Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.

      

Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.

  

Answers


Francis
Katika hadithi, tunashuhudia ndoa kati ya Suluhu na mkewe ambayo imejaa misukosuko. Abigael anasema kuwa mkewe Suluhu hana amani katika ndoa yake licha ya mali tele ya mumewe. Anapigwa na maisha na kukonda, hata kuonekana mzee kuliko umri wake. Ana wasiwasi kuhusu aliko mumewe mara kwa mara.
Barua ya Bi. Suluhu inaonyesha uchungu wake katika ndoa isiyo na sitara. Suluhu anamwacha mkewe na kuandama anasa na wanafunzi wa vyuo vikuu. Hata watoto analazimika kuwalea peke yake. Bi. Suluhu anamkumbusha makubaliano yao wakati wa kufunga ndoa, ambayo mumewe anayapuuza.
Bi. Suluhu anaonyesha pia thamani ya ndoa ya kuweka siri kwa kumhakikishia mumewe kuwa hajawahi wala hatatoa siri zake anazojua. Hatasema kuwa alishindwa kuleta maendeleo kwa sababu ya kufuja pesa akiwalipa wasichana kwa ajili ya uroda, na pia kumfidia Bwana Ngoma hela alizomkopesha akifanya kampeni. Hatasema kuwa ndiye alimuua mama Abigael baada ya kunyakua shamba lake.
Bi. Suluhu anasema yuko tayari kufa na kifo chake kitahesabiwa haki. Amechoka na dhuluma za mumewe, ambazo zinamwumiza pamoja na wanawe. Anamshukuru kwa ghiliba kwa wazazi. Aliwatendea mengi kuwahakikishia kuwa anampenda.
Isitoshe, anamwona Suluhu kuwa sababu ya kifo chake. Hili ni kutokana na upweke anaomwachia na mawazo mengi.
Anapomtembelea daktari anaambiwa kuwa afya yake iko sawa ila mawazo tu.
Anamkumbusha anathamini mapenzi yao, ndio maana hakuwahi kumdhuru japo angeweza kumsumisha.
Anakiona kifo chake kuwa cha suluhu kwa kuwa kitamwezesha mumewe kurudi kuwatunza wanao. Anamtaka kumkoma Abigael asije akamwambukiza nakama. Anahisi kuwa muda wa kujuta kila mara unaelekea tamati. Barua hii inamfanya Abigael kujuta kwa kuingilia ndoa ya Suluhu na mkewe.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 09:16


Next: Eleza Ufaafu wa Anwani ‘Kifo cha Suluhu’.
Previous: “Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions