Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Suluhu ina maana ya kusawazisha mambo ili yawe sawa. Pia inaweza kumaanisha kuwa na nguvu sawa. Mada ‘Kifo cha Suluhu’ inaweza kufasiriwa kwa maana tofauti.
Kwanza, kuna mhusika kwa jina la Suluhu. Mada hii inaweza kufasiriwa kurejelea kifo chake. Abigael ananuia kumwua Suluhu ili kulipiza kisasi kwa kumtumia kama tambara bovu na pia ampore pesa zake. Amebeba dawa ya kumtia usingizi na kisu cha makali kuwili kumwangamiza. Kifo hicho hakitukii kwani Abigael anaghairi nia. Anaona kuwa kifo hicho hakitakuwa na maana yoyote baada ya kusoma barua ya Bi. Suluhu. Anamwacha Suluhu usingizini na kuondoka kurudi chuoni.
Mada hii pia inaweza kufasiriwa kwa maana ya kifo cha kusawazisha mambo, yaani kifo cha kuleta suluhu. Natasha na Abigael wanakiona kifo cha Suluhu kuwa suluhu kwa tatizo lao la hela. Abigael anataka kumwua kisha kupora mali yake.
Bi. Suluhu anaona kuwa kifo chake kitakuwa kifo cha suluhu. Kwanza, kitakuwa kikomo cha tabu alizopitia maishani. Pia anasema ni suluhu iwapo kitamwezesha mumewe kurudi kuwashughulikia wanao.
Suluhu anapanga kumshawishi Abigael awe mkewe wa pembeni baada ya kuwazia jinsi ya kumwangamiza mkewe. Anakiona kifo cha mkewe kuwa cha suluhu kwa kuwa kitamwezesha kuwa na Abigael.
Abigael anaposoma barua ya Bi. Suluhu, anaona kuwa kifo cha Suluhu sio suluhu ya aina yoyote. Kifo cha kuleta suluhu ni kifo cha maovu yote katika jamii na waja kukumbatia utu.
Suluhu anamwangamiza mamake Abigael akihofia kuwa atamchukulia hatua ya kisheria baada ya kunyakua shamba lake. Kwa Suluhu, hiki ni kifo cha suluhu, kwani kitamwezesha kumiliki shamba hilo bila matatizo.
Mada hii pia inaweza kutoa maana ya suluhu yenyewe kufa, yaani nia ya kusawazisha mambo kufeli. Kwa mfano, wananchi wanamchagua Suluhu kuwasaidia. Wanamwona kama suluhu ya shida zao. Hata hivyo, kifo cha suluhu yao kinatokea Suluhu anapozamia uzinzi na kuwatelekeza.
Abigael anapania kumwua Suluhu na kupoka pesa zake, jambo analoliona kama suluhu ya shida zake. Hata hivyo, suluhu hii iliyopendekezwa na Natasha kwa shida zao inakufa baada ya Abigael kusoma barua ya Bi. suluhu, inayomfanya kughairi nia ya kumwua Suluhu.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:59
- Fafanua masuala ibuka yafuatoyo katika hadithi ya Kila Mchezea Wembe;
(i) Ulevi
(ii) Starehe na anasa
(iii) Mapenzi na ndoa(Solved)
Fafanua masuala ibuka yafuatoyo katika hadithi ya Kila Mchezea Wembe;
(i) Ulevi
(ii) Starehe na anasa
(iii) Mapenzi na ndoa
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza migogoro inayojitokeza katika hadithi ya ‘kila mchezea wembe’.(Solved)
Eleza migogoro inayojitokeza katika hadithi ya ‘kila mchezea wembe’.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- “Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.(Solved)
“Itikadi na ushirikina ni visa ambavyo vimekithiri katika jamii. Thibitisha kulingana na hadithi ya Mzimu wa kipwerere.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’(Solved)
Eleza ufaafu wa anwani ‘ Mzimu wa kipwerere’
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina;
(i) Sabina
(ii) Yanuke(Solved)
Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Sabina;
(i) Sabina
(ii) Yanuke
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo;
(i) Utamaduni
(ii) Usaliti(Solved)
Fafanua namna mwandishi wa Sabina ameangazia masuala yafuatayo;
(i) Utamaduni
(ii) Usaliti
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.(Solved)
Elimu ni nguzo muhimu katika maisha. Fafanua ukweli wa kauli hii kama inavyotumika katika hadithi ya Sabina.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo;
(i) Dayolojia
(ii) Kinaya(Solved)
Mwandishi wa Harubu ya Maisha amefanikisha vipi matumizi ya mbinu zifuatazo;
(i) Dayolojia
(ii) Kinaya
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.(Solved)
Fafanua namna mwandishi ameangazia maudhui ya ndoa na malezi katika hadithi ya Harubu ya Maisha.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’(Solved)
Huku ukitolea mifano mahususi, eleza ufaafu wa anwani ‘Harubu ya Maisha’
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.(Solved)
Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi ya mapambazuko ya machweo.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo.
i. majazi
ii. kinaya
iii. jazanda(Solved)
Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi ya mapambazuko ya machweo.
i. majazi
ii. kinaya
iii. jazanda
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.(Solved)
Eleza maudhui makuu ya hadithi, Mapambazuko ya Mchweo.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.(Solved)
Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia
i. Sugu Junior
ii. Machoka
iii. Zuhura(Solved)
Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya msiba wa kujitakia
i. Sugu Junior
ii. Machoka
iii. Zuhura
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia.(Solved)
Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Jadili maudhui yoyote matatu yanayojitokeza katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia(Solved)
Jadili maudhui yoyote matatu yanayojitokeza katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda ameagazia vipi suala la migogoro katika jamii.(Solved)
Mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda ameagazia vipi suala la migogoro katika jamii.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda(Solved)
Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi ya Fadhila za Punda
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda(Solved)
Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Fadhila za Punda
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)