migogoro yao ya awali. Anakumbuka malalamishi yake mara ya mwisho anapokuja kumwona. Analalamikia tabia yake ya kupotea kila mara, tena hafanyi lolote kwa ajili ya familia yake. Hata anamwomba ampe talaka, yuko tayari kuwatunza watoto, kwani amezoea tayari. Tembo anatamani angepata uwezo wa kumwomba radhi wakati huo.
Anakumbuka siku ya maangamizi. Mkewe anamwamsha mwendo wa saa nne ilia apate staftahi. Anamaliza kuamsha kinywa saa sita. Anaambiwa mkewe anachoma mahamri jikoni lakini anaondoka bila kuaga. Anahofia kujibu maswali kuhusu wapi aendapo.
Walijipata tena kwenye mgogoro baada yake kurudi nyumbani siku iliyofuata. Mkewe anamwandalia chamcha, naye anavua mavazi na kujitupa kitandani. Anasikia ukemi wa mkewe, huku ameshika nguo zake zenye alama za rangi ya midomo. Anajua ana maswali ya kujibu lakini hali yake hairuhusu. Mkewe anamshughulikia kupata matibabu.
Tembo pia anajikuta kwenye mgogoro na Angelica kwenye chumba chake anapogutuka. Hajui kafikaje humo, tena Bikizee huyu anatakaje. Anatamani kutoroka lakini hana namna. Anji anadai malipo kwa huduma zake. Analazimika kuzoa salio la mshahara wake kwenye soksi na kumpa ili kujiopoa. Anji anasema atampeza lakini Tembo hanuii kuwahi kuonana naye tena. Analazimika kutembea hadi nyumbani, mwendo wa saa nzima.
Emmi anapomtembelea pia, analalamikia migogoro ya mumewe. Anapolewa anarudi nyumbani na maudhi, matusi na vipigo tu. Analalamika kuwa hawaheshimu yeye na watoto wake, wazazi wala wakwe, na hata majirani.
Tembo pia ana mgogoro na familia yake. Hana ukuruba na wazazi wake. Dada na kaka zake wanamtema anapozua vurugu kwenye maziara wakati wa mazishi ya mpwa wake. Hivi, hapati watu wa kumtembelea hospitalini kama rafikiye Salim.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:45


Next: “Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.
Previous: Fafanua masuala ibuka yafuatoyo katika hadithi ya Kila Mchezea Wembe; (i) Ulevi (ii) Starehe na anasa (iii) Mapenzi na ndoa

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions