Eleza Ufaafu wa Anwani ‘Kifo cha Suluhu’.

      

Eleza Ufaafu wa Anwani ‘Kifo cha Suluhu’.

  

Answers


Francis
Suluhu ina maana ya kusawazisha mambo ili yawe sawa. Pia inaweza kumaanisha kuwa na nguvu sawa. Mada ‘Kifo cha Suluhu’ inaweza kufasiriwa kwa maana tofauti.
Kwanza, kuna mhusika kwa jina la Suluhu. Mada hii inaweza kufasiriwa kurejelea kifo chake. Abigael ananuia kumwua Suluhu ili kulipiza kisasi kwa kumtumia kama tambara bovu na pia ampore pesa zake. Amebeba dawa ya kumtia usingizi na kisu cha makali kuwili kumwangamiza. Kifo hicho hakitukii kwani Abigael anaghairi nia. Anaona kuwa kifo hicho hakitakuwa na maana yoyote baada ya kusoma barua ya Bi. Suluhu. Anamwacha Suluhu usingizini na kuondoka kurudi chuoni.
Mada hii pia inaweza kufasiriwa kwa maana ya kifo cha kusawazisha mambo, yaani kifo cha kuleta suluhu. Natasha na Abigael wanakiona kifo cha Suluhu kuwa suluhu kwa tatizo lao la hela. Abigael anataka kumwua kisha kupora mali yake.
Bi. Suluhu anaona kuwa kifo chake kitakuwa kifo cha suluhu. Kwanza, kitakuwa kikomo cha tabu alizopitia maishani. Pia anasema ni suluhu iwapo kitamwezesha mumewe kurudi kuwashughulikia wanao.
Suluhu anapanga kumshawishi Abigael awe mkewe wa pembeni baada ya kuwazia jinsi ya kumwangamiza mkewe. Anakiona kifo cha mkewe kuwa cha suluhu kwa kuwa kitamwezesha kuwa na Abigael.
Abigael anaposoma barua ya Bi. Suluhu, anaona kuwa kifo cha Suluhu sio suluhu ya aina yoyote. Kifo cha kuleta suluhu ni kifo cha maovu yote katika jamii na waja kukumbatia utu.
Suluhu anamwangamiza mamake Abigael akihofia kuwa atamchukulia hatua ya kisheria baada ya kunyakua shamba lake. Kwa Suluhu, hiki ni kifo cha suluhu, kwani kitamwezesha kumiliki shamba hilo bila matatizo.
Mada hii pia inaweza kutoa maana ya suluhu yenyewe kufa, yaani nia ya kusawazisha mambo kufeli. Kwa mfano, wananchi wanamchagua Suluhu kuwasaidia. Wanamwona kama suluhu ya shida zao. Hata hivyo, kifo cha suluhu yao kinatokea Suluhu anapozamia uzinzi na kuwatelekeza.
Abigael anapania kumwua Suluhu na kupoka pesa zake, jambo analoliona kama suluhu ya shida zake. Hata hivyo, suluhu hii iliyopendekezwa na Natasha kwa shida zao inakufa baada ya Abigael kusoma barua ya Bi. suluhu, inayomfanya kughairi nia ya kumwua Suluhu.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 08:59


Next: Fafanua masuala ibuka yafuatoyo katika hadithi ya Kila Mchezea Wembe; (i) Ulevi (ii) Starehe na anasa (iii) Mapenzi na ndoa
Previous: Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions