“Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.

      

“Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.

  

Answers


Francis
Suluhu na Abigael wamekuwa wapenzi kwa muda mrefu. Wanapatana katika mambo mengi. Hata hivyo, Aigael anabadilika na kunuia kumwangamiza Suluhu. Suluhu hana habari kuwa Abigael anaweza kubadilika kiasi cha kutaka kumtoa uhai.
Suluhu anaponuia kumwoa mkewe, anajitolea kuwasaidia wazazi wake kwa kila hali. Anamfurahisha mkewe pia. Baada ya ndoa, anamtelekeza mkewe kabisa na hata kumwachia majukumu yote ya malezi. Anazurura huku na huku akila uroda na wanafunzi wa vyuo vikuu.
Hali ya Suluhu ya kiuchumi pia inabadilika. Awali, anapata riziki kwa kuuza makaa. Anabadilisha hali hii kwa kumkopa pesa Bwana Ngoma na kujitoma katika siasa na kutwaa uongozi. Anaanza kuishi kifalme.
Baada ya Abigael kusoma barua ya mkewe Suluhu, anaghairi nia ya kumuua Suluhu kama alivyodhamiria. Anaona kuwa kifo hicho hakitaleta mabadiliko yoyote, bali kifo kinachofaa ni kifo cha maovu katika jamii. Pia anaonelea kuwa hakimu wa kweli ni Mungu tu.

francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 09:22


Next: Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.
Previous: Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu; (i) Kinaya (ii) Barua

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions